FAMILIA ya Brigedia General, January Nyambibo inatoa shukrani kwa ndugu jamaa na marafiki wote walioshiriki katika mazishi ya mpendwa wao aliyefariki Agosti 15, 2008 na kuzikwa Agosti 18 katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Umetimiza miaka minne tangu ulipotutoka, unakumbukwa na watoto wako Husna, Misana, Mr & Mrs Malu Stonchi, Hamisa, Masha, Mkama, Bwire, Perus, Peter, mkeo Rukia Abdalah Kitogo na wajukuu zako Haji, Amanda, Jenifer, Angel, Mkama, Devon, Robert, Muhsin, Rukia na Familia yote ya Nyambibo.
Sisi tulikupenda lakini Mungu alikupenda zaidi
Bwana ametoa na bwana ametwaa.
Amina



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...