Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akikabithi fomu za kugombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC kwa Katibu wa UVCCM mkoani Mwanza,Bw Elias Mpanda katika ofisi za CCM mkoa. Jijini Mwanza. Mstahiki meya Manispaa ya Ilala Bw Jerry Silaa anagombea nafasi ya ujumbe wa UVCCM-NEC ngazi ya taifa.Mstahiki meya aliweka wazi nia yake ya kutaka kuwawakilisha vema vijana wa kitanzania kwenye UVCCM-NEC na aliwaasa vijana wengine kushiriki kwenye mchakato huo na huku akisisitiza kwamba yuko tayari kufanya kazi kokote nchini kwa maslahi ya wananchi, vilevile meya aliwaasa viongozi wote kuwajibika na kutimiza ahadi zao walizozitoa kwa wananchi na kwa kuweka mbele maslahi ya taifa na sio yao binafsi.
Home
Unlabelled
Meya wa Ilala arudisha fomu za kugombea nafasi ya mjumbe wa NEC - UVCCM
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


Huyu mtoto wa Dr. Slaa au ndugu yake???
ReplyDelete