Wakala wa Usafiri wa Haraka (DART Agency) uliyoko katika Jengo la Ubungo Plaza Ghorofa ya Kwanza unawakumbusha wote waliokuwa Wamiliki wa nyumba za Gerezani Kota-Kariakoo, wanaostahili kulipwa fidia, wafike katika ofisi hii ili walipwe fidia yao baada ya kukamilisha taratibu za malipo. Ofisi ya Wakala wa Usafiri wa Haraka  iko wazi Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia saa 1:30 asubuhi hadi saa 9:30 alasiri. 


Watu wote waliokuwa Wamiliki wa nyumba za Gerezani Kota-Kariakoo wachukue barua zao kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gerezani Magharibi, zilizoandikwa tarehe 27 Julai, 2012 zinazoonyesha malipo stahiki ya fidia ya nyumba iliyobomolewa na kama fidia imekwishachukuliwa au bado.

Tafadhali kila aliyekuwa Mmiliki wa nyumba tajwa ambaye hajachukua fidia yake aje na yafuatayo:
Nakala ya mkataba wa umiliki wa nyumba.
Barua yenye picha ya utambulisho kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Gerezani Magharibi pamoja na barua yetu ya tarehe 27 Julai, 2012.
Jina la Benki na Tawi, Jina la Akaunti na namba ya kuweka fedha za fidia zitakazotolewa.

Kukamilika kwa zoezi hili ni muhimu kwa maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya Mabasi Yaendayo Haraka.

MTENDAJI MKUU
WAKALA WA USAFIRI WA HARAKA

S

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kutokana na uwezo wangu mdogo wa kufikiri, nilidhani wamiliki wa nyumba zilizovunjwa walitakiwa walipwe na kupewa notice ya kuhama kabla ya uvunjaji kutekelezwa.

    ReplyDelete
  2. mambo si haya ndugu zangu,nchi yetu taratibu inawekwa sawa , wenye haraka zao tangulieni,lakini kumbukeni kwamba ,kutangulia siyo kufika (mnakumbuka ROME imejengwa muda gani ?? NOT in one day) ABBA aliimba ( andante andate) Zebedayo msema kweli. Na wanaodai mafao yenu ,nendeni mkachukue,hakuna dhuruma wala rushwa. God bless Tanzania.

    ReplyDelete
  3. siku ya uvunjaji ilikuwa kituko watu walikurupushwa alfajiri na mapema na hali ilikuwa tafrani.Nilidhani walishamalizana

    ReplyDelete
  4. Duuuh zebe ahhh zebedayo kila sehemu upo Ubwabwa Leo wapi? Ushavaa kanzu na kibakora? Bongo sirudi mpaka uzeeke zebe eti unasema bongo kumeendelea haha tueleze kumeendelea nini? Ahhhhh unajua pale kwenye m'buyu umekwatwa ule kumejengwa bonge la petrol station. Ehh sasa hayo ndio maendeleo. Wewe mti unaota kwa miaka 500 unaukata kwa mda siku moja. Kwa Sababu ya petrol station? Bongo sirudi maisha!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...