Mshambuliaji wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa (8) akitafuta namna ya kuweza kumpita beki wa timu ya Botswana, Zebras Oscar Neenga wakati wa mechi Kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Molopolole mjini Gaborone Bostwana, timu hizo zilitoka Sare ya kufungana mabao 3-3.
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", Mrisho Ngassa akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya taifa ya Botswana,Zebras Edwin Elerile wakati wa mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja Molepolole nje kitogo ya jijini la Gaborone.timu hizo zilitoka Sare ya kufungana mabao 3-3.
Mabeki wa timu ya taifa "taifa stars" wakimwangilia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Botswana akifunga bao la tatu wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Molepolole mjini Gaborone.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Wafungaji ni nani?? Hivi tukushindwa kwenye michezo yenyewe, hata jisni ya kuripoti hiyo michezo tunashindwa?? safari ni ndeeeeeefu muno!!

    ReplyDelete
  2. Erasto Nyoni(Pen)...(1-0)
    Botswana............(1-1)
    Mwinyi Kazimoto.... (2-1)
    Botswana.... (2-2)

    HALFTIME.............2-2

    Botswana .......... (3-2)

    Mrisho Ngasa .......(3-3)

    Stars tumerekebisha tatizo la kufunga magoli,Ukuta tena imezibuka.

    ReplyDelete
  3. Hivi hamuoni magolikipa wa karne hii wanavyojaa golini?? Huyu wa kwetu anafaa kubadilishwa. Na kama kungekuwa na wafungaji wenye akili na kumsoma vizuri kipa kwenye recorded video, wallahi JKJ angekuwa analoweshwa migoli kila mechi. Enzi zangu nisingepata shida kumtungua, kwani kuna nafasi nyingi ziko wazi kuuipitisha mpira kutinga wavuni!!

    Ize, sijui ma-forward wa sasa hivi wanashindwa nini!

    ReplyDelete
  4. Huu ndo ushindi wa hii timu kwa fikra zangu za haraka haraka naikumnbuka ushindi mmoja tu wa hii timu uleee wa BURKINAFASO zilozobakia nyingi hivi kudroo au kufungwa

    ReplyDelete
  5. Aisee Tanzania tuna vipaji vya soka,yaani usipime!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...