Mambo mzee habari za siku. MC Catunda hapa...Mie mzima, pole na kazi. Pokea picha toka Songea ambapo kundi la Wamarekani 18 kwa kushirikiana na Mwangaza Jitegemee USA tuliweza kuwaleta wahisani toka Woodville Alliance Church ya Seattle, Washington, ambapo walishiriki katika shughuli mbali mbali za kusaidia kituo cha kulelea watoto yatima cha SWACCO kilichopo Songea mjini ikiwemo kutoa misaada ya madawa ,vitabu nguo,pamoja na kujenga nyumba za akinamama wasiojiweza ...Vile vile wameahidi kuja kuanza mara moja ujenzi wa kituo kikubwa cha watoto hao kitakachokuwa na huduma zote za kijamii ambapo uzio wa mradi huo umeshakamilika mpaka sasa.
wakifurahi na wenyeji wao katika ngoma ya lizombe
kundi la Woodville Alliance Church toka Marekani wakiwa katika picha ya pamoja na wenyeji wao
tukishiriki katika ujenzi wa nyumba za wasiojiweza
watoto wakifurahi mabegi ya shule
MC Katunda toka Mwangaza jitegemee USA pamoja na woodvile alliance church wakiwafariji watoto yatima kwa misaada mbali mbali
Matt Hesselgrave mkandarasi akimfariji mama Leodard ambaye ni mlemavu baada ya kujengewa nyumba ya kisasa na wataalam hao wa woodvile church kwa kushirikiana na Mwangaza jitegemee USA


Una waona hao binadamu ?? huko kwao pengine hata nyumba hawana , wamepanga ,lakini moyo wa kutoa wanao ,kuja kuwajengea nyumba wengine !!!!! sisi mpaka zibaki ndipo tutoe msaada.Tangu lini hela zikabaki ???? Zebedayo msema kweli
ReplyDeletehongera catunda , kweli na mimi natamani siku moja nifanye kitu kama hiki kwa jamii, ishallah nitaweza tuu mbona katunda ameweza?
ReplyDeleteNingependa hawa Wamarekani wanifahamishe wapi wamepata haya mabegi, kwa kuwa yanatumika kwa shule za Kijapani tu. Nimeishi Marekani na sijaona wanafunzi wao wanayatumia. Huwa watoto wa darasa la kwanza mpaka sita wanatumia haya na yanagharimu USD250 kwa kuwa ni magumu na yanatumika miaka sita bila kuchanika. Jekundu kwa wasichana na Jeusi kwa wavulana.
ReplyDeleteNimefurahi watoto wetu wamepata mabegi haya, ni magumu sana, yatawasaidia.