Kwa kuwa mchakato wa kupata Katiba Mpya ni utaratibu unaosimamiwa na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83; tunashauri kuwa Watanzania wote wanaotaka kushiriki katika mchakato huo ni vizuri kuzifahamu Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura ya 83 ambazo zote zinapatikana katika tovuti ya Tume ambayo ni www.katiba.go.tz
Kusoma Sheria hizo kutasaidia kuielewa Katiba ya sasa ubora na upungufu wake na kuelewa utaratibu na masharti yanayoainishwa kisheria kuhusiana na mchakato wa upatikanaji wa Katiba Mpya.
1. 1. MAMBO YA KUZINGATIA
Kwa kuwa uratibu na ukusanyaji wa maoni unatawaliwa na kusimamiwa na Sheria, Tume inaelekeza mambo yafuatayo yazingatiwe:
(a)Nani Mwenye Haki ya Kushiriki:
Mtu yeyote ambaye ni Mtanzania kwa uraia wake anayo haki ya kushiriki katika mchakato huu. Mtu ambaye kwa asili yake ni Mtanzania, lakini amepoteza uraia wa Tanzania hatoweza kushiriki; na akifanya hivyo atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria.
(b)Utaratibu wa Utoaji Maoni:
Njia tatu za ukusanyaji wa maoni zitatumika. Njia hizo ni kama zifuatazo:
(i) Utoaji wa maoni kupitia mitandao ya kijamii, tovuti (www.katiba.go.tz) barua pepe ya Tume, ( katibu@katiba.go.tz ), nukushi + 255-22-2133442 na +255-224-2230769
(ii)Utoaji wa maoni kupitia nyaraka na barua zitakazotumwa kwa Tume kutumia anwani ya Tume, ambao ni: Katibu, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, S.L.P. 1681 DSM au Ofisi ndogo ya Tume, S.L.P. 2775 Zanzibar.
Endapo Mtanzania anayeishi Ughaibuni atabahatika kuwepo Tanzania wakati wa ukusanyaji wa maoni, anaweza kushiriki katika mchakato huo kama Watanzania wengine walioko nchini kwa kuhudhuria mikutano ya kukusanya maoni iliyoandaliwa na Tume.
(c) Utambulisho wa Mtoa Maoni:
Kila mtu atakayetoa maoni yake Tume anapaswa kubainisha mambo yafuatayo:-
(i) majina yake matatu;
(ii) namba ya pasi yake ya kusafiria na mahali ilipotolewa;
(iii) nchi na mji anaoishi;
(iv) endapo atatumia nyaraka au barua, ataambatanisha kivuli cha pasi yake (ukurasa unaoonyesha maelezo ya mtu mwenye pasi hiyo).
Tume inapenda kuwakumbusha tena Watanzania kuwa utoaji wa maoni ni jambo la uhuru na hiari ya mtu na kwamba mchakato wa kupata Katiba Mpya unawahusu raia wa Tanzania pekee.
Kwa maelezo zaidi bofya: http://www.katiba.go.tz/index.php/maoni-nje-ya-nchi


ingekuwa vizuri kama huyu john mashaka angeshirikishwa kwenye mambo ya katiba kwa maana naona anayoayaandika yanazingatiwa. wazo langu tu
ReplyDeleteJe mtu anayeishi nchini haruhusiwi kutoa maoni kwa barua pepe?
ReplyDeleteMasharti ni yapi?
Kupoteza urai maanake nini? Mbona serikali imesha watumia waTanzania wenye asili walio poteza urai? Sharia iko wapi? Wakati serikali ina watumia watu walio poteza urai hawa watu hawana haki? Watu wasio na asili ya Tanzania wana pewa haki zaidi kushinda yule alio poteza urai wake. Mnatu oneya waTanzania tulio poteza urai wetu.
ReplyDeletemtu aliyeupateza uraiya waTz ni yupi kati ya hawa hapa chini,,Aliyeomba uraiya wa nchi nyingine akapewa na bila kuukana uzawa uraiya wake,au aliyejiripua katika nchi,na akapewa uraiya ktk hiyo nchi aliyozamia?.......
ReplyDeleteKwani TZ hawajapitisha mtu kuwa na Raiya mbili?,,,Ni Swali tu hilo kwa faida ya tusiojuwa maana ya "ALIYEPOTEZA URAIYA WA TANZANIA"
Na ikumbukwe kwamba hao waliokuja kuomba uraiya wa TZ mkawapa,bado wana uraiya wa nchi zao ina maana wana raiya mbili,na pia Passport zao wanazo pia za nchi zao,,na wanakwenda na kurudi kama kawaida,na wanaekeza kwao vile vile,,WaTz ndo mnawaonea!
Ahlam
Ahsante Michuzi kwa ujumbe huu. mimi nilikuwa natafuta jinsi ya kutoa maoni yangu sasa jibu nimepata
ReplyDeletewabeba boxi wa yohana mashaka, changamkeni sasa
ReplyDeleteSasa naona kweli demokrasia inaingia kwa mikono yote ,Tunashukuru sisiwatanzania tuishio nje kamatunaweza kusikilizwa kwa kutoa maoni ya katiba. Mimi kama mtanzania ninayeishi ughaibuni, nimefurahishwa na issue hii, tusikubali kabisa kuwaruhusu watanzania waliobadilisha uraia na kuchukua uraia wa nchi zingine ka ma, UK,Holland,Sweden,Norway,Finland,Denmark, USA, na nchi nyinginezo nyingi. Kwani kuna watu wengi ambao tayari wanauraia wa nchi nyingine lakini wanamilki manyumba tanzania na ni kinyume cha sheria , kwani wao ni wageni tayari hata kama baba na mama zao ni watanzania, wanamanyumba Zanzibar, mpaka bara na hawalipi kodi yoyote hapo nyumbani ninachomba serekali iamke kulitupia jicho swala hilo, kama hawafati sheria za kuwekeza tanzania basi swataifishwe majumba yao, na wengi wanajulikana kama serekali inataka majina yao itayapata kwa muda wa miezi miwili.
ReplyDeletemimi kwa maoni yangu napendekeza kuwa wale watanzania walioukana utanzania wasipewe haki ya kumiliki chochote hapo kwetu. Wengi wanamilki majumba fukwe za Zanzibar, mbezi beach, Bagamoyo mpaka mitaa ya arusha wakati wao si watanzania hata kidogo ati kwa sababu mama yake au baba yake ni mtanzania, hio ipigwe marufuku anaetaka kujenga aombe kibali cha kuwekeza nchini akikubaliwa ndio apewe fursa ya kujenga.
Naomba katiba iwabane kwa nini wameukana uraia halafu bado wanakuja kuwekeza?
WASIPEWE HAKI WATNZANIA AMBAO HAWANA URAIA WA TANZANIA;SEREKALI ITUPIE JICHO KWA MAKINI, NA WAKIBAINIKA WANA BASI WATAIFISHWE MIRADI YAO, NA HATA MAJUMBA YAO WAKO WENGI WANAOJULIKANA
ReplyDeleteAs salaam Alaykum....Nimeguswa na kipengele cha haki ya kushiriki kutoa maoni ya katiba....Mzawa wa Tanzaniaaliepoteza uraia wake,kwa sababu yoyote ile,hana haki ya kushiriki kutoa maoni....lakini mgeni raia wa kuandikishwa ANAYO..!! uwiiii,hivi nyie viongozi mmefikiria vyema ndani ya nyoyo zenu,nini maana yake hilyooo..????Tena ni kosa la kisheria kutoa maoni..wawooo,ni sheria kifungu namba gapi hicho,kinachomzuia mzawa asitoe maoni eti kwa sababu ameandikishwa uraia kwinginepo..?? hivi hao wageni mliowaandikisha huko wawasaidieni kuandika maoni ya ya katiba ya nchi wasiyoijua(wamekuja kwetu,kama tulivyoenda kwao)mnahisia kuwa wao ni wakereketwa zaidi na mfumo mzima wa maisha yetu ktk nyanja zote za Ki-tanzania..??? hebu tuondoleeni hilo changa la macho,tuwape maoni ya kweli na yenye uadilifu kwa faida ya nchi baadae.....Kwanza,naomba mjifahamu kuwa nyie ni watumishi wetu na mnayo dhamana kwa Mwenye Enz na hii Dunia,hivyo mfahamu kuwa kinachofanyika hapa waeza ukakiwahi kukiona au usiwahi...iwe ni swadaka njema kwa nchi na sio maslahi ya fulani au kundi fulani......hayo ndio yanayoleta sasa Uamsho Zanzibar na sufuria ina tobo maji hayakai wala kujazika tena....kiwe ni kioo hicho mnajiangalia.....Wasalaam..!
ReplyDeleteMasikini ni masikini tu utamjua kimawazo kifikira na hata kiuwezo, badala ya kufikiria aliye juu umfuate hukohuko unafikiria aliye juu umngoje chini. Sasa nyie wadau kama mkianza hizi chokochoko nani ndie analoose mi naona watanzania, wenye majumba yao wakiyauza na pesa waamue kupeleka nchi wanazoishi si uchumi wa nchi utazidi kuzorota, akili finyu. wenzenu wa nchi zilizoendelea ndio maana wanatoa uraia wa nchi mbili ili wananchi wao wajenge nyumbani, mtazidi kuachwa nyuma na Roho zenu mbaya za chuki. Mfano mzuri kenya na Uganda wanawapita nyie mmelala usingizi mzito mnafikiria kuwakomoa watanzania walio nje.
ReplyDeleteMi mambo yakiwa magumu si nauza nyumba zangu nakuja kuwekeza huku kwenye amani na haki tuone nani analoose. Nchi hiyo ishauzwa badala ya kuwabana wageni mnafikiria kuwabana watanzania wenzenu walioenda nje kutafuta maisha, Poleni sana Masikini wa mawazo
ReplyDelete