Mbunge wa Jimbo la Rungwe Mashariki Profesa MARK MWANDOSYA  (pichani) amerejea Bungeni Mjini Dodoma leo ikiwa ni zaidi ya kipindi cha mwaka mmoja tangu awe nje ya Bunge kwa sababu za kiafya.

Profesa MWANDOSYA ambaye pia ni Waziri asiye na Wizara Maalumu amerejea Bungeni na kutoa shukrani zake kwa Watanzania wote na viongozi mbalimbali wa serikali akiwemo Rais JAKAYA KIKWETE ambaye alimsisitiza kwenda kutibiwa kutokana na kuona kuwa suala la afya ni muhimu.

Pia amewashukuru Wabunge wa vyama vyote vya siasa na kusema kuwa wamechangia kwa kiasi kikubwa yeye kupona haraka kutokana na kwamba katika kipindi chote alichokuwa akiuguwa walionesha umoja wao kwa kumfariji bila kujali itikadi za vyama.
Katika shukrani zake pia ameitaka jamii kutambua kuwa suala la afya ni muhimu kwani bila afya hawataweza kutekeleza majukumu mbalimbali ya kujileta maendeleo.
Profesa MWANDOSYA pia ametoa rai kwa Wabunge kupima afya zao mara kwa mara hata baada ya kustaafu Ubunge kwani wasihadaike na hali waliyonayo hivi sasa ya kujiona wazima kutokana na kukaa Bungeni muda mwingi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Mungu mwema ametenda kwako, nakupenda sana huna makuu, nakuombea upate heri na baraka pia, Kyala akutule, Emeni

    ReplyDelete
  2. one of the leaders that really makes me proud to be Tanzanian.May our good lord grant you much more strength!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...