Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen leo (Agosti 1 mwaka huu) ametangaza kikosi cha wachezaji 21 kwa ajili ya mechi ya kirafiki itakayochezwa ugenini Agosti 15 mwaka huu.

Wachezaji walioitwa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager wanatakiwa kuripoti kambi kwenye hoteli ya Tansoma, Dar es Salaam, Agosti 8 mwaka huu saa 1 jioni tayari kwa mazoezi yatakayoanza siku inayofuata.

Makipa walioitwa kwenye kikosi hicho ni Deogratias Munishi (Azam), nahodha Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni nahodha msaidizi Aggrey Morris (Azam), Erasto Nyoni (Azam), Kelvin Yondani (Yanga) na Shomari Kapombe (Simba).

Viungo ni Athuman Idd (Yanga), Frank Domayo (Yanga), Haruna Moshi (Simba), Mrisho Ngassa (Azam), Mwinyi Kazimoto (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Salum Abubakar (Azam) na Shabani Nditi (Mtibwa Sugar).

Wachezaji wanaounda safu ya ushambuliaji ni John Bocco (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Said Bahanuzi (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC).

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kikosi kiko pouwa, ila hili la makipa wawili toka timu moja Kocha kachemka, mwadini kamwona wapi wakati hiyo kAGAME yote kakaa Benchi!? na amemwacha Ally Mustapha ambae hakufungwa hata Goli Moja Kagame na Kaonesha Kiwango!!

    ReplyDelete
  2. Nadhani ipo haja ya kuitafutia jina jingine hii timu kwani haina hadhi ya kuitwa 'Timu ya Taifa'. Hii timu ni kombaini ya timu za Azam, Yanga na Simba pamoja na hao wachace kutoka DRC. Hivi hakuna wanaoweza kufaa kutoka timu nyingine kama Mtibwa, Coastal Union, Ruvu JKT kutaja kwa uchache ukiachilia mbali mchango wa timu kutoka Zanzibar kama Mafunzo ambao sote ni juzi tu tulishuhudia soka lake? Tuache dhihaka na tuwe makini.

    ReplyDelete
  3. Wambura Ugenini wapi?Hujui siku hizi mashabiki wanasafiri na timu?Sema tukate tiketi za ndege mapema.Hapo

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...