Mwenyekiti wa Kijiji cha Emairete, Moran Poyoni, akimkabidhi zawadi ya fimbo maalumu Mgeni rasmi Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo, wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorijo, yaliyokarabatiwa na Kampuni ya Samsung na kutangaza msaada wa milioni 144 kwa shule hiyo na Sekondari ya Winning Sprit Monduli Arusha jana.
 Mama wa Kimasai akimpa zawadi Dada wa Kikorea wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorijo baada ya ukarabati uliofanywa na Kampuni ya Samsung na kutangaza msaada wa Sh. milioni 144 kwa shule hiyo na Sekondari ya Winning Sprit Monduli Arusha jana.
 Wakinamama wa Kimasai wa Kijiji cha Emairete Wilayani Monduli, wakimkabidhi zawadi ya Mbuzi, Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorijo.
Makamu wa Rais wa Samsung, Choi Woo-Soo akiwa katika vazi la Kimasai huku akionyesha zawadi ya fimbo maalum aliyokabidhiwa wakati wa hafla ya kukabidhi madarasa kwa shule ya Irmorij.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwani huku Arusha tu ndio watu wanasoma kuna na mikoa mengine in wasiojiweza na wanahitaji elimu hamuoni aibu

    ReplyDelete
  2. mdau wa kwanza...hata mimi nashangaa, tena kuna mingine ipo karibu tu na hapo kama suala ni umbali na imechoka kweli...enewei hiyo naona baada ya miaka kadhaa huo mkoa utakuwa ni nchi pekee....ni mawazo yangu tu jamani!

    ReplyDelete
  3. Yaani Wadau hapo juu! Ni sawa na mtu akape pipi unasema unataka a ya mumeo au mkeo. Shukuru kwa hicho kidogo uluchopewa nendeni huko mnakona bado zinahitajika nanyi mfanye jambo msikae tu maneno matupu!
    Kweli sasa naona sifa ya "baadhi" ya waTZ! Midomoooooooooooooooooooo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...