Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora.

Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.

Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo.

Imetolewa na;-

Nape Nnauye

KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM WA ITIKADI NA UENEZI
22/08/2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Uamuzi wa kukata rufaa ni wa hekima sana. Ingawa mimi si mwanaCCM wala sina interest na mambo ya siasa, lakini ni mfuatiliaji mzuri wa media communication, i.e. electronic, print na hizi new media;kumbukumbu zangu zinanifahamisha kuwa kama hii kesi ingelikuwa ni mchezo wa mpira wa miguu basi timu ya Dr. Bilali ilicheza under protest kwa vile toka awali ililalamikia biasness ya jaji kiasi cha kutamka bayana kuwa haina imani naye na malalamiko hayo kupuuzwa. Ni hukumu iliyotegemewa!!!!

    ReplyDelete
  2. Che GuevaraAugust 23, 2012

    Tukubali ukweli, CCM ilicheza rafu mbaya sana Igunga.

    Sijui kama wametafakari kabla ya kukata rufaa kwani waendako naona ni kule kule walikotoka (mahakama kuu).

    ReplyDelete
  3. CCM wanachelewesha uchaguzi tuu wote tuliona kwenye TV na tukawasikia Magufuli, Rage,nk wakisema waliosema. kwenye rufaa watasema hawakusema hayo au hawakuwa na maana hiyo (walikuwa wanatania!!!). CCM badilikeni. Tanzania ya leo sio ile ya zamani ki-vile.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...