Na George Jinasa

Kwa mujibu wa ibara ya 63  ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 (“Katiba”) Bunge linayo mamlaka ya kuisimamia na kuishauri Serikali. Mamlaka haya hutumiwa na Bunge katika vikao vyake mbalimbali kwa kujadili bajeti na taarifa mbalimbali za Wizara na inapobidi kutunga sheria zinazolenga katika kurekebisha kasoro katika mwenendo wa Serikali.
Kwa mujibu wa ibara ya 107 A, mamlaka ya kufasiri sheria na kutoa haki yako mikononi mwa Mahakama.  Hakuna hata sehemu moja katika Katiba ambapo Bunge limepewa mamlaka yoyote ya kuisimamia na kuishauri Mahakama. Nafasi ya Bunge kuirekebisha Mahakama katika mfumo wa “checks and balance”, ni kwa njia ya kutunga sheria.
 Na hilo limefanyika mara nyingi japo mara nyingine limetumika vibaya kama pale Mahakama Kuu ilivyobatilisha kifungu katika Sheria ya Uchaguzi kilichokuwa kinazuia mgombea binafsi na Bunge likajibu kwa kurekebisha Katiba na kuliingiza sharti hilo katika Katiba. Kwa kufanya hivyo, suala la mgombea binafsi lilifanywa kuwa la kikatiba badala ya sheria ya Bunge kama ilivyokuwa mwanzo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mdau,
    George Jinasa, Majaji siyo Miungu pia wapo ambao wana udhaifu wa kimaadili n.k

    Tumeona mfano huko Kenya, Naibu Jaji Mkuu wa Kenya Mh. Nancy Baraza alionekana ana upungufu wa kimaadili kwa kutumia nafasi yake kunyanyasa raia.

    Hivyo Mh. Tundu Lissu anastahili pongezi kwa kusaili 'utendaji' ,'maadili' , 'uzoefu' na pia 'shule' za 'baadhi ya waheshimiwa Majaji.

    Mifani ipo mingi Italy, Uingereza, Kenya n.k na sasa hata Tanzania ambapo 'maamuzi' ya baadhi narudia baadhi ya Majaji lazima uhojiwe na siyo siasa.

    Mh. Tundu Lissu ni mwakilishi wa jimbo lake na pia wananchi ambao siyo wa jimbo lake ambao mara nyingi wameshindwa kupata fursa ya kuwakilisha maoni yao juu ya udhaifu wa aina zote za baadhi ya Majaji.

    Ripoti ya Mh. Tundu Lissu inabainisha bila shaka yoyote yale ambayo wananchi wanyonge walikuwa wanahoji kila siku.

    Hapa hakuna siasa bali ni kusaili utendaji, maamuzi, maadili na uwezo wa kumudu ongezeko wa kazi kwa baadhi ya waheshimiwa Majaji.

    Mdau
    Kisarawe

    ReplyDelete
  2. Mtu aliyeandika haya kweli ni mwanasheria? Anajua anachokiongelea au anataka na yeye asikikike tuu? Akiwa mwaka wa kwanza chuoni alijifunza jinsi ya ku-reason kweli? Mwanasheria mzima anapotosha watu namna hii kwa kuandika DS tuu hapa?

    Kwa mfano kwenye kipengele cha tatu cha "JAJI KUAJIRIWA BILA KUWA NA SIFA KITAALUMA" ni kweli kabisa kuwa sifa za kitaaluma za mtu kuwa Jaji Tanzania Zanzibar ni sawa na za Tanzania bara. Pia ni kweli kabisa kuwa Rais kwa kushirikiana na Jaji Mkuu anaweza kumteuwa mtu kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa yule ambaye anasifa ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania au Mahakama Kuu ya Zanzibar. Pia ni kweli kabisa kuwa jaji mhusika wakati anateuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa alishakuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar.

    Lakini ni makosa makubwa sana kusema kuwa kwa kuwa alishakuwa jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar basi Rais na Jaji Mkuu hawakuwa na sababu yoyote ya maana kutilia shaka uteuzi wake kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Kusema hivyo sio kupotosha jamii tuu bali pia fani ya sheria. Unataka kusema kuwa kama Zanzibar wakimteua mtu kichaa kuwa jaji wa mahakama kuu Zanzibar, basi Rais kwa kushirikiana na jaji mkuu wanaweza kumteua huyo jaji kichaa kuwa jaji wa mahakama ya rufaa kwa sababu tuu alikuwa jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar? Ndivyo unavyo-reason?

    Ukweli ni kwamba Zanzibar walifanya makosa makubwa kikatiba kumteua jaji asiye na degree ya sheria kuwa jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar. Huyo jaji alikuwa jaji wa mahakama kuu ya zanzibar kinyume na katiba ya Zanzibar. Hakuwa na degree ya sheria kama katiba ya Zanzibar inavyosema. Sasa Rais hawezi kikatiba kumteua jaji asiye na degree kuwa jaji wa mahakama ya rufaa kwa sababu tuu eti alikuwa jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar.

    Kufanya kosa sio kosa bali kurudia kosa ndio kosa. Zanzibar walifanya kosa kwa kumteua mtu asiye na degree ya sheria kuwa jaji wa mahakama kuu ya Zanzibar. Rais nae alirudia kosa hilo hilo kwa kumteua huyo jaji asiye na degree ya sheria kuwa jaji wa mahakama kuu kinyume na katiba.

    Kwa mujibu wa Ibara ya 94(3) ya Katiba ya Zanzibar, 1984, “mtu hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji au Kaimu Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na shahada ya Sheria ya Chuo Kikuu kinachotambuliwa au Chuo cha aina hiyo; au awe au amewahi kuwa Jaji wa Mahkama zilizofanana na hii kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yoyote ya Jumuiya ya Madola au Mahakama ya Rufaa kutoka Mahakama hizo; au awe Mwanasheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba; au awe na uzoefu wa Jaji au mwanasheria kwa pamoja usiopungua miaka saba.”

    Jaji Mbarouk hajatimiza hata moja ya masharti hayo ya Katiba ya Zanzibar. Jaji huyu hana shahada yoyote ya sheria inayotambuliwa na mamlaka ya ithibati ya Tanzania kama inavyotakiwa na Ibara ya 109(7) ya Katiba. Jaji huyu ana stashahada ya juu ya sheria (Post Graduate Diploma in Law) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Shahada ya Uzamili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha nchini Uingereza.

    The issue here is not whether he was a judge of the High Court of Zanzibar. The issue here is whether he have the required qualifications, i.e. law degree, to be a judge in the first place. Kama hana degree na kwa kuwa Rais aliapa kuwa atailinda katiba ya Tanzania basi inambidi atengue uteuzi wa huyu jaji mapema iwezekanavyo.

    ReplyDelete
  3. To the best of my knowledge and belief Judge Mbarouk is capable for holding such a position, kilichopo ni siasa tu za chochoroni baina ya Lissu na aliyempaka matope ambazo hata hivyo, siko tayari kuzianika hapa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...