Leo tunawaletea shairi la kuchanganya lugha (Kiswahili/English) lilioimbwa jana kwenye hafla maalum ya uchangishaji kwa ajili ya Jubilei ya miaka 50, iliyofanyika kwenye bustani ya Hospitali ya Igogwe. Shairi linaitwa Nusu Karne Hospitali ya Igogwe.
Hafla ilifanikiwa na hata waliokuwa mbali -k.m wabunge wote wa mkoa wa Mbeya- walishiriki kwa ahadi na michango kupitia akaunti zetu za:
IGOGWE HOSPITAL – JUBILEE 
AT NBC TUKUYU BRANCH A/C = 038201127120 na
 IGOGWE HOSPITAL – 
AT NMB TUKUYU BRANCH A/C = 61403500064.

Mbunge wa Mkoa Mama Hilda Cynthia Ngoye alipiga simu wakati wa hafla akiwa njiani kwenda NMB Dodoma kuweka 400,000/=, Mbunge wa Rungwe Magharibi aliahidi 500,000/=, Mbunge wa Ileje aliahidi 500,000/=, Aidha kwa pamoja wabunge wa mkoa wa Mbeya walichangishana 1.4m- hizi ni mbali na michango iliyotajwa hapo juu ya mbunge mmoja mmoja.

Mwenyekiti wa Bodi ya Madini- Richard Kasesela- aliahidi 1m kwa njia ya simu wakati hafla inaendelea.

Zaidi ya shilingi 25 milioni zilipatikana jana na taarifa zaidi zitatolewa kwa wadau wa Globu ya Jamii  siku ya J5 wiki ijayo. Michango kwa wenye nia njema na Igogwe Hospital na Mkoa wa Mbeya bado inaendelea kupokelewa. 

1.   Tufumbe macho tuombe kwa jina la Mungu Baba,
Nyoyo zetu zisiyumbe, tutazame msalaba,
Tusifu tena tuombe, Yesu wetu wa mahaba,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

2.   Tangu ilipoanzishwa Igogwe Hospitali,
Sana tumefurahishwa wa Karibu na wa mbali,
Maisha yamerefushwa kwa matendo na kauli,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

3.   Hii ni nusu karne, umri umetimia,
Nia ni watu wapone, ili wapate afia,
Maradhi waje wapime, maisha yawe murua,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

4.   Heko majirani nyote, Igogwe eneo zuri,
Kuilinda mali yote, pasiwepo na hatari,
Mila, desturi zote, kwenu zizidi shamiri,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

5.   Ziende kwake pongezi yule Padre Mellsoni,
Jitihada za uwazi kutafuta masikani,
Na hatimae ujenzi, hongera sana misheni,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

6.   Katoliki ni dhehebu, la kiroho na kimwili,
Watu wapate thawabu, wamjue Mungu kweli,
Maombi na matibabu, elimu pia injili,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

7.   Umma umenufaika kuwepo hospitali,
Vipimo vya kusifika, wataalam mbalimbali,
Maabara imeboreka, hongera kwa kutujali,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.
  
8.   Huduma mmeitoa pasipo dini kujali,
Eneo wala jinsia, kabila hata imani,
Mzidi kuendelea, awabariki Maanani,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.
  
9.   Waganga na wauguzi sifazo zawamulika,
Vipimo vyenye mionzi kwa wagonjwa hitajika,
Tumepata ukombozi kwa wakati muafaka,
Hii ni nusu karne, Igogwe Hospitali.

10.       Kituo chetu yatima, watoto wanalelewa,
Waliofiwa na mama, mahitaji wanapewa,
Afya zao wanapima, lishe wanahudumiwa,
Hii ni nusu karne, Igogwe isonge mbele.

11.      Basisita, bapatili, ndaga fijo mukulwasya,
Bakundwe mwe babombeli, abonywa mukubakasya,
Muli ni kisa naloli, buno mukubatetesya,
Finja kalongo bahano, ikipatala kya Igogwe.

12.        Tutwale ubonywa bwetu, tungifisaga kukaja,
Kukupimigwa bagwetu, fiki bamo tukufuja,
Ubukimwi mbungo jetu, ngulalusya ba kukaja?
Finja kalongo bahano, ikipatala kya Igogwe.

13.        Ukyala akisajege, ikipatala kikiki,
Nkyeni kyendelelege, ku bandu kije kifuki,
Abandu baponelege, basimanyege isoki,
Finja kalongo bahano, ikipatala kya Igogwe.

©Daudi Lugano Kilindu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Miaka yote nilidhani kuwa ninaifahamu English au angalau kuwa na uhakika kuwa neno fulani ni la lugha hiyo. Lakini baada ya kusoma shairi hili ambalo linaelezewa kuwa liko katika lugha za (Kiswahili / English)nimegundua kuwa English niijuwayo mimi siyo!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...