Awali ya yote napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza Vodacom kwa kuja na wazo zuri la kutambua michango na umuhimu wa mitandao ya kijamii, hususan blogs na web site na kuamua kuwatunuku.


Pamoja na pongezi hizo, lakini mmekosea katika utekelezaji wake. Kwa mtizamo wa wahusika wengi (Blogers), tuzo mlizotoa baadhi zimeenda kwa wasiostahili na mmeacha wengi waliostahili kupata tuzo hizo.

Ingawa hamkuweka wazi vigezo vyote, lakini baadhi ya mlivyovitaja ni pamoja na blog kuwa inayofanyakazi (active), ambayo inaweka habari mpya kila siku, iwe inayoandika vitu halisi na siyo vya kukopi au kutafsiri kutoka BBC na mitandao mingine ya Kiingereza na kupesti.

Hali kadhalika mkasema kuwa web site au blog hiyo inachokiandika kiwe kimeandikwa na mtu mwenye ujuzi nacho, mkatoa na mfano kuwa kama ni mapishi, basi yaandikwe na mtu mwenye kujua mapishi. Pia mtandao huo uwe maarufu.

Bila shaka kwenye ulimwengu wa mitandao, unaposema mtandao fulani ni maarufu, ina maana unatembelewa na visitors wengi kwa siku, mtandao hauwezi kuwa maarufu kisha ukawa na visitors 500 au 800 tu kwa siku.

Bloggers maarufu nchini wanajuana na wanahesabika, inakuwa kichekesho inapokuja kutangazwa blog fulani ndiyo maarufu wakati haijulikani hata miongoini mwa bloggers wenyewe, achilia mbali wasomaji wengine.
 

Hawa ndiyo washindi wenyewe:

  1. Mikocheni Report,
  2. Issa Michuzi
  3. Wanamuziki Tanzania.
  4. Kipanya.co.tz
  5. Vijana FM
  6. Millardayo.com
  7. Taste of Tanzania
  8. Jamii Forums
  9. Mambo Magazine
  10. DJ Fetty Blog

Kwa mtizamo wa wengi, katika orodha hiyo ya watu kumi, ni wanne tu ndiyo walistahili na waliobaki hawakustahili kabisa, kwa sababu licha ya kuwa hawajulikani sana, lakini pia huoni hata namna ambavyo Vodacom, kama kampuni, inaweza kunufaika nao iwapo mtaamua kujitangaza kupitia kwao.
 Kuna Bloggers wameachwa ambao wao ku blog ndiyo maisha yao, wanalala, wanaamka, wanatembea, wanakula, wanakunywa, wanakaa wana blog tu. Wao na Blog, Blog na wao. Hakuna taarifa, breaking news au picha za matukio yote muhimu zinazowapita hapa nchini na hata katika kuripoti matukio ya promosheni ya Vodacom kwenye mitandao yao wako mstari wa mbele. Wengine kazi yao ni kukopi na kupesti kazi za wengine!
Pengine hatuyajui malengo ya Vodacom, kwa sababu kama kweli mnanataka kuthamini michango ya 'social media' na wao kunufaika na media hizo, basi mmekosea katika hili.
Waulizeni mliowatuma, wamefanya research ya kutosha na kuona hao washindi wana visitors wangapi na pageviews ngapi kwa siku? Je, Google Analytics Report zao zinaoneshaje? Na, je, habari na picha wanazoziweka kwenye mitandao yao, kweli ni za kwao, au wamekopi na kupesti tu kutoka kwingine?
 Naomba mliopewa kazi ya kuandaa tuzo hizi myachukue haya kama changamoto na kuyafanyia kazi ili msiharibu kazi nzuri inayofanywa na Vodacom nchini Tanzania na wala hatuyasemi haya kwa sababu ya chuki binafsi, bali kwa ukweli na uwazi tu!
 

Wassalaam!

 Global Publisherstz.com

"Great achievement, involves great risks"

Abdallah Mrisho

The General Manager

Global Publishers&General Enterprises Ltd

"The House Of Favorite Newspapers"

P. O. Box 7534, Dar es salaam

Tel: +255 22 2773356-7



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. How sad is!???Haya ndiyo matokeo ya kuwapa kazi watu ambao hawana weledi, ujuzi na uzoefu wa kazi zao....ni aibu kuchagua blogu ambazo hata hazifahamiki. Binafsi ninaweza nisiwe mjuzi saana lakini inawezekanaje ukachagua blogu bora ukamuacha mjengwa na haki ngowi?...HAIINGII AKILINI. VODACOM MLITAKA HAWA JAMAA WAWAPE KITU KIDOGO NDIYO MUWACHAGUE...????

    Hao washindi wenu nanao wafahamu ni wawili tu!!!!INASKITISHA SAAANA

    ReplyDelete
  2. ni kweli kabisa kwa mimi washindi ni michuzi na mjengwa blog,jamii forum wengine mmhh kucopy na kupaste

    ReplyDelete
  3. Anko Michuzi,jamii forums,millardayo ndio walio stahili,wengine ni kujuana tu that why wamepata hizo tuzo..duhh eti dj fetty...hahahahahahah!!!!

    ReplyDelete
  4. Sasa na wewe si utoe zawadi zako? Kwani tatizo ni lipi? Wenyewe wameona hao ndio washindi, kama wewe unao wengine basi toa zawadi zako.

    ReplyDelete
  5. wapo out u-turn kwenye umaarufu inaongoza

    ReplyDelete
  6. Abdallah Mrisho huwezi kulalamika wakati hujui vigezo vyote vilivyotumika kuchagua washindi,na kuna kila aina blogs siyo lazima zote ziwe zinatoa breaking news tu, kuna vitu vingi vya blogger anaweza kuhabarisha watu. Japo najua inakuuma siyo mbaya ukiwasilisha malalamiko yako Vodaco.

    ReplyDelete
  7. shamimu-zeze, u-turn, dina marios, michuzi, jamii forum, mjengwa, sinta etc eti mikocheni report ndio uchafu gani hapo big NOOOOOOOO!

    ReplyDelete
  8. LIST HII HAPA:

    1.JAMII FORUMS
    2.MICHUZI BLOG
    3.HAKI NGOI
    4.U-TURN
    5. N.K

    ReplyDelete
  9. MIe pia nasangaa mjengwa hayumo humu au hatangazi biashara zao labda, ila kweli hawa wengine sijawahi kuwasikia katika , ni kujuana au? kumbe ufisadi upo kila sehemu jamani enh?!

    ReplyDelete
  10. hmm! hata mm nimeshangaa!! eti watu 10 akiwemo Dj Fetty!! VODACOM wangechukua votes kwa wadau wangepata jibu kamili! hapo namba moja ni mzee Michuzi wengine ndo wanafuata! tunaomba msifanye hvyo tena!

    ReplyDelete
  11. Ndio maana hata Mikocheni Report blog kaandika kwenye blogu yake:

    "I was minding my own business, lamenting the fact that the blog doesn't get updated nearly enough and that there aren't enough hours in the day, et cetera, moan moan moan, woe is me. Then Vodacom Tanzania decided to include me in their inaugural intake of online Fellows. They just kinda emailed me out of the blue. Bam! Award! Fellowship! Want it?"

    Blogu maarufu Tanzania zinajulikana bana. Michuzi kweli kuna mtu ambaye hatambui mchango wako kwenye masuala ya ku-blogu? Kuna sehemu yoyote duniani unaweza kwenda na kukosa mwenyeji Mtanzania? Hata ukienda Afghanistan na ukasimama na bango lako kubwa Kabul city centre lililoandikwa kwa Kswahili kuwa wewe ni Michuzi na unatafuta pa kulala lazima utampata Mbongo tuu.

    Ingewasaidia Watanzania kama hiyo pesa vodacom waliotumia hapo wangeijumuisha kwenye profit ili ikatwe kodi.JK kasema juzi serikali haina pesa, mapato ya serikali madogo, wakati pesa yenyewe inasepea huku.

    Mdau Kabul

    ReplyDelete
  12. Wabongo, Mungu atusaidie. Wasingetoa kwa yeyote ingekuwaje? Kwani ni mashindano au tuzo?? Tatizo kukurupuka na kuanza kuongea mada bila kupima. Ndio maana tunafeli vitu vingi kisa ushabiki, lini tutajifunza?

    ReplyDelete
  13. Kwakweli haki haikutendeka. Kama blog ya kipanya inaonyesha ame apdate 2005 kwa pale chini, alafu hakuna kitu kwanza mimi ndiyo nimeiona leo, Vodacom jiulizeni mara 2.

    ReplyDelete
  14. mikocheni report ndio kitu gani. jamani hata mimi sio mjuzi sana lakini nimeona huu uchaguzi sio, eti DJ Fetty???

    ReplyDelete
  15. woteeee hao waigaji tu waalisia (bloggers wa ukweli)ni uncle misupu na mjengwa basi kamati ya kuchagua bloggers nahisi hata tasnia ya habari hawaijui fully kupeana tu, Ramadhan Kareem mkumbuke leo Chungu 12.

    ReplyDelete
  16. MIMI NAFIKIRI WALIKUWA WANAFUATA BLOG ZINAZOTOA MATUKIO SANA SANA,NA HASA HASA KWA KILA SIKU
    MTU UKISEMA U-TURN AU ZEZE NITASHANGAA SANA MAANA HAO SANA SANA WANATOA HABARI ZA MAISHA YAO,NA PICHA ZA WATU WA ULAYA,NA UDAKUZI WA MAMBO.NA HASA U-TURN NI BLOG YA WALIOOLEWA NA WAZUNGU.NA KUFUNDISHA JAMII JINSI WATU WANAVYOKULA MAISHA.
    KIDOGO ZEZE ANA NAFUU,,,NA KUHUSU MASWALA YA JAMII DINA NAMKUBALI SANA....
    MTU AKIAMUA KUTOA KITU CHAKE ANAMPA ALIYESTAHIKI KUPEWA WALA SIO KUPANGIWA NA MTU MWINGINE.

    NAFIKIRI VODA WAKO RIGHT!
    MAANA VIGEZO WAO NDO WANAVIJUWA.WALA SIO UWINGI WA KUTEMBELEWA NA WATU

    ReplyDelete
  17. hapo ni JF na Ankal kushnei...nimecheka kweli eti dj fetty,milard ayo ukiangalia hata age ya hizo blogs zao zinawasuta. JF thread moja tu unaweza kuta ina visitors 1000+ hiyo idadi hyo dj fetty haifikii kwa blog yake nzima ptu ptu ptutuuttututu shame on you vodacom and your allies. huyo Kelvin twisa kaweka watu wake wanaoudhuria disko lake...waone wale..

    ReplyDelete
  18. Kwa michuzi tumekubali mia kwa mia na hizo tunzo zina category kwa sbb kila blogger ana lengo lak, kama mchangiaji mada alivyosema hapo juu U-TURN yeye anatuonyesha maisha yake jinsi anavyokula bata, na zeze zamani alikuwa kotekote ila sasa naona kasimama sana kwenye Fashion, Dina mariios yeye ameamua kwenda kwenye maswala ya jamii, na Mashughuli yeye kasimama kwenye harusi za kitanzania na anatuletea mpaka zile za uswazi ambazo wengi wao ni ngumu kuyaona yanayoendelea huko! hata leo ukiwa nje ya nchi unaweza kumuonysha mtu jinsi tunavyosherekea harusi zetu, sitomuongelea sintah kwani hajui anachofanya huwezi kufungua blog halafu unasema mimi msomi je ingekuwa ni enzi zile nyerere wewe ndio msomi kama ilivyokuwa kwa Raisi wetu wa kwanza ungenyanyasa sana watanzanai?? kwa hiyo ukitaka kuwatunza hawa lazima uzingatie category sio kutoa tunzo tu!!! kwa sbb kila mtu anafanya kazi kwa utashi wake!!!

    ReplyDelete
  19. Mimi nakesha kwenye mtandao lakini baadhi ya blogu 'zilizoshinda' ndio kwanza naziona katika listi hii ya Voda. Michuzi, Millard Ayo na Jamii Forums nakubali lakini hao wengine nadhani kuna kasoro au labda Vodacom walikuwa na vigezo vyao ambavyo wengine hatuvijui. Siamini kama Mjengwa anaweza kukosa katoka orodha yoyote ya blogu tatu bora za Kibongo achilia mbali kumi.

    ReplyDelete
  20. Mimi nakesha kwenye mtandao lakini baadhi ya blogu 'zilizoshinda' ndio kwanza naziona katika listi hii ya Voda. Michuzi, Millard Ayo na Jamii Forums nakubali lakini hao wengine nadhani kuna kasoro au labda Vodacom walikuwa na vigezo vyao ambavyo wengine hatuvijui. Siamini kama Mjengwa anaweza kukosa katoka orodha yoyote ya blogu tatu bora za Kibongo achilia mbali kumi.

    ReplyDelete
  21. Kuzawadia bloggers tu kwa kuwashindanisha ni makosa. Ni sawa na kuwaambia waliotoswa waachane na habari za vodacom. Be careful, mnafikiri manjenga kumbe mnajiharibia wenyewe.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...