Historia kubwa ya jiji la London lililopo nchini Uingereza kama kituo cha mambo ya uchumi duniani, kimeufanya mji huo uwe ni kivutio kwa uchumi unaofuata sheria za kiIslam. Inaaminika kwamba mzunguuko wa pesa kupitia soko la London ni mkubwa kuliko wa sehemu nyingine yoyote duniani.  
Benki ya kwanza ya kiIslam ilianzishwa nchini Uingereza mwaka 2004 ktk mji wa Birmingham. Mwaka 2006 aliyekuwa waziri mkuu wa wakati huo Gordon Brown alitangaza malengo yake kwamba atapenda London iwe ni kituo kikubwa duniani cha uschumi wa Kiislamu. 
UK imekaribisha watafiti wengi wa maswala ya benki za kiIslam na university nyingi  kama vile CASS business school, Reading University, Durham University, Loughborough University na Surrey University zimeanzisha  courses za uchumi wa kiislam.
The Chartered Institution of Mangement Accountants (CIMA) hivi sasa inatoa certificate ambayo ni ya kwanza kutolewa na Professional chartered accountancy body. Kwa maelezo zaidi wasiliana na www.ijuebankiyakiislam.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. daaah!!! eti bank ya kwanza ya kiislam ilianzishwa nchini Uingereza mwaka 2004? mmmmh habari nyengine bwana? mbona ipo miaka mingi saaana tu yani about more than 20 years,hizo habari nyengine sijui mnazitoa wapi jamani? mdau toka buja

    ReplyDelete
  2. Mzungu anafanya chochote kile atakachopata fedha. Hivi karibuni walikuwa wakitaka kupiga marufuku wanafunzi wasije kusoma hapa UK kutoka nje. Lakini amengundua kuwa vyuo vyao vinaondeshwa na fedha wanazolipa wanafunzi wageni. Bila pesa ya wageni vyuo vyao vitafungwa. Hivyo serikali ya UK imeamua wageni waendelea kupewa viza kusoma na maprofesa wote wamefurahia agizo hilo, raia wa mitaani wamepewa uelewa kuhusu wanafunzi wa kigeni. Hapa nilipo mimi sasa ukiwa mwanafunzi unabebelezwa na raia na kila kona wanakuchekelea ili pesa ibaki UK.

    ReplyDelete
  3. Nahisi hizi benki za Kiislamu zitaweza kuwa afadhali, maana benki nyingine zote zimekosa sifa, yaani "Trust" ambao ndio msingi mkubwa wa benki. Kuanzia mabenki makubwa yenye jina zuri huko majuu, taasisi za fedha za baadhi ya makanisa, kuja mpaka hapa kwetu kwenye mabenki yanayoshangilia kushirikiana na makampuni ya minada kuuza mali za wakopaji!!

    Sehemu nyingine hali ya biashara au uchumi unapoyumba, benki inayostahili kuitwa benki hukaa na wakopaji kuandalia jinsi ya ku-reschedule mkopo ili uweze kulipika. Hapa kwetu wanakimbilia kukutisha kuchukua mali zako, hata bila kufuata utaratibu. Sasa mkimfanya mkopaji kila siku afikirie jinsi ya kurejesha, ni lini atafikiri jinsi ya kukuza biashara? Maafisa wengine kwa kukimbilia kukuza "loan book" zao ndio wanaowashawishi watu wengine kukopa, pindi akijua kuwa biashara inaweza isilipe. Hii ni sawa na mtu mmoja maarufu hapa mjini anayekukopesha akijua una mali ili achukue utakaposhindwa, na hata kukuondoa duniani!!

    Islamic benki, naomba muingie sokoni mkijua hizo kasoro na mateso wanayoyapata wahitaji, hakika biashara mtapata!!

    Na kwa sisi wananchi tutakaohitaji huduma za benki, tujipange vizuri kifedha ili tujiepushe na maafisa wanaojali "loan book" zao kuliko hatima ya biashara zako na maisha yako kifedha!!

    ReplyDelete
  4. Mwaka 2006 waziri mkuu wa UINGEREZA hakuwa Gordon Brown Sahihisha hapo tafazari.Alikuwa ni Tony Blair harafu Mwezi SITA 2007 ndio aliachia kiti cha MADARAKA akaingia huyo Gordon Brown.....
    MDAU...Mtanzania HALISI.

    ReplyDelete
  5. Ipo haja ya wataalam wa uchumi kuzisoma kozi hizo na kujua tofauti iliyopo kati ya mifumo miwili hiyo ya kibenki. Nanadhani Tanzania imeanza vizuri ktk upande huo na nivyema kama BOT wakaungana kama bado hawajafanya hivyo na nchi nyingine kuzikaribisha benki hizo

    ReplyDelete
  6. Hii haina uhusiano na kashfa ya Standard C. Bank...maana nimeona CNN wametuhumiwa kuhifadhi ela za maghaidi na ela za Iran. Wadhungu ukiwa na pesa mbona watafata mila na desturi zako.

    ReplyDelete
  7. Samahani kulikua na makosa ya uchapishaji iliyokusudiwa ni the Islamic Bank of Britain ndio iliyoanzishwa mwaka 2004. Accept our apologies

    ReplyDelete
  8. Samahani kulikua na makosa ya uchapishaji iliyofunguliwa mwaka 2004 na the Islamic bank of Britain

    ReplyDelete
  9. Ni kweli mdau Gordon Brown wakati huo alikua the chancellor of the exchequer. samahani kwa usumbufu

    ReplyDelete
  10. Ninakupongeza ijue benk ya kiislam kwa kuweka maelezo yako vizuri na kwa kuomba msamaha kwa usumbufu uliojitokeza, huo ndio uungwana na sio kufanya kosa baadae ukang'ang'ania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...