Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhimiza masuala mbalimbali ya maendeleo ya mkoa na zoezi la Sensa ya watu na makazi itakayofanyika nchini Agosti 26, 2012.
Na. Aron Msigwa -MAELEZO
Dar es salaam.
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa zoezi la Sensa ya watu na makazi nchini, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa mkoa huo kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa watakaoendesha zoezi hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema maandalizi ya ukamilishaji wa zoezi hilo yanaendelea vizuri na kuongeza kuwa Waziri mkuu Mizengo Pinda anatarajia kuzindua kampeni ya uhamasishaji wa watu kushiriki katika zoezi hilo kesho (17/8/2012) katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...