Bondia Maneno Oswald akitangazwa baada ya kumdunda Rashid Matumla.
Matumla akisulubiwa jukwaani wakati wa mpambano huo.

MPAMBANO wa ndondi baina ya mabondia Maneno Oswald na Rashid Matumla ambao ulifanyika ukumbi wa maraha wa Dar Live Mbagala, jijini Dar es Salaam, katika kuadhimisha sikukuu ya Idd el Fitr, ulishuhudia Oswald akimchakaza Matumla kwa pointi.

Mbali na mpambano huo uliofanyika usiku wa kuamkia leo, kulikuwa pia na burudani za aina mbalimbali, likiwemo disko la watoto ambao pia walifurahia kuogelea katika bwawa maalum na michezo mingine mingi. Kwa upande wa muziki kulikuwa na shoo kali zilizofanywa na wanamuziki Juma Nature, Mwasiti Almasi, Estelinah Sanga ‘Linah’, Maunda Zorro na kundi zima la Jahazi Modern Taarab likiongozwa na mfalme, Mzee Yusuf.

(Picha: Musa Mateja na Richard Bukos/GPL)
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Huyo Matumla na kitambi chote hicho jamani. Hizi ngumi jamani nzito acheni umri umeshaenda.

    ReplyDelete
  2. Che GUevaraAugust 21, 2012

    Matumla kwishiney! Achana na makonde sasa, jaribu kazi nyingine hata kubeba mizigo itakulipa

    ReplyDelete
  3. mambo ya aibu kuingia ulingoni na shepu kama hii.Watu tugome kwenda kulipia ngumi za wanamasumbwi ambao wanaganga njaa ambao hawako makini na kazi zao. Huyu jamaa ameenda kupigania uzoefu tu

    ReplyDelete
  4. matumla umezidi bora ulivyobondwa, pumzika sasa kila kitu kina mwisho eboh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...