TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa John Gabriel Tupa salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kepteni (mst) James Charles Yamungu kilichotokea alfajiri ya leo, Jumatano, Agosti 22, 2012, kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam ambako alikuwa amelazwa.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amemwambia Mheshimiwa Tupa, “ Nimepokea kwa huzuni na mshtuko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kepteni Mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Mheshimiwa James Yamungu. “

Amesema Rais Kikwete katika salamu hizo: “ Kifo cha Kepteni Yamungu kimeinyang’anya nchi yetu na Serikali yetu mtumishi hodari na mwadilifu wa umma ambaye katika utumishi wake wote tokea alipokuwa Jeshi hadi anaingia uongozi wa siasa alithibitisha uaminifu wake kwa nchi yetu na uongozi wake.”

“Kufuatia msiba huu mkubwa, nakutumia wewe Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Tupa, salamu zangu za rambirambi, na kupitia kwako naitumia salamu zangu za dhati kabisa familia ya marehemu, wana-Mara na Wana-Serengeti wote ambako ndio kwanza alikuwa ameripoti kuanza kazi yake ya ukuu wa wilaya hiyo,” amesema Mheshimiwa Rais Kikwete na kuongeza:

“Napenda kuwajulisheni kuwa moyo wangu uko nanyi katika kipindi hiki kigumu. Nawaombea uvumilivu na subira na naungana nanyi kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, aiweke pema peponi roho ya Marehemu James Charles Yamungu. Amen.”

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
22 Agosti, 2012

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...