Katikati ni Rashid Matumla akipima uzito wake (kilo 76) mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani). Kushoto ni promota wa pambano hilo, Siraji Kaike na kulia ni daktari, Michael Abraham na Maneno Oswald.
 
Katikati ni bondia Maneno Oswald akipanda kwenye mizani kupima uzito wake (kilo 56)
Mmoja wa kati ya mabondia watakaosindikiza pambano hilo, Venas Mponji akipima uzito.

 
…Juma Shaban akipima uzito.

 
Kushoto ni Maneno Oswald, promota wa pambano hilo, Kaike Siraji na Rashid Matumla wakiwa katika picha ya pamoja hotelini hapo.
Mabondia wa kitambo Bongo, Rashid Matumla na Maneno Oswarld, leo walikuwa katika Hoteli ya The Atriums kwa ajili ya kupima uzito kujiandaa kwa pambano kali litakalochezwa siku ya Iddi Mosi katika Ukumbi wa Dar Live jijini, Dar.
  Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari, promota wa pambano hilo, Kaike Silaji, kila bondia yupo katika afya nzuri na wapo tayari kwa ajili ya pambano hilo siku ya Idd Mosi.
“Niwahakikishie wapenzi wa mchezo wa ngumi kufika kwa wingi siku hiyo kwani mabondia wetu wamejipanga vilivyo kuhakikisha kila mmoja anajiwekea heshima ya kuwa mshindi. “Kutakuwepo na mapambano ya utangulizi ya vijana matata katika mchezo wa Boxa kabla ya Maneno na Matumla hawajapanda ulingoni,” alisema Kaike.

STORI/PICHA: ERICK EVARIST & GEORGE KAYALA/ GPL.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. MsemaKweliAugust 18, 2012

    Sasa huyo Maneno ana kg 56, na huyo Matumla ana kg 76 wanapigana kwenye uzito gani? Mbona uzito tofauti? Mabingwa wa ngumi hebu nielimisheni uzito unatakiwa uwe sawa au unaweza pitiliza na kama unaweza pitiliza je kwa kiwango gani?

    ReplyDelete
  2. Naona mara hii mmeamuwa kutoonyesha mpaka mwisho (miguuni kwenye scale) hizo image zao, naamini mmeficha hiyo scale isiyostahili kufuatia kiwango chake kuwa duni na kutokuwa professional kwa kupimia uzito wa mabondia wetu. Wahusika jaribuni kutatuwa tatizo ili mwende na wakati na kuwa professional katika fani yenu, acheni ya janja ya nyani.

    ReplyDelete
  3. Mi naona siku hizi,hizi ngumi ni kuganga njaa tu hapa bongo kwa mabondia wengine. Kwanza uzito wa 76 na 6 inakuwaje.
    Pili huyu matumla haonekani kama anapiga zoezi na kuheshimu afya yake kama mwana michezo bali upigania experience, ebu cheki shepu yake.
    Hawa mabondia watangulizi wanaonekana wako fiti zaidi.
    Harafu haya maneno ya prove if you are not a robot nadhani unatakiwa kuwa roboti kuyasoma maana huu mcharazo unatutatiza sisi watu wazima na macho yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...