![]() |
| Hapa ni Magomeni Kagera ambako ujenzi wa barabara maalumu wa kupita basi ziendazo kasi katika barabara ya Morogoro road umeshamiri |
Hapa ni daraja la Tegeta ambako ujenzi wa barabara za njia mbili kutokea Mwenge unaendelea kwa kasi. Kazi hizi zitabadilisha kabisa muonekano wa jiji la Dar baada ya muda si mrefu na pia kupunguza foleni za magari kwa kiasi kikubwa.




Ni neema kwetu ila nashauri tujitahidi kuzingatia viwango vya kimataifa hasa alama za barabarani tusiishie kujenga kama ya mbagara inatupa hasara sana.
ReplyDeletedah nzuri sanaaaaaaaa 2
ReplyDeleteHuyo jamaa aliyekaa hapo barabarani kama machinga anafanya nini? Ila kama viwango vya kimataifa na alama za barabarani hazitazingatiwa itakuwa sana na kupoteza pesa bure. Watu wazingatie sheria na taratibu za barabara ikiwemo kutokukatisha barabara ovyo.
ReplyDeletehivi mbona hakuna habari kuhusu hayo mabasi yenyewe? ni haya haya yetu ama yanaagizwa mabasi rasmi? ya serikali ama ya nani? taxi na daladala hazitakatiza humo na kusimama kushusha na kupakia? taswira na stori kamili inapatikana wapi?
ReplyDeletenashauri meya wa jiji ama waziri wa ujenzi/uchukuzi azungumze na wakazi wa Dar kwa kina juu ya suala hili, na ajibu maswali. mkuu wa kikosi cha usalama barabarani naye awepo katika mazungumzo hayo. wadau na watumiaji wa barabara wawakilishe hadhira itakayouliza maswali ya moja kwa moja. wengine tutapiga simu na kutuma maswali kwa barua pepe. kipindi kiwe kirefu (tv na radio), na pia kuwe na mhadhara/mjadala hadharani. liongeleeni hili suala sana wakati huu, msisubiri hadi barabara zianze kutumika.
Sidhani kama barabara hizi zote zinajengwa kwa mapato yetu wenyewe. Nian uhakika kwa mfano barabara ya Mwenge-Tegeta wajapni pia wanachangia
ReplyDeleteAnyway regardless of where the money come from, tunashukuru kwamba hatimaye tutakuwa na barabara angalau kilometa chache zenye nafasi ya kutosha. Hata hivyo serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kupanua barabara ya Morogoro angalau mpaka Kibaha. Kuishia Kimara hakutasaidia sana kupunguza adaha watu waendao na wanaotoka mikoani wanpata.
pale mwenge kwenye hiyo barabara mnayosema tunajenga kwa pesa zetu wenyewe kuna bango Grant aid from the people of japan.(pesa za walipa kodi wa Japan)nahili linahitaji akili nyingi.Tusidanganyane.Tena haya ni matusi na sielewe kwa nini tunaendelea kulipa kodi kwani kila kinachofanyika nchi hii ni msaada au mkopo na matokeo yake si mazuri mbeleni ( no free lunch )
ReplyDeletePale mwenge kuna bango,Limeandikwa IS A GRANT AID FROM THE PEOPLE OF JAPAN .Jamani hilo nalo linahitaji akili nyingi ( Maana Msaada kutoka kwa walipa kodi wa japan)haya ni matusi.sasa sisi kodi tunayolipa inafanya nini?sio mradi huu tu mingi tu inayoendelea hivi sasa.Kwani kama sio msaada ni mkopo.Tusipoangalia itatufikisha hadi kuamuliwa nini cha kufanya.tuache ushabiki kwa hili.
ReplyDeletesio pesa zetu baba misaada hizi zote mbili
ReplyDeleteMmh! Mimi baada ya kuona ya wakenya hii bado hainishtui. Na sisi tu demand lane 4X4 bwana. Mji unakuwa hiyo side, muda si mwingi, yatuwa yale yale ya traffic.
ReplyDeletesio fedha zetu wenyewe, ujenzi wa barabara ya mwenge tegeta ni msaada kutoka Japan na upanuzi wa barabara za basi ziendazo kasi ni mkopo kutoka IBRD aka World Bank
ReplyDeletekaka hizi sio pesa zetu wenyewe,lets be honest na tusikose shukran kwa ndugu zetu. Huu ni msaada wa serikali ya Japan kaka.
ReplyDeleteSorry kaka michuzi hii barabara ya Mwenge-Tegeta haijengwi kwa hela zetu ni msaaada kutoka Serikali ya Japan
ReplyDeleteNdudu wadanganyika amkeni sasa muwe macho na hawa watu hicho kinachosemwa ni msaada kutuka watu wa japanisi sahihi,ngoja niwafungue macho ni kweli wanatuletea pesa zisemazwo ni msaada kumbukeni toka tupate uhuru hadi leo serikali na idara zake zote imekuwa ikitumia magari kwa ajiri ya shuhuri zake za usafiri made in japani,sasa piga hsabu magari mangapi tunanunua kila mwaka si magari tu spare parts zake pia,wafanyacho hapo ni kutufumba macho ili tuendelee tumia magari yao.
ReplyDeleteIt's 2012, hiyo barabara ni ndogo sana, December mwakani foleni itakuwa palepale. Kwanini tusifanye kitu mara moja na cha uhakika. Sasa mjini wote unahamia Tegeta/Mbezi halafu barabara ndio imeongezwa lane moja tu. Where is future vision, tatizo la kuwa na viongozi waliosoma 1950's
ReplyDeleteKwa wale wanaofikiri hizi njia zitapunguza foleni mnajidanganya. Tatizo litakuwa pale Mwenge barabara zinapoishia kutakuwa na msongamano mkubwa sana.
ReplyDelete