Ngoma Africa band aka FFU yenye makao yake nchini Ujerumani,Bendi hiyo maarufu barani ulaya itatingisha tena jukwaa la onyesho ya kimataifa la International African festival ,mjini Tubingen,Ujerumani.

siku ya jumamosi 11-08 na jumapili 12-08-2012 katika uwanja wa FestPlatz, Tubingen Habari za uhakika zinaeleza kuwa bendi hiyo imechaguliwa kuwa bendi bora ya kiafrika barani ulaya na kushinda tuzo la Award ya "IDA - International Diaspora Award". 

tuzo hilo litakabidhiwa kwa kiongozi wa bendi hiyo mwanamuziki mahiri Kamanda Ras Makunja usiku wa Jumapili 2012,Kikosi kazi cha Ngoma Africa band kimepigiwa kura nyingi na washabiki,pamoja na tahasisi mbali mbali kwa kutajwa kuwa ndio bendi pekee ya kiafrika barani ulaya iliyoweza kutumia muziki wake kama daraja na kufanikiwa kuziteka nyoyo za washabiki na kuwaunganisha washabiki wa mataifa mbali mbali duniani.

Pia kikosi kazi hiko kimetajwa mara nyingi kuwa kimediliki kujitoa muanga kwa kupiga muziki mpaka kwenye nchi zenye usalama mdogo na mazingira ya kivita !
kwa ujasili huu Ngoma Africa band inavuna inachopanda

Ngoma Africa band imetajwa kuwa muziki wake umefanikiwa kuzoa mamilioni ya washabiki na kuchangia kwa kiasi kikubwa kutukomeza fikira za kiubaguzi wa rangi zilizomo kwa baadhi ya wazungu barani ulaya.

Ngoma Africa band inasemekana kuwa na washabiki au wafuasi milioni 50 dunia nzima,na washabiki wengine milioni 11 wanapitia tovuti ya bendi hiyo at http://www.ngoma-africa.com

miongoni mwa wapenzi hao ni wapo wanawake na wanaume,watoto ,vijana na wazee wenye rika na mataifa mbali mbali,bila kujali itikadi za dini na matabaka ya maisha yao,wote wapo chini ya kivuli cha mzuka wa muziki wa Ngoma Africa Band aka FFU inayoongozwa na kamanda Ras Makunja aliyepindia akili kazi yake !

Tusikose kuwasikiliza FFU at www.ngoma-africa.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Kikamnda ketu ras makunja kweli kimeidatia akili kazi yake,mwe !mwe! mpaka kieleweke

    ReplyDelete
  2. Kikamnda ketu ras makunja kweli kimeidatia akili kazi yake,mwe !mwe! mpaka kieleweke

    ReplyDelete
  3. ffu wanajituma tumeiona kazi yao leo Morogoro muziki ulikua mkubwa

    ReplyDelete
  4. Jamani siku za nyuma nilishasema ya kwamba hapa tz kuhusu mambo ya miziki ni ya watu wa mji kasoro bahari yaani moro..nawashauri mjalibu kuchunguza..kwakweli wana vipaji lukuki tena watoto wadogo lakini wanatisha.

    ReplyDelete
  5. ffu aka watoto wa mbwa,hongereni sana

    ReplyDelete
  6. ffu aka watoto wa mbwa,hongereni sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...