Hapa ni Magomeni Kagera ambako ujenzi wa barabara maalumu wa kupita basi ziendazo kasi katika barabara ya Morogoro road umeshamiri
Hapa ni daraja la Tegeta ambako ujenzi wa barabara za njia mbili kutokea Mwenge unaendelea kwa kasi. Kazi hizi  zitabadilisha kabisa muonekano wa jiji la Dar baada ya muda si mrefu na pia kupunguza foleni za magari kwa kiasi kikubwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Ni neema kwetu ila nashauri tujitahidi kuzingatia viwango vya kimataifa hasa alama za barabarani tusiishie kujenga kama ya mbagara inatupa hasara sana.

    ReplyDelete
  2. dah nzuri sanaaaaaaaa 2

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa aliyekaa hapo barabarani kama machinga anafanya nini? Ila kama viwango vya kimataifa na alama za barabarani hazitazingatiwa itakuwa sana na kupoteza pesa bure. Watu wazingatie sheria na taratibu za barabara ikiwemo kutokukatisha barabara ovyo.

    ReplyDelete
  4. hivi mbona hakuna habari kuhusu hayo mabasi yenyewe? ni haya haya yetu ama yanaagizwa mabasi rasmi? ya serikali ama ya nani? taxi na daladala hazitakatiza humo na kusimama kushusha na kupakia? taswira na stori kamili inapatikana wapi?

    nashauri meya wa jiji ama waziri wa ujenzi/uchukuzi azungumze na wakazi wa Dar kwa kina juu ya suala hili, na ajibu maswali. mkuu wa kikosi cha usalama barabarani naye awepo katika mazungumzo hayo. wadau na watumiaji wa barabara wawakilishe hadhira itakayouliza maswali ya moja kwa moja. wengine tutapiga simu na kutuma maswali kwa barua pepe. kipindi kiwe kirefu (tv na radio), na pia kuwe na mhadhara/mjadala hadharani. liongeleeni hili suala sana wakati huu, msisubiri hadi barabara zianze kutumika.

    ReplyDelete
  5. Sidhani kama barabara hizi zote zinajengwa kwa mapato yetu wenyewe. Nian uhakika kwa mfano barabara ya Mwenge-Tegeta wajapni pia wanachangia

    Anyway regardless of where the money come from, tunashukuru kwamba hatimaye tutakuwa na barabara angalau kilometa chache zenye nafasi ya kutosha. Hata hivyo serikali inatakiwa kuchukua hatua za haraka kupanua barabara ya Morogoro angalau mpaka Kibaha. Kuishia Kimara hakutasaidia sana kupunguza adaha watu waendao na wanaotoka mikoani wanpata.

    ReplyDelete
  6. pale mwenge kwenye hiyo barabara mnayosema tunajenga kwa pesa zetu wenyewe kuna bango Grant aid from the people of japan.(pesa za walipa kodi wa Japan)nahili linahitaji akili nyingi.Tusidanganyane.Tena haya ni matusi na sielewe kwa nini tunaendelea kulipa kodi kwani kila kinachofanyika nchi hii ni msaada au mkopo na matokeo yake si mazuri mbeleni ( no free lunch )

    ReplyDelete
  7. Pale mwenge kuna bango,Limeandikwa IS A GRANT AID FROM THE PEOPLE OF JAPAN .Jamani hilo nalo linahitaji akili nyingi ( Maana Msaada kutoka kwa walipa kodi wa japan)haya ni matusi.sasa sisi kodi tunayolipa inafanya nini?sio mradi huu tu mingi tu inayoendelea hivi sasa.Kwani kama sio msaada ni mkopo.Tusipoangalia itatufikisha hadi kuamuliwa nini cha kufanya.tuache ushabiki kwa hili.

    ReplyDelete
  8. sio pesa zetu baba misaada hizi zote mbili

    ReplyDelete
  9. Mmh! Mimi baada ya kuona ya wakenya hii bado hainishtui. Na sisi tu demand lane 4X4 bwana. Mji unakuwa hiyo side, muda si mwingi, yatuwa yale yale ya traffic.

    ReplyDelete
  10. sio fedha zetu wenyewe, ujenzi wa barabara ya mwenge tegeta ni msaada kutoka Japan na upanuzi wa barabara za basi ziendazo kasi ni mkopo kutoka IBRD aka World Bank

    ReplyDelete
  11. kaka hizi sio pesa zetu wenyewe,lets be honest na tusikose shukran kwa ndugu zetu. Huu ni msaada wa serikali ya Japan kaka.

    ReplyDelete
  12. Sorry kaka michuzi hii barabara ya Mwenge-Tegeta haijengwi kwa hela zetu ni msaaada kutoka Serikali ya Japan

    ReplyDelete
  13. Ndudu wadanganyika amkeni sasa muwe macho na hawa watu hicho kinachosemwa ni msaada kutuka watu wa japanisi sahihi,ngoja niwafungue macho ni kweli wanatuletea pesa zisemazwo ni msaada kumbukeni toka tupate uhuru hadi leo serikali na idara zake zote imekuwa ikitumia magari kwa ajiri ya shuhuri zake za usafiri made in japani,sasa piga hsabu magari mangapi tunanunua kila mwaka si magari tu spare parts zake pia,wafanyacho hapo ni kutufumba macho ili tuendelee tumia magari yao.

    ReplyDelete
  14. It's 2012, hiyo barabara ni ndogo sana, December mwakani foleni itakuwa palepale. Kwanini tusifanye kitu mara moja na cha uhakika. Sasa mjini wote unahamia Tegeta/Mbezi halafu barabara ndio imeongezwa lane moja tu. Where is future vision, tatizo la kuwa na viongozi waliosoma 1950's

    ReplyDelete
  15. Kwa wale wanaofikiri hizi njia zitapunguza foleni mnajidanganya. Tatizo litakuwa pale Mwenge barabara zinapoishia kutakuwa na msongamano mkubwa sana.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...