Taswira hizi zilinaswa na kamera ya Globu ya Jamii hivi karibuni wilayani Ngorongoro, moja kati wilaya tano zinazounda mkoa wa Arusha nchini. Wilaya hii inapakana na nchi ya Kenya kwa upande wa kaskazini, Wilaya ya Monduli kwa upande wa Mashariki, Wilaya ya Karatu kwa upande wa Kusini na mkoa wa Mara kwa upande wa Magharibi.
Eneo maarufu na linalojulikana sana ulimwenguni la Ngorongoro kreta liko katika wilaya hii. Pia mlima wenye volkano hai ujulikanao kama Oldoinyo Le Ngai upo katika wilaya hii. Kwa maana hii wilaya nzima ya Ngorongoro ni eneo lililohifadhiwa. Kabila kuu katika wilaya ya Ngorongoro ni Wamasai. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Ngorongoro ilihesabiwa kuwa 129,776
Morani
Vijana
Kinamama |
Mkeka wa nguvu kuelekea Ngorongoro
Eneo maarufu na linalojulikana sana ulimwenguni la Ngorongoro kreta
Mlima wenye volkano hai ujulikanao kama Oldoinyo Le Ngai
hii nchi wee acha tu, sasa hao wanawake uwezekano upo wa kuolewa na kabila jingine na kuhamia Dar ?
ReplyDeleteSura za hao akina dada sio wamasai bali ni wambulu a.k.a WAIRAQ
ReplyDeleteSi mchezo.Picha ya juu kabisa wa kwanza kutoka kulia...macho ya mtego hayo!!
ReplyDeleteDavid V
Ah, mavazi asilia na miwani ya jua! Imenikumbusha Is It Possible? kwa wale ma-bookworm wenzangu...
ReplyDeleteWarembo wa Mujini kumekucha!
ReplyDeleteEnhee wa mujini mukae mkao wa kiupinzani maana na wenzenu mademu wa msituni wameanza kuujua uzuri kwa kuanza kuvaa mawani.
Kazi kwenu!
Nikirudi Bongo jambo moja ambalo ni lazim nilifanye ni kutembelea sehemu hizi. Ngoja nikuambie kisa kilichonisibu.Tulikuwa kwenye hafla baada ya harusi ya jamaa huko London, vijana kama wanne hivi wakanizunguka walipoambiwa kuwa miye natoka Tanzania, wakaanza kuzungumza na kuisifu nchi, na matembezi yao ya Ngorongoro,aib,mie nimezaliwa Moshi, lakini hiyo Ngorongoro naisikia tu.
ReplyDeleteAnkal picha nzuri sana.
ReplyDeletePicha zote hapo unaweza ukatengeneza pot card nzuri sana.
Hasa m-tz alie nje anafurahia sana mantdar hizi asilia.
Tanzania yetu ni nzuri.
Eti uamsho ndo wanasema HAWAUTAKI.
MDAU ZNZ
Hahahahaha mdau hapo juu umenikumbusha mbali sana Is It Possible? sijui kama siku hizi bado vitabu hivyo vinasomwa mashuleni, na kumbukuka na kile The River Between
ReplyDeleteYaani kuna mdau hapo made my day! alivyosema kama kuna uwezekano wa kuoa na kumwamishia Dar! ushaona vijana wa kimasai walivyo na misuli nguvu za kutosha wamepikwa wamepikika.. wewe mdau wa Dar softiiii hujui hata kupambana.. utapata nafasi kweli?
ReplyDelete