Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akikata utepe kuzindua vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiswahili leo jijini Dar es salaam. Kulia ni mkurugenzi wa washirika wa huduma za Afya duniani (CLSI) Connie Adams.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiowaonyesha wadau wa huduma za afya nchini (hawapo pichani) moja ya kitabu cha mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu kilichoandikwa kwa lugha ya Kiswahili mara baada ya uzinduzi. Wanaoshuhudia ni mkurugenzi wa washirika wa huduma za Afya duniani (CLSI) Connie Adams (kulia) na Magreth Mhando, Mkurugenzi wa huduma za Kinga wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii (kushoto).
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kuhusu sekta ya afya nchini mara baada ya kuzindua vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara nchini.
Viongozi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wakiongozwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya kutoka ndani na nje ya nchi leo jijini Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa vitabu vya mwongozo wa kutekeleza mfumo wa usimamizi wa ubora wa huduma za maabara kitabibu.Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Huyu Waziri anawakilisha jimbo la Zanzibar lakini anaongoza wizara sio ya muungano, hapa vipi wadau?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...