Shamba la mitiki 300 yenye miaka 14 linauzwa Hale Tanga. Bado miaka chini ya kumi tu kuvunwa.  Lina ukubwa wa eka 2 yenye mitiki katika shamba la eka 15.  Linafaa kwa dhamana kwa mtu anataka kuombea mkopo Benki. Bei ni $65000. Lakini maelewano yapo. Thamani ya mtiki mmoja kwa kutathmini kwa mkopo ni zaidi ya $250.

CONTACTS:
SIMU 0762560088

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. What valuation is that, hiyo ni ya benki gani? $250 per tree.

    ReplyDelete
  2. E bwana ,ama kweli watu mnadhamanisha ardhi etc . siku hizi huko bongo,yaani bila ya kuwa fisadi hapo bei hiyo mbongo wa kawaida hawezi kabisa kununua ,bei ni kubwa kuliko huku ughaibuni.Acheni kuwa wababaishaji namna hiyo ,hata bei za viwanja na nyumba ama kweli huko bongo siku hizi zinakatisha tamaa ,halafu huduma zenyewe ndiyo hizo ,umeme mgao ,maji hamna na usalama mdogo ,yaani majambazi kibao ,hivyo ni bora nikiwa na fedha kununua huku huku ughaibuni .Halafu badala ya kuweka thamani ktk Tshs. unataka dollar ,whatsupp?Mdau big Joe

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Pili.

    Kwani bei ya EQUIVALENT shamba huko ughaibuni ni kiasi gani?
    Lazima bei za nyumba/viwanja zipande kwa sababu VALUE ya "huku bongo" imepanda au kwa maneno mengine thamani yetu inapanda, do you have a problem with this?

    Suala la hizo huduma zingine ulizozitaja haviingilani kabisa na hili tangazo la biashara hapa.

    ReplyDelete
  4. Mdau wa kwanza unashangazwa na bei ya $65,000? Mbona hiyo ni cha mtoto siku hizi bongo? Nenda jijini dar uliza bei ya kiwanja kidogo tu cha 20 X 25 utasikia milioni 800. Nenda pia miji ya mikoa mfano moro, moshi, arusha, kakiwanja kama hako utasikia milioni 300. hizo ndizo faida na hasara za kuukaribisha uwekezaji toka nje. Maana kama muwekezaji atatoka kwao ambapo bei ya kiwanja ni dola 200 halafu aje bongo umuuzie kiwanja kwa dola 3000, haiingii akilini, ni kama umempa bure.

    ReplyDelete
  5. Mdau wa tatu nadhani haunielewi /au haujaelwwa comment yangu.Nadhani mimi nacomment kiujumla na mtazamo mkubwa siyo kwangu peke yangu tu bali kwa maslahi ya wananchi walio wengi.Bei hizi ni za kukurupuka sana na mwananchi wa kawaida bila ya kuwa fisadi au mwizi hataweza kununua kiwanja au shamba au nyumba huko.Bei hizi ambazo hata hamtaki kutumia Tshs mnaweka dollar ni kubwa kuliko ughaibuni na kwa mtu aliyetembea kama mimi au wadau wengine waliotembea kama mimi ,watakubaliana nami kabisa ,hizi bei siyo kama ardhi imepanda thamani ,bali TSH imeshuka thamani kwa sana na serikali isipoangalia jambo hili ,tunaelekea kwenye Inflation ambayo kuna kipindi watu inabidi wawe wanatembea na mabegi au viroba vya fedha ili kupata mahitaji ya kawaida.Inasikitisha sana kuona hivi.Mdau big Joe

    ReplyDelete
  6. Ughaibuni unauziwa kiwanja kwa miaka mia, halafu urudishe. Bongo unauziwa maisha.

    ReplyDelete
  7. we mdau wa pili acha ushamba... kila saa "huko bongo... huko bongo" sema nyumbani.

    na kama tukiuza vitu zaidi ya ughaibuni inahusu nini, isitoshe ni maendeleo....

    comment zako zimejaa umbea umbea na ushamba mwingi.... umenichefua kusema kweli.

    Achana na kasumba... kuwa mzalendo!!

    ReplyDelete
  8. Mdau wa Pili.

    Sijakuelewa, tueleweshane.
    Mbona unaweka picha Kama vile ardhi "huku bongo" haina thamani?

    Huku nyumbani wengi wetu tuko na mashamba au for that matter ardhi za kurithi kwa wazee wetu. Wengine opt kuuza wengine opt kuendeleza.

    Wananchi walio wengi wako na ardhi zao za asili/kimila but most of them from ignorance na ufukara opt kuuza, and they really throw away. Some of us tunapima na kupata hati and now you have a potential pocket bulge.

    Jamaa zangu wengi waliuzauza holela sasa wanagaragara. Siku zote nasema kama uko na ardhi siyo kitu cha kukichukulia juu juu maana ni mali.
    Leo unauza laki 2 unaona umepata, uliemuuzia baada ya 5 yrs anauza milioni 2. Haviingilani na inflation hivi, ni ardhi always inapanda bei.

    Hao "wananchi wa kawaida" ambao hawataweza kununua kiwanja au shamba, tell us, je? huko uliko mwananchi wa kawaida anaweza? Najua, wanaishi kwenye apartments, very few professionals or very few anyone's affort villas.

    Huko nje ardhi " mwananchi wa kawaida" wala haifikirii maana ni out of bounds, too expensive.

    Pamoja na kuwa shilling imeshuka thamani, sikuelewi unapokataa kuwa nyumbani ardhi imepanda sana thamani. Land always appreciates (inapanda bei kama niko sawa). Zile zama za ardhi, shamba eka 10 kwa shs laki 1 is long gone!l (and was just a few yrs ago).
    Kumbuka, we have a very beautiful country.

    Kuweka thamani kwa dola is just for easier and faster reference. WaTZ wengi wapo nje, wana loose track of our unstable shilling, at least dola iko more stable than shilling.

    Hujanijibu swali langu, bei ya equivalent ya hilo shamba huko ughaibuni ni kiasi gani?

    Mimi sie naeuza hilo shamba, niko TZ I like my country and it is a beautiful place.
    And it has value, very good value.

    ReplyDelete
  9. Big up mdau joe frm abroad,this clearly shows the mind set of most tzans who lives abroad,they got the exposure and knowledge to for see the problems our country is facing and that will face in the future, the land is issues in bongo is a boiling issue soon or later to explode,only few ppl will b able to purchase land coz the price is too overstated,we all know that majority of bongos got no money even to afford a single meal a day,but the dishonest ppl who r fisadis and who stills and involves themselvels in dirty deals r the ones with all the money n the rest struggling,ANY ONE THAT APPEARS TO CHALLENGE THE OVERSTATED PRICES,SOME OF YOU GUYS MAKE IT WAR WORDS,JOE DOESN'T LIVE THERE AND FOR GODS SAKE WOULD HAVE CARES LESS BUT HE IS STANDING WITH THE MAJORITIES WHO ARE STRUGGLING, THE LAND PRICES IN BONGO IS INSANE AND REDICULOUS AND DOESN'T RELATE TO THE CURRENT ECONOMIC AND MONETARY HEALTHY OF MOST TANZANIANS, THIS BULSHIT BLACK MARKET SHOULD END IMMEDIATEL.UNITED STATES IS ONE OF DEVELOPED COUNTRIES IS THE WORLD, DEPENDING WHICH STATE YOU LIVE IN THE UNITATED STATES,YOU COULD FOR RESTANCE BUY A BRAND NEW HOUSE WITH 3-4 BEDROOMS FOR $150,000 WITH. ALL AMMENITIES YOU WILL THINK OF AND PAVED ROADS AROUND IT,SECURE ELECTRICITY,POSTAL SERVICES,SECURE WATER SERVICES,INTERNET AND CABEL READY ,CENTRAL HEATING AND AIR BUT THE SAME HOUSE IN KIJITONYAMA OR SINZA WOULD SALE FOR $300,000 ,THIS WHAT I CALL REDICULOUS AND INSANE. TULIOTEMBEA NA TUNAKAA NJE TUNAELEWA HIVI VITU JAMANI SO ACHANE KUSHABIKIA UJINGA WA BEI ZA NYUMBA NA VIWANJA NA KODI ZA MAPANGO. BONGO,ITS TOOO MUCH KWA TANZANIA. DISCLAIMER: THIS IS NOT TO THE REFERENCE OF THE AD ABOVE COZ HILI NI SHAMBA NA LINA MALI SO MDAU ANAWEZA KULISAMINISHA NA KUUZA KWA BEI HIYO ALOTANGAZA,MIMI VITA YANGU NI BEI YA VIWANJA VYA KUJENGA NYUMBA NA KODI ZA PANGO

    ReplyDelete
  10. Annon wa Fri Aug 17 07:08:00 PM

    Crying out loud...

    CHANGE YOUR MINDSETS OF HOME.

    HUKO NJE NJAA INAZAGAA LIKE WILD FIRE, NO WONDER PRICES FALL.

    WHERE CAN YOU BUY CHEAP LAND IN TODAY'S WORLD?
    Kila mtu kaamka!!! Sio mnakaa huko nje mkifikiri mtakuja kulalia watu huku or get cheap land!

    Hizo nyumba za 150,000USD ni za mbao na cardboard ambazo have short lifespan, hiyo ya k'nyama or sinza ni tofali...has a longer life. And the area is prime.

    Wewe shida yako unataka kulalia watu kutaka precious things for cheap.

    Some of you huko nje need to CHANGE the picture you have of home..Land is getting precious as days go by, jirani zetu wamemaliza kila kitu as far as land is concerned, nyie mnataka rahisi.

    True land issue is boiling here bcoz tumeamka! wala msitutishe eti will soon explode. Watu wanahimizwa kusajili ardhi zao na mashamba yao ya asili wapate hati for obvious reasons.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...