Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Issa Machibya katikati akipata maelezo kuhusu umeme wa jua toka kwa wataalamu.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya akitoa zawadi kwa wachezaji wa mpira wa miguu baada ya mashindano yaliyoitishwa na wafadhili wa umeme wa jua MCA Tanzania.
Bi. Hadijah Rashid Nyembo Mkuu wa Wilaya ya Uvinza akielekezwa namna umeme wa jua unavyoweza kufanya kazi (Picha na Afisa Habari Kigoma RS).
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Luteni Kanali Mstaafu Issa Salehe Machibya jana alizindua mradi wa umeme wa jua ambao utawanufaisha wakazi wa Wilaya za Kasulu na Kigoma vijijini. Mradi wa umeme wa jua katika hatua ya kwanza umelenga katika vituo vya afya, shule, masoko, vyama vya ushirika, na Vyombo wanavyotumia wavuvi.
Akizungumza katika hafla ya uzinguzi huo katika uwanja wa Mwanga Centre uliopo Kigoma mjini Mhe. Machibya alisema mradi huo unafadhiliwa na Millenium Challenge Account (MCA), mradi huu unatarajiwa kudumu kwa mwaka mmoja. Mradi hu utagharimu dola za Kimarekani milioni 4.7 sawa na shilingi za Tanzania trilioni 7,05 .
Naye Mhandisi wa masuala ya umeme wa jua kutoka MCA Bw. Andrew Mzava alisema kuwa serikali kupitia Wizara ya Nishati Pamoja na wafadhili wa mradi huu wameandaa wataalamu wa kufunga na wa kuhudumia pia wauzaji wamepewa mafunzo ili waweze kuwauzia watu bidhaa bora.
Aliwasisitiza watu , taasisi mbalimbali zijitokeze kutumiwa umeme huo wenye gharama nafuu na hauchafui amzingira.





Tatizo sio wao ni serikali yetu haioni umuhimu wa umeme wa jua, huku nje umeme wa jua hauna ushuru mkubwa, hapo nyumbani ushuru wake unakatisha tamaa bora uendelee kutumia tanesco.
ReplyDelete