Vijana wa kazi walionyesha staili yao mpya ya kucheza.
NA MWANDISHI WETU 
WASANII wa muziki wa kizazi kipya Mwasiti Almasi na Zena Mohamed ‘Shilole’ wanatarajiwa kusindikiza uzinduzi wa bendi ya Skylight wakati wa Sikukuu ya Iddi Mosi. 
 Akizungumza na vyombo vya habari jana kiongozi wa Skylight Band Aneth Kusila ‘AK47’ alisema uzinduzi huo utafanyika kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Giraffe, uliyopo Mbezi Beach. 
AK47 alisema uzinduzi huo utakuwa wa namna yake kutokana na uwezo mkubwa walionao wasanii wanaounda Skylight.

“Mashabiki wote wa muziki Tanzania waje washuhudie vipaji hivyo na jinsi tulivyojiandaa kuwapa burudani ya aina yake,” alisema AK47. 

Skylight Band inaundwa na wakali kama AK47 na Mary Lucos, ambaye aliwahi kushiriki mashindano ya Bongo Star Search (BSS). 
Wengine ni Joniko Flower na Sam Machozi, ambao wote wametoka Machozi Band, inayomilikiwa na Lady Jay Dee. 
Baada ya uzinduzi huo Skylight Band watafanya onyesho jingine kwenye ukumbi huo wa Giraffe siku ya Iddi Pili, ambapo Dj Nelly ataonyesha uwezo kwa kupagawisha mashabiki kwenye maonyesho yote mawili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Waislam hatutaki muinasibishe sikukuu yetu kwa mambo ya kumuudhi ALLAH, kwanini hizo ngoma zenu hamzitambulishi siku nyengine ila siku yetu hii tukufu. Watanganyika tulio waislam tuige mfano wa wenzetu wa Zanzibar ngoma na madisko marufuku kunasibishwa na sikukuu yetu wailam

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...