Maharusi wakikata keki kwenye sherehe iliyofanyikia Kiramuu Hall Mbezi Beach hivi karibuni
 Maharusi wakiwa katika picha ya pamoja na wapambe wao.
Maharusi (Elihuruma Ngowi na my wife wake) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wazazi wao mara baada ya kufunga pingu za maisha hivi karibuni.
 Maharusi wakiingia ukumbini Kiramuu Mbezi Beach huku wakicheza wimbo wa Christina Shusho uitwao “Mungu akiwa upande wetu” 
Maharusi wakiwa kwenye picha ya pamoja na wasimamizi au washauri wao Bwana na Bibi Paul Mashauri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Siku hizi harusi imekuwa ni biashara kubwa tu,Yaani Mie sipendi harusi za kifahari zenye gharama kubwa kwa kulazimisha watu wachange,sioni sababu ya mtu unaalikwa harusi halafu uichangie kabla ya kwenda,yaani ni kama unalipia gharama ya kwenda kusheherekea!Kwakweli haipendezi kabisaaaaaa!Kama mtu hauna uwezo wa kufanya harusi kubwa basi nendeni na mashahidi wenu aidha kanisani au msikitini mkafunge ndoa hiyo tosha kabisa,Lakini msilazimishe watu wawachangie kwa kufanya sherehe kubwa ya siku moja isiyokuwa na faida yeyote kwenu!Watu jaribuni kubadilika mchangie maendeleo lakini sio upuuzi na sherehe zisizokuwa na maana,kwa mfano changieni watoto wasiokuwa na uwezo wa kusoma,changieni wagonjwa wasiokuwa na uwezo wa kutibiwa n.k.

    ReplyDelete
  2. Mdau wa kwanza hapo juu umepiga Pentagon Makao Makuu!

    Ni hulka mbaya sana kuegemea anasa bila kuwa na uwezo.

    Ni vema anayetaka Sherehe ya anasa atumie fedha zake kuandaa halafu na awaalike awapendao ili wakafanye sherehe.

    Hiki kitu kimechangia sana kuwarudihsa watu kimaisha, kwa kuwa maisha yanaheshimu 'economic law'(sheria ,kanuni za kiuchumi) na zaidi haswa kuishi aina ya maisha kulingana na uwezo mtu ulio nao, pia kuzingatia 'life preferences'(vipaumbele).

    Haiwezekani mfano mzazi unawajibika kumwandaa mtoto mwanafunzi kwa Muhula wa masomo huku ukiwa na hela ya ngama, halafu ushinikizwe kuitoa fedha hiyo kwenye mchango wa Harusi,,,ina maana ukifuata shinikizo hilo ni wazi mwanafunzi hataweza kwenda shule masomoni.

    PANA MIFANO MINGI INAYOENDANA NA KWA KUTOZINGATIA HAYA MAWILI:

    1.KUDHARAU 'ECONOMIC LAW' ILIVYO
    2.KUTOFUATA MAISHA YA 'PREFERENCES'

    IMEBAKI WATU WANAKUFA NA TAI SHINGONI, WATU WANAISHI KWA KUOGOPANA HUKU WAKIWA DUNI KIMAISHA NA KAMA UKIKATAA ETI UNANUNIWA NA UNATENGWA!!!

    ReplyDelete
  3. HII NI TRADITION YETU KUONYESHA SISI WATANZANIA TUNAPENDANA KWENYE SHIDA NA FURAHA PIA.KWA HIYO MDAU HAPA JUU USITULEE USENGE WAKO HAPA WEWE.

    ReplyDelete
  4. Kweli kabisa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...