Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama (kushoto) akimkabidhi msaada wa fedha taslimu sh. milioni moja mchezaji wa zamani wa Simba, Mtibwa na Taifa Stars, Alphonce Modest kwa ajili ya kumsaidia katika matibabu ya ugonjwa wa mifupa unaosababisha miguu kufa ganzi ‘yabisi baridi’. Modest nasumbuliwa na ugonjwa huo tangu mwaka 2011. Kwa yeyote anayeguswa na tatizo lake awasiliane na mtangazaji wa Chanel 10, Said Kilumanga (wa pili kulia) kwa kupitia namba 0718 427426. Wa Pili kushoto ni Mhariri Kiongozi wa Champion, Saleh Ally.
Mtangazaji wa Channel 10, Said Kilumanga akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa rai kwa watu mbalimbali kujitolkeza katika kumsaidia mchezaji wa zamani wa Simba na timu ya Taifa Alfonce Modest ambaye anasumbuliwa na matatizo ya miguu.
Beki wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Alfonce Modest akimshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions baada ya kumsaidia kiasi cha sh milioni moja kwa ajili ya kuanza matibabu ya miguu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Nakumbuka wakati akiwa Simba alikuwa beki mahiri sana.

    Hongera Msama na klabu zetu ziwe na utamaduni wa kusaidia wakongwe wao jamani

    ReplyDelete
  2. Hadi machozi yamenitoka mbarikiwe msama promotions hii dunia kama mtu hajui kama umebanwa anakuangalia tu. Sura ya huyo Alfonce inaeleza alivo na huzuni kubwa. Mungu akusaidie upone maradhi yanayokusumbua. Simba jamani hamuwezi kumsaidia? make mwenyekiti ni mbunge naamini hashindwi kumpatia hata milion 5 jamani. Mmmh hii dunia majaribu mengi hasa ukiumwa na huna hela

    ReplyDelete
  3. Kuna mchezaji juzi juzi tulimuona anasifiwa sana kwa kuishi kwenye jumba la kifahari na anaendesha gari la bei mbaya sana. USIA wa bure, wachezaji mpira punguzeni starehe, jifunzeni kujiwekea akiba , maisha hayana garanti na huwezi kujua kesho utaamuka na hali gani. Hii si kwa wacheza mpira peke yake ,USIA huu ni kwa kila mtu.Tuishini maisha ya kawaida ( low profile) majigambo na matanuzi ni kinyume ya maandiko, Yesu na mitume yote hawakuishi kiufahali. Tupunguze au kuacha kutembeza jando kila kona, kumbukeni kwamba hii ni starehe ya dakika 1 tu lakini gharama zake na mihangaiko yake ,hailingani na faida unazozipata baada ya kitendo,na si ajabu ukaondoka unajikuna , hela hiyo ungeiweka bank au NSSF ingelikusaidia wakati kama huu wa kuumwa au hata huko uzeeni, kuliko ulivyoitumia kwa kumhonga huyu ( PAPA ) kwa starehe ya dakika moja. Tatizo ni kwamba ,Papa akisha kukamua ,humuoni tena.Hawana fadhira ,tumieni sabuni.Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  4. Hii mimi siipendi!! Nafikiri faraja kubwa na pengine thawabu unazipata kwa kutoa kimya kimya, na sio kuita vyombo vyote vya habari!!

    Labda itokee bahati mbaya mpokeaji ameshafaidika na huduma yako yeye mwenyewe kwa nafsi yake aamue kuusimulia umma, na hapo ndipo chati yako itapaa mawinguni!!

    Mh. Rage na viongozi wengine wa michezo nafikiri mnaona, ni changamoto kubwa inayotukabili jinsi ya kuwahudumia wanamichezo wetu pindi vipato vya mpito vinapofikia ukomo!!

    ReplyDelete
  5. yaani msama wameguswa sana na tatizo la Modest kuliko simba na mtibwa!!,inamaana hata hawakumbuki mchango wa modest wakati akichezea vilabu hivyo? kweli bongo bado saana.Hongera msama.

    ReplyDelete
  6. hivi kweli Taifa has kwa wizara a michezo linahusika vipi na watu kama huyo?

    ReplyDelete
  7. watu kama hawa nchi za wenzetu wanathaminiwa sana na kutunzwa ila tz yetu hovyo hovyo tuuu inatia kinyaaa sana hii nchi hakuna watu wanaofikiria mbali na kama wapo wamelala..pole sana ndugu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...