Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuelezea hali ya Ukuaji wa Pato la Taifa kwa 7.1% katika kipindi cha robo mwaka 2012.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es salaam.
Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa taarifa ya hali ya uchumi nchini na kufafanua kuwa pato la taifa la Tanzania limekua kwa asilimia 7.1 katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ikilinganishwa na asilimia 6.1 za mwaka jana.
Ukuaji huo wa asilimia 7.1 unatokana na ongezeko la uzalishaji katika shughuli mbalimbali za kiuchumi zikiwemo za kilimo, Uvuvi, Viwanda, Ujenzi na zile za utoaji wa huduma mbalimbali za jamii.
Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morrice Oyuke amesema kuwa lengo la utoaji wa taarifa hizo kwa vipindi vifupi vya vya robo mwaka unalenga kuwapatia wadau wa Takwimu za Pato la Taifa uwezo wa kutathmini mabadiliko ya ukuaji wa uchumi nchini.
Amesema kuwa jumla ya thamani ya pato la Taifa katika kipindi cha robo ya mwaka 2012 ni shilingi 4,220,535 milioni ikilinganishwa na kiasi cha shilingi milioni 3,940,261 za mwaka 2011.
Amefafanua kuwa ukuaji wa shughuli uzalishaji katika shughuli za kilimo nchini ulifikia asilimia 1.4 katika kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka 2012 zikilinganishwa na asilimia 1.2 katika kipindi hicho kwa mwaka 2011 kutokana na upatikanaji wa mvua za kutosha nchini katika mikoa inayozalisha mazao kwa wingi.
Amesema ukuaji katika shughuli za uvuvi ulikua asilimia 2.6 katika robo ya kwanza ya mwaka 2012 huku shughuli za uchumi katika sekta ya viwanda na Ujenzi ambayo inahusisha uchimbaji wa madini na kokoto ikikua kwa asilimia 14.3 ikilinganishwa na 0.8% za mwaka 2011.
Bw. Oyuke ameongeza kuwa ongezeko hilo la uzalishaji wa madini ya dhahabu linatokana na uzalishaji wa wa madini ya dhahabu kutoka kilo 8,140 kwa mwaka 2011 hadi kufikia kilo 16,736 kwa mwaka 2012.
Pia amebainisha kuwa shughuli za utoaji wa huduma za biashara za jumla na rejareja, ukarabati wa magari na pikipiki na vifaa vingine vya majumbani katika kipindi hicho zilifikia asilimia 9.0 huku shughuli za upangishaji nyumba na biashara zikiwa 8.2 %, uchukuzi na mawasiliano 16.4%, hoteli na migahawa 3.8%, Benki asilimia 15 shughuli za uendeshaji serikali 6.4%, Elimu 6.1% na utoaji wa huduma za Afya nchini zikikua kwa kasi ya asilimia 5.1.



Go go tz..ila kilichobaki muhakikishe wananch wa vijijini wanapata huduna zote muhimu..kama vile mashule mazuri..mahospitali mazuri..mabarabara mazuri. Na vinginevyo..ushari kwa wa tz wote tuchape kazi kwa uzalendo wa hali ya juu..tuache uvivu usiokua na maana yoyote.
ReplyDeleteUtoaji wa Takwimu za Ukuaji wa Pato la Taifa tu peke yake hautakuwa na maana yoyote iwapo ukuaji huo hautaongozana na takwimu za 1)kiwango cha kupungua kwa ukosefu wa ajira nchini au kiwango cha ongezeko la nafasi za ajira nchini kisekta, 2)kiwango cha ongezeko au kupungua kwa mfumuko wa bei nchini(inflation rate), 3)kiwango cha ongezeko au kushuka kwa Tija katika uzalishaji mali (rise or decline in labour productivity), 4)kiwango cha kupanda au kushuka kwa thamani ya shilingi yetu (rise or decline in exchenge rate valuations vs other international currencies,etc etc.
ReplyDeleteBila ya hizo takwimu au viashiria hivyo vya ukuaji uchumi,takwimu za kukua kwa pato la taifa tu peke yake hazina maana yoyote! zinaweza kupikwa bila ya shida yoyote kwa malengo ya kisiasa au kulinda ajira ya mtu!that is my personal opinion!
How come it does not feel like we are living in a high growth economy?
ReplyDeleteJambo linalonisikitisha katika utoaji wa takwimu za kitaifa umekuwa hauna utashi wa kuleta maendeleo halisi ya nchi, inasikitisha kutoa takwimu kama GDP, Inflation, Interest rates nk bila maelezo ya kina kuwa vimesaidiaje wananchi wa kawaida kupunguza gharama za maisha? Muwe na upeo zaidi na sio kutengeneza takwimu kihistoria
ReplyDeleteSiasa tupu. Pato limekua kivipi wakati wananchi wa kawaida wanateseka? Haisaidii kwenye vitabu kuonyesha pato limekuwa wakati sio kweli kwenye maisha ya kawaida ya mtanzania.
ReplyDelete"Uchumi umekuwa kwa asilimia 7.1 kutoka 6.1%" na umaskini kwa watu wa kawaida umekuwa kwa asilimia 27 -30%. Asanteni sana kwa takwimu nzuri.
ReplyDeletewapeni walimu chao.
ReplyDelete