Assalam alykum Warahmatullahi Wabarakatuh:
Kwa niaba ya East African Community Slough tunapenda kuwatangazia Waislam wote wa Slough na Vitongoji vyake kua Sala ya Eid itasaliwa siku ya Jumapili tarehe: 19-08-2012 Mahala ni Langley Pavillion, Langley Road, Slough, SL3 8BS.
Takbira zitaanza saa moja na nusu 7:30 am na Sala itasaliwa Saa mbili kamili 8:00 am,
sote wake kwa waume, wadogo kwa wakubwa, tunaombwa kuhudhuria kwa wingi katika ibada hii, ili kupata fadhila za siku hii adhimun.
Jazzakallahu 'lkhairy...


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...