NA MWANDISHI WETU

CCM imesema imesikitishwa na iliouita usanii mkubwa unaofanywa na Chadema, kuwahadaa Watanzania kwa kufanya harambee kwa lengo la kuhalalisha mabilioni ya chama hicho yanayodaiwa kutolewa na wafadhali kutoka mataifa tajiri duniani.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye aliyasema hayo leo, Agosti 12, 2012, wakati akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, mtaa wa Lumumba jijijni Dar es salaam.

“Itakumbukwa mara kadhaa Chadema wamekuwa wakiitisha harambee za kisanii kwa kujaribu kuwahadaa baadhi ya Watanzania kwa kuwaomba wakichangie chama hicho huku viongozi wa chama hicho wakijua kuwa tayari wameshapata mabilioni toka kwa wafadhili wao. Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Jumamosi, Agosti 10, 2012, kwenye hoteli ya Serena ambapo walifanyika kiini macho cha harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni." alisema Nape.

Alisema ,umekuwa ni utamaduni wa Chadema kuhadaa watu kwa kuitisha harambee za kisanii kina wanapokuwa wameshapewa mabilioni ya fedha na wafadhili wao, ili mradi wahalalishe kuwa fedha wanazotumia zimetokana na michango ya watanzania wakati si kweli.

Nape alisisitiza kuwa CCM wanao ushahidi kuhusu zinakotoka fedha na mikataba wanayoingia Chadema na wafadhili hao na kudai kuwa kama hawatasema wenyewe basi yeye (Nape) ipo siku atawasaidia kwa kutaja wafadhili hao na kuanika hadarani mikataba hiyo.

“Tunao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema juzi na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni zao mbalimbali nchini. Cha kushangaza badala ya kuwaambia wanachama wao na Watanzania kwa jumla mikataba na wanakoyapata mabilioni haya, wanawahadaa kwa kuwachangisha na kugeuza mapato hayo mtaji wa baadhi ya watu binafsi ndani ya chama”, Alisema Nape

Nape alidai kwamba, siri kubwa inayofichwa kuhusu mikataba na mabilioni wanayopewa Chadema ni kwa sababu wanaotoa fedha hizo wana ajenda ya kunyemelea rasilimali za nchi hii zinazoanza kuonyesha matumaini ya kuwepo kwa wingi ili wapate kizikwapua kwa urahisi kupitia mgongo wa chama hicho.

"Kwanini mabilioni hayo yanatolewa kwa Chadema wakati huu ambapo sasa Tanzania imo katika kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta? Na Je ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?", Nape alihoji.

Alisema, hatua hiyo ya Chadema itaitumbukiza Tanzania katika machafuko yasiyoisha, kama ambavyo inashuhudiwa katika baadhi ya nchi zenye rasilimali kama madini ambako nchi zenye utajiri wa fedha zilijipenyeza kupitia walioitwa wapambanaji wa uhuru na haki katika nchi hizo na hadi sasa hakuna amani.

"Migogoro mingi tunayoshuhudia hasa katika nchi zinazoendelea pamoja na kuwepo sababu zingine lakini moja ya chanzo kikubwa ni uwepo wa utajiri wa rasilimali mbalimbali ambapo mataifa makubwa huzitamani na njia pekee ya kuzipata kwa urahisi ni kuchochea migogoro ya ndani na hivyo kuwa rahisi kupora rasilimali hizo wakati wenye nchi wanahangaika katika migogoro na kuachwa wakiwa masikini wa kutupwa huku waadhirika wakubwa wa migogoro na vita hivi vikiwanufaisha wakubwa.” Alisema Nape.

Nape alitoa mwito kwa Watanzania kuwa ni muhimu macho na ulaghai huo wa Chadema na wafadhili wao na kukitaka chama hicho na wafadhili wao kama kweli wana nia njema na Tanzania, waweke wazi mashariti ya ufadhili huo wa mabilioni ya fedha ili Watanzania wote wajue kama yana manufaa kwao au la hasa ikizingatiwa kuwa vyama vya siasa hapa nchini vinaendeshwa kwa fedha za walipa kodi, hivyo Watanzania wana haki ya kujua.

Pamoja na kuwataka kuweka wazi mashariti yanayoambatana na mabilioni hayo Nape aliwataka Chadema waseme hadharani wenyewe kwamba wamepewa mabilioni hayo, na kuwataka waache mara moja kuwahadaa Watanzania na kujaribu kujipachika kuwa ni Chama cha wanyonge kinachotegemea kujiendesha kwa michango ya watanzania huku wakiendelea kuchukua mabilioni kwa siri kutoka nje.

“ Wasipowaeleza watanzania ukweli , tutawasidia kuwaeleza watanzania ukweli wa kiasi halisi cha mabilioni haya, walikozitoa na mikataba waliyoingia. Lengo la hili ni kuhakikisha kuwa nchi yetu haiwekwi rehani kwa uroho wa madaraka wa baadhi ya wana siasa.” Nape alisema.

Nape akawaasa wanasiasa, kuendesha siasa za nchi kwa kuzingatia uzalendo na kukwepa kudumbukia kwenye tamaa za madaraka kujisahau na kuwa tayari hata kuweka nchi rehani, hasa kipindi hichi ambapo ugunduzi wa rasilimali mbali mbali hasa madini, gesi na mafuta vikiwa vinashika kasi nchini na kwamba ugunduzi huo uwe baraka kwa nchi badala ya laana na kuwa chanzo cha kuiuza nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 45 mpaka sasa

  1. Uzalendo wa CCM huko wapi?Si waliiba pesa zetu za kodi na ku-inject kwenye uchaguzi?Hii ina uthibitisho lakini yeye hajawahi kuzungumzia.Yaani siasa za Tanzania ni matope sana.

    ReplyDelete
  2. NAPE KAMA UMEISHIWA SERA NAKUSHAURI QUIT POLITICS AND GO BACK TO YOUR MOTHER LAND. HUU SI WAKATI WA KUPOTEZA MUDA WETU KUTULETEA RIWAYA ZINAZOHUSU CHADEMA WAKATI HUKU KWETU CCM MAMBO HAYAELEWIKI. TUNATAKA SERA ZA KUFUFUA CCM AND NOTHING ELSE. KAMA HIVYO VYAMA VINGINE VINAHADAA WASHABIKI WAO NI JUU YA WASHABIKI KULALAMIKA NA SIYO WEWE KUWASAIDIA KULALAMIKA. AMA MWENZETU UNATUMIKIA CCM NA CHADEMA? UNACHOFANYA NI KUWAPA NONDO CHADEMA ZA KUJENGA MIKAKATI BORA ZAIDI YA KUSHAWISHI WATANZANIA NA SIYO KUKIBOMOA

    ReplyDelete
  3. Halo halooo!
    Wenye wivu wajinyonge!!
    Wivu tu na kijiba cha roho!

    ReplyDelete
  4. Mkuu umeishiwa....

    ReplyDelete
  5. Upuuzi mtupu kutoka CCM.

    1. Tulianza kutafuta mafuta na gesi kwenye miaka ya 1950 kabla ya uhuru tukiwa chini ya mkoloni aliyeamua kutafuta mwenyewe. Miaka yote hiyo Tanzania na chama tawala vilikuwa vikipokea pesa kutoka nje. Mbona hamsemi?

    2. Hivi leo maliasili zetu zote zinapigwa minada na viongozi wa CCM. Mbona hamsemi?

    3. Chadema haipendwi na wafadhili kwa kuwa inasema ukweli dhidi yao. Nani atawapa fedha?

    CCM acheni uongo na upuuzi. Watanzania wamewachokeni; mtaondoka tu hata mkiiba kura na kuua watu.

    CCM na polisi wao; Watanzania na Chadema yao.

    ReplyDelete
  6. Mimi nijuavyo katika nchi yoyote fedha zinapoingia kupitia ufadhili ama msaada kwa shirika ama taasisi yoyote huwa zinaratibiwa na benki kuu ili kubaini madhara kiuchumi na kisiasa na lengo mahususi la fedha hizo kwa mustakabali wa taifa. Sasa kama Nape ulibaini pesa hizi zina madhara hatua gani zilichukuliwa? Pia popote pale "mobilization of internal resource' ni jambo ambalo linakubalika kisheria. Mimi sioni tatizo kwa CHADEMA kupata nyongeza ya nguvu ya wafuasi wake ili kuboresha harakati zao za kuingia madarakani. Mr. Nape twambie ni kiasi gani na ni wafadhili gani wameipa mapesa CHADEMA na ni taratibu zipi zilikiukwa katika kuzipata pesa hizo ili tuunge mkono hoja yako. Sisi kuipa support CHADEMA si tatizo. Ikumbukwe CHADEMA hawakusanyi kodi hivyo kupata pesa katika source mbalimbali si tatizo ili mradi hawavunji sheria.

    ReplyDelete
  7. Du kama ni kweli.ikidhibitika tutawatosa tu nafuu tubaki na manyangumi wetu wa kifidi.Ndugu wananchi ufisadi usiwe mtaji wa kutuweka rehani.Hao wachaga si ajabu wana ajenda ya siri.Tangu lini mchaga akaendesha resources za nchi.Lakini Nape ni yale yale dola yenu iko wapi ?usalama wa taifa uko wapi?Haiwezekani ukaungana na wannchi kulia lia wakati wewe ndo wa kuwahoji unayo dola siyo?

    ReplyDelete
  8. Hongera sana nape kwa mapenzi yako kwa nchi yako na watu wako..hakiyamungu chadema mungu atawalani..kama mpango wenu ndio huo..lazima wawa ambie watz wote huo ufadhiri unafaida gani kwa nchi..na hiyo mikataba ni mikataba gani..jamani msituletee vita watoto wetu wataumia mama zetu pia bibi zetu mababu zetu..na kwa wananchi wote kwa ujumla...wote kwa pamoja tuseme hatutaki vita..ni mm mdau wenu tajiri wa mawazo endelevu.nipo uk...amani kwa watz wote.

    ReplyDelete
  9. Nape kaishiwa sera na anachemka sana ,hii harambee ya chadema siyo kitu cha kusimulia kabisa kwani hata USA chama cha Democratic party ambaye rais wake ni Obama huwa wanafanya harambee na kuchangisha mabilioni ambayo yanatolewa na wananchi wapenzi wa chama na utendaji ktk uongozi ,hivyo Nape naona ameishiwa sera.Wananchi wanataka mabadiliko na maendeleo ndiyo maana wapo tayari kutoa kidogo walichonacho kwa maendeleo ya baadaye.Big up mdau big Joe,bro michuzi naomba uipost hii comment yangu

    ReplyDelete
  10. Nape wacha kuchochea na kuleta vita kwenye nchini letu sasa kama unawajua na unaushaihidi ya nini leo hii kukimbilia kwnye vyombo vya habari badala ya kutoa ushahidi bungeni na pia police. naomba viongozi wetu wa vyama vyote msiwe na tabia ya umbeyaumbeya kwennda kwenye vyombo vya habari kusema mambo yasio na msingi na pia kusema eti nina ushahidi tosha na haya mambo ni watu wa ccm na chadema wanafanya kila siku ila ipo siku mambo yatakuwa mabaya ndio mtaona umbeya kwa ummma sio faida

    ReplyDelete
  11. huyu nape ameshindwa kisiasa kabisa kama anao ushaidi kwa nini asipeleke sehemu zinazo husika ? amesema anaoushaidi wa kutosha ccm imekwisha it is time for change watanzania wamechoka na michezo ya kuigiza ya selikali ya ccm m4change

    ReplyDelete
  12. Ndugu yangu NAPE, kwanini unakubali kuwa mkia kuibuka kila Chadema wanapofanya jambo? Hebu jaribu kutangulia ili wenyewe wawe mkia, la sivyo unajimaliza.

    ReplyDelete
  13. Ukizingatia anatoka chama tawala kulikuwa na sababu gani ya kuropoka kwenye vyombo vya habari wakati dola iko chini yao.

    Hayo ni majungu tu...mngekuwa na ushaidi mmgewaacha nyie. Umaarufu umekwisha CCM sasa mnatafuta mchawi.

    ReplyDelete
  14. Nyie watu tena muogopeni Mungu na wala dont mention kabisaa

    ReplyDelete
  15. CHADENA ni chama kinachotarajia kuchukua madaraka kwa namna moja au nyingine maneno ya Nape yanaweza kuwa kweli. Niliposikia watanzania wamechangia hela zote hizo kwa CHADEMA nilikuwa na mawazo hayo hayo... kufunga mjadala CHADEMA itoe majina ya watanzania waliochangia hela hizo na Nape atuletee majina ya hao wafadhiri.

    ReplyDelete
  16. nape vipi zile ahadi zako za kung'oa magamba? kijana naona ngoma kwako haijaisha unaenda kwa jirani.

    ReplyDelete
  17. NAPE CHAMA SIO YAKO PEKEE HATUTAKI SERA ZA MAJUNGU JAMBO KUBWA LINALO TU UMIZA WANA CCM NIKUWAPA MISIFA VYAMA VINGINE ACHANA NAYO MAJUNGU KOSA KUBWA HILO CHA MSINGI FOCUS MUELEKEO WETU CCM ITUMIE MBINU ZIPI KU KIIMARISHA CHAMA KATIKA HAYA MAGROUP YALIO NDANI YA CHAMA HAPO ITAKUA BORA ZAIDI ACHANA NA CHADEMA UNA ZIDI WAPA CHART AU WEWE NAWE MMOJA WAO NINI BANA KAMA HUWEZI KAZI SEMA GARI LIKIPATA PANCHA TAFUTA UTARATIBU KULI TENGENEZA SIO VINGINE SASA CCM NIPANCHA TU HIVYO TUITENGENEZE SIO HIVI AU VILE NA SIASA HAMTAJI MTU JINA

    ReplyDelete
  18. kama mnao ushahidi si mfungue kesi mahakamani, kama mmefaulu kufungua kesi ya uhujumu uchumi dhidi ya Profesa Costa Mahalu ambaye alikuwa Balozi katika Serikali yenu huku mkiwa hamna "ushahidi" na akawabwaga mahakamani, mtashindwa kuwafungulia kesi CHADEMA huku mna ushahidi, isitoshe si sehemu ya chama chenu wala serikali yenu.

    ReplyDelete
  19. Namshangaa Nape na CCM yake kufanya kazi ya Msajili wa vyama vya Siasa. Kama CCM inafanya kazi ya vyama vingine,nini kazi ya Msajili wa vyama vya Siasa? Huu ni wivu uliotamalaki.

    ReplyDelete
  20. Nape, so what, unaogopa nini, na wewe uza sera zako

    ReplyDelete
  21. Ni kweli Chadema wanapokea fedha kutoka makanisa duniani kwa sababu wamesikia ni chama cha dini. Mwananchi gani huyo mnayemzungumzie, labda wa wachaga wenzenu lakini kwengine tuacheni hivyo hivyo. Chama kitachukua nchi bila ya kuwa na roots. mmeshika matawi tu. Labda 2020 lakini kabla ya hapo hamwoni ndani. Mbuyu ulingoka lini.

    ReplyDelete
  22. Huyu ni muongo na mzushi. watanzania wameshashtuka. kuna kipindi fulani waliwahi kutuambia kuwa chama cha wananchi CUF kimeingiza nchini meli ya mapanga kumbe ilikuwa nikuwahadaa na kuwatisha watu waokione CUF kinaleta vita. Nape, fanyeni siasa zenye tija kwa taifa.

    ReplyDelete
  23. Tatizo sio CHADEMA kupewa mabilioni, tatizo ni hiyo mikataba. Nape ungeweka hadharani hiyo mikataba ili tuone ina masharti gani na hatari yake kwa ustawi wa nchi ni nini. Kupewa mabilioni ni njia moja wapo ya kukuza uchumi kama mikataba haina masharti magumu.

    ReplyDelete
  24. Hawa wafadhili ndiyo wanaharibu nchi.. Angalia yaliyotokea Siera Leon na Liberia yata kuja tokea Tanzania tusipoangalia. Katiba mpya iweke sheria hakuna chama chochote kitakachopewa ruzuku toka nje ya Tanzania na makampuni ya Tanzania yawekewe kiasi fulani ya pesa na watu binafsi pia wawekewe kiasi chao cha kuchangia kwenye chama. Na chama kinachokiuka sheria basi kifutwe. Kama Chadema wamepata msaada huu na hakuna sheria inayokataza hawana makosa. Ila wanahatarisha usalama wa nchi kwa kupokea hiyo misaada maana hapa duniani hakuna kitu cha bure na ndiyo mwanzo wa kuanza kuwa na ma Mafia. Angalieni CHADEMA mlianza vizuri sasa na mnaaanza kuleta doa si vizuri. Wasomi wengi wameweka imani kwenu kumaliza ufisadi ambao baadhi ya viongozi wa CCM wanao.LAkini pamoja na hivyo tusisahau Amani na utulivu ilayopo nchini ni kwa sababu ya CCM!

    ReplyDelete
  25. MIE NAWASHANGAA WATU, WENGINE NA AKILI ZAO, HATA MAPROFESA, KUWA BRAINWASHED NA MTU KAMA FREEMAN MBOWE NA DR SLAA AMBAO WAO WENYEWE KIMAISHA NI MAGUMASHI TU. HUYU MMOJA MPIGA DISCO NA MWINGINE KONDOO ALIYEASI. HAWA KWELI UKIANGALIA HARAKA HARAKA NDIO WA KUWAPA MADARAKA, ACHILIA MBALI NCHI. HALAFU UKASKAZINI ULIVYOSHIKA HATAMU NAONA HATA MNYIKA NAYE ANAUNGA MKONO KABILA LA MAMA YAKE KUPAMBANA NA WAPAMBANAJI WA KWELI KAMA ZITTO. PIGA UA 2015 HAMUONI NDANI, HATA MPEWE MICHANGO NA CAMERON KABISA!

    ReplyDelete
  26. Inatisha pale wanaharakati wanapojisahau hata kusoma hoja ya mtu kwa sababu kavaa kijani. Mbona anachosema Nape kiko clear. Issue sio kupata wala hio hela ya nje, issue anayosema ni kutokuwa wazi na hela inapopatikana na kudai ni ya wazalendo. Sasa kama Nape anapotosha sawa, lakini wanaharakati, jibuni hoja maana mnapokimbilia kutoa labels..haisaidii kitu na hamuwatendei watanzania wenu haki.. uchu wa kuchukua au kutoa mtu madarakani usiwapeleke huko huko ambako mmejengea hoja ya kwanini CCM watoke.

    ReplyDelete
  27. CCM FANYENI MAMBO YENU ACHENI KUSHABIKIA MAMBO YA MSINGI WANAYOFANYA CHADEMA...HATA MAREKANI OBAMA ALIFANYA FUND RAISING.....KWANI NYIE HAMNA SERA ZENU NA MIKAKATI YENU? KWA NINI MNASHABIKIA ISSUES ZA CHADEMA.....

    ReplyDelete
  28. Kazi kwelikweli its complexity of reality.Watanzania wengi tuna upeo mdogo sana wa kupambanua mambo.Kwanza kabisa hatusomi vitabu vya discipline mbalimbali.Ndio kusema ni ngumu kwetu kutoa maamuzi sahihi inapotokea hoja kama hii ya NAPE. Ndiyo maana hata viongozi wenyewe hawapati tabu kuaddress vitu kama hivi kwa jamii yao na zaidi hata vyombo vya habari havipati tabu hiyo.Hili pia linatiwa moto wa mafuta na ulimwengu wa leo ambao watu wana hamu ya kusikia kitu kipya upesi wakati mkononi anacho kitu kipya kingine.Si vema sana namna tunavyowaamini watu kushika nafasi kubwa za maamuzi au uenezi na hata usemaji mkuu katika taasisi nyeti bila kujiridhisha na viwango vya maarifa, ujuzi kuona mbali zaidi na subira.Tatizo hilo ni kubwa na linaonekana sasa na bila shaka litatukosti mno kt. kufikia upeo wa mafanikio kwa taifa letu.Tafadhali Michuzi posti hii ndugu zangu wachangie.

    ReplyDelete
  29. Che GuevaraAugust 13, 2012

    Wewe Anoy. wa 06.43 unafikiri kwa kutumia MAKALIO na uu tasa wa kufikiri!tunachohitaji na mabadiliko kuondoka na wizi, dhuluma ya CCM! hatuhitaji maprofesa kutuletea maajabu kwani wapo siku zote na hawafanya lolote na hawa CHADEMA naamini kabisa NI MUNGU amesikia kilio cha waTZ.Hawa ni MUSA na HARUNI wa BIBLIA

    ReplyDelete
  30. Watanzania tuache siasa za ushabiki. Hili la kuchukua fedha za ughaibuni ni hatari kwa taifa letu kwa maana ya uhuru, rasilimali na utaifa wetu. Ikumbukwe hata baba wa taifa alikemea sana kitendo cha kuchukua fedha kutoka kwa wakoloni kwa ajili ya kugombea madaraka hapa kwetu. Mtazilipaje pesa hizo kama si kuuza nchi yenu wenyewe? Jamani! tuwabane mafisadi kwa kuhakikisha hawapati nafasi ya kutuibia lakini si kwa kuuza kabisa na uhuru wetu.

    ReplyDelete
  31. HIYO MIKATABA NDO MUHIMU ZAIDI NA SIO PESA. HIYO MIKATABA IWEKENI HUMU TUIANGALIE KAMA INA MASLAHI AU HAINA KWA TZ. NAPE TUWEKEE HUMU.

    ReplyDelete
  32. Mmeshikwa PABAYA NAPE, mbona huu ni mwanzo tu!!!!! Subirini mtatunga na mengine mengi zaidi ya haya. Mbona nyie (CCM) huwa mnasiainia mikataba HOTELINI tena kwa kuwafuata huko huko nchini mwao hao wenye kuja kuchimba madini??? Kiukweli MMESHIKWA PABAYA

    ReplyDelete
  33. Kwakweli huyu Nape mimi namuona nikiongozi wa majungu na hafai kuwa kiongozi sbb anapenda sana fitna!Nimemfatilia sana kwenye fc kazi yake anapiga mafumbo kutupa maneno ya fitina fitina watu wengi wanajaribu kumpa nyezo zakuweza kuisaidia jamii lakini hajui kuitumia nafasi!huwa analalamika kuhusu ufisadi jamii wanajaribu kumuelewesha wapi asaidie jamii sehemu ulipo ufisadi lakini hana reaction yeyote zaidi yakubuni fitna nyingine kwa siku inayofuata!tangu siku alipopewa uongozi sijaona kitu alichosaidia kutokomeza ufisadi zaidi yakuufinika na kuufanya uendelee kuwa na mizizi!tafadhali tunamuomba ajaribu kuwa kiongozi mwenye msimamo!matunda ya chadema nape yanaonekana kwakufichuwa mengi ambayo yangewafanya nyinyi kujisafisha!

    ReplyDelete
  34. safi sana Mh Nape Nnauye. Ni bora kukusanya fedha za chama kwa kuiba mali ya nchi kuliko kusaidiwa na wafadhili. Unatumia cha watu wako kujenga chako kuliko kutumia cha wengine kuinua chako. Big up Nnape, Big up Kikwete, Big up CCM! Daima Mbele!!!!!!

    ReplyDelete
  35. If we are serious about changing the direction of our country we should think of a different way of selecting MPs and leaders tusiwe na watu ambao sio responsible kwa wananchi.We pay them a lot of money,they do nothing and yet the people are still suffering.

    ReplyDelete
  36. Haya aliyosema Nape si mambo madogo hata kidogo na ni hatari sana kwa mustakbali wa taifa hili,
    Kinachonishangaza ni kuwa wengi wa wachangiaji hawaoni hatari kubwa iliyopo mbele ya nchi hii, kweli watanzania tumezoea amani mpaka tunatafuta kitu kingine,
    CHADEMA wakanushe basi ili nape awataje hadharani na ikiwezekana washtakiwe hawa kwa kuhatarisha au kuuza nchi,
    Mimi nasisitiza linapokuja swala la amani ya nchi hii basi siasa ziwekwe kando na tulitazame jambo hilo kwa macho yatafakari zaidi,
    naamini kuna watu what come may ni CDM/ CCM ila hapa tafadhali ... twende mbali zaidi, nina amini hata mnyika anacheza ngoma asiyoijua...

    ReplyDelete
  37. TOENI HOJA WATU WA CHADEMA MSIISHIE KUSEMA WIVU... NAPE KAONGEA WAZI TU MBONA MNAMWITA WIVU,, WIVU KWA LIPI WATU WANASERIKALI WAWAONEE WIVU WABABAISHAJI KUTOKA KASKAZINI HAHHAAA. NYIE VIPI. CCM OYEEE!!! HAHAHAA.

    ReplyDelete
  38. Wadau naomba mtupe CV ya huyu Nape.

    ReplyDelete
  39. KIONGOZI KADA WA CHAMA Nape,

    Wala usiogope !

    Hizo ndio Siasa za kiushindani.

    Fedha nyingi sio kigezo za Ushindi wa Kisiasa.

    Kinachotakiwa muwe na Sera za kiukweli na muache uongo uongo ili mrudishe imani ya wananchi juu ya Chama Tawala.

    Mfano Marekani Wagombea Uraisi mwaka huu 2012 Barack Obama-DEMOCRATIC na Mpinzani wake Mitt Romney-REPUBLICAN wametofautiana sana kuanzia wao binafsi hadi kwenye vyama vyao kwa uwezo wa Kifedha.

    Ina maana Mitt Romney ni Tajiri zaidi ya Barack Obama pia chama chao Romney cha Republican ni Tajiri zaidi ya Chama cha Omaba Democratic, lakini sio kuwa Mgombe na Chama cha Republican kuwa na fedha nyingi sio kigezo cha Ushindi ktk Uchaguzi!!!

    ReplyDelete
  40. CCM hayo Mabilioni ya CHADEMA ndio iwe fundisho kwenu muache siasa za Kifisadi ndani ya Chama Tawala.

    ReplyDelete
  41. Enheee CCM kunya anye kuku akinya bata kaharisha!

    ReplyDelete
  42. Nape hizo ndio Siasa za kiushindani, ninyi mkichota za ndani watu wanatafuta za nje ya nchi!

    Na wala msitishike na Mabilioni hayo kazi kwenu, jipangeni tu kwenye Sera na ahadi za kuacha uongo uongo!

    Mpo hapo???

    ReplyDelete
  43. Bola tufe masikini na CCM yetu haina udini, kuliko kuchagua chama kinatoa misaada ya kidini toka nje, bado tunapenda amani yetu hao waroho wa madaraka wamefulia. Wanadanganya toto, badilisheni katiba ya chama chenu kiwe na dini zote then ndio tuwape nchi

    ReplyDelete
  44. Wametoa misaada vatican

    ReplyDelete
  45. Hivi nyie mnaokimbilia kutoka mifano ya marekani ni kwamba hamjui au hamtaki kujua swala la uwazi wa hio michango. Kwani hela anayopokea Obama inafichwa? Iko waazi na kwa wao ni sheria kwamba hela inayopatikana iwe wazi iikotokea.

    Obama akitoka kufanya fundraiser kila senti inajulikana ilikotokea. f

    Hio ndio hoja yakuzungumzia. Tuache uvivu wa ku copy na paste bila kufanya ka utafiki kidogo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...