Bondia Mohamed Bonzo (63yrs) akitoa nasaha baada ya kumpiga bondia chipukizi James Martin (22) ambae ni sawa na mwanae wa tatu.upande wa kulia ni Ibrahim kamwe na kushoto ni Yasin Abdallah-Ustadh.
Bondia Mohamed Bonzo (63) inasemekana ndio bondia mzee nchini atacheza siku ya iddi mosi.
Kampuni ya Mwanzoa Promotions ya Tanga chini ya mkurugenzi wake Ally mmar inaendeleza mkakati wake wa kunyanyua vipaji vya wanamichezo wa jiji la Tanga hasa katika mchezo wa ngumi kwa mapambano ya ubingwa wa Afrika mashariki yatakayopigwa siku ya iddi mosi na iddi pili.
Ally omar’Mwazoa’ akikimuhakikishia katibu mkuu wa ngumi za kulipwa nchini Ibrahim kamwe”bigright” kuwa maandalizi ya mapambano yote yamekamilika na mabondia wapo katika hali nzuri ya ushindani ambapo siku hiyo ya iddi mosi katika ukumbi wa CCM HALL, Said mundi wa Tanga atazipiga na Habibu pengo wa Dar es salaam katika kugombania ubingwa wa Taifa wa TPBC uzito wa super feather raundi kumi.
nae jumanne Mohamed wa Tanga atazipiga na ali bugingo wa Dar es salaam uzito wa light weight raundi kumi,katika uzito wa super fly Haji juma (Tanga) na Mwaite juma (Dsm) watacheza raundi nane na mapambano mengineyo mengi ya utangulizi wa mabondia wa watakaotoka katika vitongoji mbalimbali vya jiji la tanga.
Na siku ya idi pili katika ukumbi wa pweza kutakuwa na pambano kubwa la ubingwa wa Afrika mashariki na kati, kati ya Alen Kamote wa Tanga na bondia toka Uganda ni pambano la raundi kumi pia zuberi kitandula wa Tanga atazipiga na Sadiki Abdul azizi wa Dar es salaam raundi kumi.
jay jay ngotiko wa tanga atapigana na bondia juma afande toka morogoro pia kutakuwepo na mapambano mengi ya utangulizi ya mabondia wakongwe wa tanga na wale chipukizi takribani mabondia wote wa kulipwa wa jiji la Tanga watashindana hakuna atakaekosa kazi labda awe na matatizo binafsi.
mwazoa alimalizia kwa kusema hizi ni mbio za kuyakusanya mataji yote ya Tanzania na Afrika mashariki yaje mkoani Tanga na tayari mpaka sasa ina mabingwa sita wa Tanzania na mmoja wa Afrika mashariki.
Jamani jamani msije mkatulia hao wazee bure sababu ya njaa zenu bureee.
ReplyDeleteI like that tatoo, it could be almost anything!!!
ReplyDeleteUtakufa wewe hebu tulia umeshazeeka.
ReplyDeletewe nyamaza kabisa hapo juu, eti njaa ,mtu yuko fiti kabisa huyu alitakiwa atangazwe kwenye BBC na CNN na akaonane na waandishi wa kitabu cha gueness ili awekwe kwenye record-haki ya nani ,huyu mtu anasitahili sifa . wewe unayemuita mzee, kambake mwanae ukione cha moto, fala mkubwa weye. Zebedayo msema kweli
ReplyDeleteTafuta msala ulipo baba!!
ReplyDeleteFedha fedheha!
ReplyDeleteAndaeni Ambulance kwa kubeba mgonjwa mahututi!
Asije huyu mzee akafia Ulingoni, chezea damu changa weye?
Duh huyu BBB Bonzo Boxer Bandari ni wa zamani sana.Amenikumbusha mabli sana wakati nikiwa mdogo pale kwenye uwanja wa mkwakwani.Dah mabondia kama kina Mambea Bakari Master na akina Abeid Makubeli.Pia kulikua na chipukizi km kina Magoma Shaban ambae baadae alikuja kutamba sana,Akina Fadhili Kea,Haji Pera na wengine wengi.Ila kati ya wote Mambea Master chini ya kocha Charles Spencer alikuwa bondia mzuri sana.Huyu mzee Bonzo apumzike bco alikua mlevi sana baade so cjui km afya yake bado inaruhusu.
ReplyDeletenjaa bwana kitu kibaya. hivi huyo mzee mbona hatujawahi kumsikia akipigana kwenye ujana?
ReplyDelete