Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akikutana na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda mjini Maputo Msumbiji leo asubuhi kuzungumzia kutafuta suluhu katika mgogoro wa mpaka kati nchi hizo uliopo kwenye ziwa Nyasa.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda na wameelezea nia ya nchi zao kufikia suluhu kwa njia za kidiplomasia kupititia kamati maalumu iliyoundwa kushughulikia mgogoro huo (picha na Freddy Maro).
Tanzania haina nia wala mpango wa kuingia katika vita na nchi jirani ya Malawi kufuatia tofauti zao kuhusu mpaka katika Ziwa Nyasa. Rais Jakaya Kikwete amesema hayo leo kufuatia mazungumzo baina yake na Rais aw Malawi, mheshimiwa Joyce Banda.
"Namhakikishia dada yangu na watu wote wa Malawi kwamba hatuna nia wala mpango we kuingia vitani, hatuna matayarisho ya jeshi wala jeshi halijasogea popote kwani hakuna sababu" amesema na kuongeza kuwa "Mimi ndiye kamanda Mkuu wa Majeshi na sijapanga wala kutoa maelekezo ya vita".
Rais amesema hayo, mbele ya Rais Banda na kuongeza kuwa Kumekuwa na sintofahamu ya muda mrefu kuhusu suala la mpaka na tayari maafisa wa pande zote mbili wameshaanza kulizungumzia Kwa nia ya kulitatua Kwa Amani.
"Tuviachie vyombo vyetu vifanye kazi, hebu tuvipe nafasi, wanasiasa na waandishi we habari wajiepushe na maneno haya yanayosababisha taharuki na chokochoko, hayana maana yeyote wwachie diplomasia ifanye kazi yake" Rais amesisitiza.
Naye Rais Banda amesema amefurahishwa na kufarijika baada ya kuhakikishiwa kuwa hakuna vita na Rais Kikwete.
"Nimefarijika sana, swala hili limetusumbua sana, mpaka wa-Malawi wote wakaungana na kuwa kitu kimoja na kuzuia tofauti zao" amesema na kuvishukuru vyombo vya habari vya Malawi Kwa kuonyesha uzalendo na ukomavu katika suala hili.
Rais Kikwete yuko Maputo, Msumbiji kuhudhuria kikao cha viongozi wa Jumuiya Ya Maendeleo Kusini Kwa Afrika (SADC) uliofunguliwa tarehe 17 August, 2021 na unatarajiwa kumalizika leo jioni ( tarehe 18.august 2012)
Katika kikao cha Jana Tanzania imechukua uenyekiti wa Kamati ya Siasa, Ulinzi na Usalama kutoka Afrika ya Kusini ambapo uenyekiti wa SADC umechukuliwa na Msumbiji kutoka Angola, nafasi hizi ni za mwaka mmoja mmoja Kwa zamu.
Rais Kikwete anatarajia kurejea nyumbani Mara baada ya kikao hiki.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
18 August , 2012
Maputo, Msumbiji


Nina imani na mh raisi wetu Jakaya Kikwete kuwa kwa busara yake muafaka utafikiwa kwa amani na mh. Joyce Banda.Go JK we are praying for you.we dont want war with our neighbours!
ReplyDeleteMhe. Raisi wetu JK na Mhe.Bernard Membe,
ReplyDeleteMwelezeni wazi wazi huyo mama na hakuna sababu ya kupoteza muda ya kuwa mipaka ya kwenye maji inagawanywa miongoni mwa nchi.
MIFANO DUNIANI:
1.Great Lakes MAREKANI na CANADA:
Maziwa karibuni yite matatu (3) yamo ndani ya MAREKANI lakini kwa sheria hii mpaka umepita ndani ya maji na hivyo CANADA ina sehemu ya maziwa.
2.River RHINE EUROPE:
Mto umepita mipakani SWITZERLAND /GERMANY na GERMANY/ FRANCE, pia GERMANY/NETHERLANDS lakini mpaka umepita kati kati na kila nchi hapo ina maji yake.
3.Ziwa VICTORIA:
Tanzania ina maji yake, Kenya ina maji yake, Uganda ina maji yake, zaidi ya hapo hadi nchi kama Rwanda na Congo, hadi Sudan na Misri pamoja na kuwa hazipo ktk ziwa Victoria lakini zina haki zao kwa maji ya ziwa hilo.
Kama kigezo ni hicho cha wao kutaka ziwa lote, basi na sisi ziwa Tanganyika na ziwa Victoria yote ni yetu!
Zaidi huyo mama Joyce Banda anahitaji kuelimika na aelewe ya kuwa kusoma sana ama kusomeshwa na Mwingereza sana sio kigezo cha kuelimika!
LOOSER'S FACE,
ReplyDeleteWINERS V/S LOOSER:
Picha ya chini Raisi Madam Joyce Banda ana uso wa huzuni kwa dalili ya kuwa ni looser katika mchakato wa madai yake!
Uso wa msiba unaweza kutoa tabasamu?
Uso wa mtu si ndio hutoa dalili wajameni?
Madai ya Malawi yamethibitisha wao ni vilaza pasee, na pia kusoma sana sio kuelemika na vile vile kukaa karibu na Mahakama sio kujua sheria ,pia kusomeshwa na Mwingereza sio kuwa mwerevu, na kuwa kukifahamu Kiingereza vizuri sio kujua sheria!
ReplyDeleteHizi kanuni za Mipaka na sheria za mipaka zimeandikwa kwa Kiingereza na hawa wa Malawi, wa Nubi wa Sudani Kusini na Wazambia ndio wanaohesabika kama Waingereza waliobaki katika Afrika.
Huyu Mama ametukuta wastaarabu sana Tanzania na Raisi wetu JK angekuwa Paul Kagame angesha mchapa vikali sana!
ReplyDeleteMchina unaweza kushindana na Mbuyu?
ReplyDeletePicha ya chini Raisi JK yupo makini na anachokieleza na kuwa uso wake una hakika ni nini anasema, wakati mama Joyce Banda ameonekana ameshapoteza matumaini kabisa na madai yake.
Joyce Banda akumbuke ya kuwa Mhe.Raisi JK ni miongoni mwa Wanadiplomasia wazoefu na wakubwa sana ktk Afrika na Duniani, hivyo aelewe ni wazi atagaragazwa vikali katika mchakato wa madai yao umiliki wa ziwa Nyasa.
Mhe.Raisi Jakaya Mrisho Kikwete na Mhe.Benard Membe picha ya chini mpeni vipande vyake huyo mama aache kuota ndoto za mchana kweupe!
ReplyDeleteMadai ya umiliki wa Ziwa lote la Nyasa alishindwa baba yako Hayati Raisi Kamuzu Banda utaweza wewe binti Joyce Banda???
Ziwa Nyasa lote ni letu!
ReplyDeleteAma kweli kuitwa Muingereza wa pili sio kigezo cha kuelewa mambo na kuelimika!
Malawi na viongozi wake akiwemo Raisi wao wametuhibitishia hilo.
Si mchezo!
ReplyDeleteMama Joyce Banda picha ya chini anatia huruma sana, inaonyesha wazi ya kuwa madai ya ziwa Nyasa ni vigumu wao kupata watakacho.
Uso wake una huzuni za kushindwa hoja ktk dispute hii.
Kwani nyumbani mnapo uguliwa na mgonjwa akiwa anazidi kupoteza matumaini nyuso za watu wazima mnazionaje?
Kama Malawi watashinda madai haya ya kulitaka ziwa Nyasa lote, basi kule Amerika ya Kaskazini mpakani mwa Marekani na Canada yale maziwa makuu Superior,Huron,Erie,Michigan na Ontario itabidi Ramani ya mipaka ya Duniani iwe hivi:
ReplyDelete1.Marekani-itabidi wamilikishwe maziwa Michigan na Erie.
2.Canada-itabidi wamilikishwe maziwa Superior ,Huron na Ontario
KWA KUWA KTK MAZIWA YOTE HAYO YAKO UPANDE MMOJA WA NCHI KAMA HAPO JUU LAKINI KWA KUWA NI MIPAKA YA KWENYE MAJI IMEBIDI WAGAWANE MPAKA UPITE NDANI YA MAJI KWA MAZIWA TOTE MAKUU MATANO (5) BAINA YAO LICHA YA KUJALI YAPO UPANDE WA NCHI GANI.
NADHANI SHERIA HII NDIO ITATUMIKA KWA SUALA LA MALAWI NA TANZANIA.
3.Tanzania-na sisi itabidi tumilikishwe ziwa Tanganyika na Victoria!!!
..KOMON SENSI.. Ni kwamba jamaa HUKU WAMEONA KUNA MLO (ULAJI MWIGI) TANZANIA,HASA UKIJUMUISHA NA ZIWA NYASA. SASA WANACHOTAKA NI SISI TUGOMBANE ILI WAO WACHUKUE KIULAINI..GUUD EKZAMPLE...CONGO NA RWANDA...MATAIFA TAJIRI ASILIMIA KUBWA LA PATO LAO (NETI PROFITI) INACHNGIWA NA WIZI UNAOTOKANA NA(SOKO JEUSI).
ReplyDeleteUmiliki wa ziwa Nyasa lote kuwa lenu sio suluhisho la kujikwamua kiuchumi:
ReplyDeleteMadame Presidaa Joyce Banda kajipange kivingine nchini kwako na kuwa kumiliki ziwa lote kuwa la kwenu ''kinyume na taratibu na kanuni'' sio njia ya kuyafikia malengo ya kujinasua na ugumu wa kiuchumi nchini mwenu!
Lazima muelewe na mjifunze ujasiri wa kukabiliana na maisha!
Sisi tumebarikiwa na vingi sana zaidi ya sehemu ya hilo ziwa, gesi tunayo lukuki na tumeanza kuchimba!
Mtalijua jiji Malawi!!!
Ohhh nimefurahi sana nacheka Kitaalamu riziki mafungu saba kwa Mungu hakuna kubwaaa X 2
ReplyDeleteOhhh hamuipati bahati kwa Waganga mkikesha ohhh kwa Mungu hakuna kubwaaa X 2
MALAWI ACHENI KUOTA RIZIKI ZETU WANA WA TANZANIA TUMESHA JAALIWA, HAKUNA JINSI LABDA MUOMBE TUWASHIRIKISHE TU KWA BUSARA!
Hapo ;picha ya chini Mhe.Kikwete anaongea na mama Banda huku akicheka na kutabasamu kitaalamu, kwa vile anajua ni wazi tumeshindaaaaaa!!!
Tuacheni tuchekeleee na Raisi wetu mpendwa Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete!
Madame Joyce Banda pole sana!
ReplyDeleteBahati mbaya sana unabishana na Mwanadiplomasia Mkongwe na Balozi wa muda mrefu katika Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Huyo si mwingine bali ni Mhe.Raisi JK !
Mamaa Banda Joyce kwa picha ya chini ni dalili tosha ya kuwa umeshavuna mawe!
ReplyDeleteWewe umepata uso wa mbuzi ghafla, mamaa uso umekuporomoka kama wa mbuzi tofauti na ulvyokuwa unatoa hotuba nchini kwako kwa njia ya Televisheni, ukilihutubia Taifa lako kwa jazba na majigambo!
Kiko wapi sasa?, ujasiri wako umeyeyuka ghafla!
Ni wazi wazi kuwa umesha garagazwa vibaya kabisa!
Umemuona Mhe. Kikwete hapo anavyotabasamu kwa ushindi?
Picha ya chini ni wazi mama Joyce Banda anaonyesha amekwisha elekezwa Kibla na amekwisha kula kula kisu!
ReplyDeleteUsoni matumaini yameshapotea kabisa na ndio kama anavyoshuhudia mwenyewe kwa macho yake wanaume wanatoka na makoti yao.
Chezea Tanzania weye?
Mama wa watu ameshakubali yaishe,sura yake inaonyesha dhahiri.Chezea JWTZ weyeee!!
ReplyDeletembona Nyerere na Kawawa walikubali kwamba ziwa nyasa ni mali ya Malawi 100%? wengi wenu ni wavivu kwa kusoma. nendeni kwenye hansard za miaka ya 60 wakati chifu mhaiki alipotoa hoja kuhusu mpaka na Malawi ktk bunge la Tanganyika mtakuta mambo yote humo.
ReplyDeletemi nadhani nchi ya malawi ulikuwa mkoa wa tanganyika miaka iliyopita, au. Wataalamu wa mipaka, hii imekaaje? Malawi ni sehemu ya Tanganyika, kwa nini tusirudishe ,koa wetu. Mheshimiwa rais ebu toa mwongozo.
ReplyDeletena nyie wengi pia hamna elimu mnajisemea tu kama mlivosema wenyewe kuwa hamna elimu,kuwa ziwa sehemu ya Tanzania au Malawi si sababu ya kuwa la mtu,hata Nile Canal ipo Egypt lakini wamiliki ni waliojenga,
ReplyDeletewacha hapo kuna visiwa vingi mfano vinavyomilikiwa na Muingereza hizo ni oversees territoris tu mfano kilichopo Argentina ,au Diego Garcia ni cha Seychelles na kipo na wao lakini wamiliki ni US na UK
lakini mfano zaidi ni kuwa Cyprus ipo chini ya Mturuki lakini ni ya Mgiriki,hapo ni suluhu kwanza kwenda kwenye history kisha ndio diplomasia tusijipe moyo.
Hiyo picha ya chini namuona Membe ana hasira na huyo mama, anatamani amzabe kibao!
ReplyDeleteHuyu Mama anafikiri vita ni rahisi,tangu lini rais wa kike akaongoza vita,waoga hawa.Ana mume huyu???Rais wetu ni SOJA anafahamu vizuri madhara ya vita
ReplyDeletenyie angalieni picha wenzenu wanachukua maziwa,Nimejaribu kuirekebisha wikipedia KWA KUWA mwandishi amebadilisha jina kabisa kutoka LAKE NYASA kwenda Lake Malawi,
ReplyDeletenimejaribu kurudisha lake Nyasa baadhi ya sehemu mkipata nafasi pitieni na rekebisheni kila kwenye Malawi,
Pili mipaka ya sehemu inaonesha Ziwa hili lipo Malawi kwa historia ya NYASA ni Nyasa land,na maana yake ni LAKE LAKE (lake nyasa) so hapo tutumie diplomasia tugaiwe kipande cha 3rd largest lake in AFRICA,
tatu kuhusu kuwepo Tanzania si kigezo hiyo tuangalie ukweli wabongo tukizidiwa hatuna hoja tunakwenda kuongelea mambo yasiyohusu ya picha.