TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Serikali, kuanzia leo tarehe 01 Agosti, 2012, imewavua hadhi ya ukimbizi wakimbizi 38,050 wa kutoka Burundi wanaohifadhiwa katika kambi  ya wakimbizi ya Mtabila iliyoko wilayani Kasulu mkoani Kigoma.
Uamuzi huu wa kuwavua hadhi ya ukimbizi umefanywa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Wakimbizi.

Kufuatana na Sheria hiyo mkimbizi anapoteza hadhi ya ukimbizi kama mazingira yaliyomfanya kuwa mkimbizi yatakuwa hayapo tena, na atavuliwa hadhi hiyo kama ataendelea kukaidi maagizo halali ya kumtaka kurejea kwao kwa hiari.

Hatua ya kuwavua hadhi ya ukimbizi wakimbizi hawa imefikiwa baada ya Serikali za Tanzania na Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kujiridhisha kuwa hapakuwa tena na sababu ya kuendelea  kuwahifadhi wakimbizi hao baada ya hali ya amani kurejea nchini mwao na hivyo kuwataka kurejea kwao.

Zoezi la kuwasaili wakimbizi waliopo katika kambi ya wakimbizi ya Mtabila lilifanyika kuanzia mwezi Septemba hadi Desemba mwaka 2011 kwa lengo la kubaini kama walikuwepo wakimbizi wenye sababu za msingi za kuendelea kuwepo nchini, ambapo ilibainika kuwa wakimbizi 38,050 hawakuwa na sababu za kuendelea kuwa wakimbizi.

Kufuatia matokeo ya zoezi hilo, Kikao cha Pande Tatu, kilichojumuisha wawakilishi wa Serikali  za Tanzania na Burundi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), kilifanyika jijini Bujumbura nchini Burundi tarehe 22 Februari, 2012 na kukubaliana kwa pamoja kuifunga kambi ya Mtabila ifikapo tarehe 31 Desemba, 2012.

Baada ya kuwavua hadhi ya ukimbizi, raia hawa wa Burundi sasa wataendelea kusaidiwa kurejea kwao kwa hiari hadi tarehe 31 Desemba mwaka huu, ambapo Kambi hiyo ya Mtabila itafungwa rasmi, na wale ambao watakuwa hawajaondoka baada ya tarehe hiyo watachukuliwa kuwa ni wahamiaji haramu, na kushughulikiwa kufuatana na Sheria ya Uhamiaji.

Historia ya hifadhi ya wakimbizi hapa nchini ilianza tangu mwaka 1961 ambapo Tanzania ilikuwa na idadi kubwa ya wakimbizi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, idadi ambayo katika miaka ya tisini ilifikia takribani milioni moja, 641,386 kati yao wakiwa ni wakimbizi kutoka Burundi.

Zoezi la kuwarejesha  kwao wakimbizi wa Burundi lilianza rasmi mwaka 2002 baada ya nchi yao kurejea katika hali ya amani na hadi sasa kambi nane zilizokuwa zikihifadhi wakimbizi toka Burundi zimefungwa. Kambi hizo ni Karago, Mtendeli, Kanembwa na Nduta zilizokuwa wilayani Kibondo, na Muyovosi iliyokuwa wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Kambi nyingine zilizofungwa ni Kitali iliyokuwa wilayani Biharamulo, Lukole A na B zilizokuwa wilayani Ngara, mkoani Kigoma.
Kambi ya wakimbizi ya Mtabila ndiyo itakuwa ya mwisho kufungwa katika mlolongo wa kambi zilizokuwa zikihifadhi wakimbizi kutoka Burundi hapa nchini.
  
Imetolewa na Isaac J. Nantanga:
MSEMAJI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. vipi kuhusu kambi zilizokuwaga wilaya ya mpanda, KAMA VILE KATUMBA, MWESE...Je zilishafungwa??

    ReplyDelete
  2. Tanzania kueni na moyo wa ubunadamu hasa tukichukulia kipindi hiki cha mufungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.Wapeni ulaia nao waishi kama laia wengine.Sio kwamba hawataki kwao kwawalio wengi Kwao hawapajui wamezaliwa ukumbizini kwahio hawana pa kwenda.

    ReplyDelete
  3. Mbona mliwapa uraia wakimbizi 400,000 toka Somalia inakuwaje hao mnawarejesha kwao? mngewapa uraia kama mlivyofanya kwa wasomali kama wanataka na si kukimbilia kuwarudisha makwao.

    ReplyDelete
  4. Binafsi siamini iwapo Tanzania inaweza kutoa uraia kwa waombaji 400,000 kutoka taifa moja! Iwe tunatoa mawazo yanayoingia akilini na tuepuke kila aina ya hisia mgando.

    ReplyDelete
  5. Huyo aliye sema wakimbizi 400,000 wakisomali ana data, si kiasi hicho alichokitaja, hata Warundi waliopo Mpanda ambao wamepata uraia ni 160,000 hii inajumuisha makazi ya zamani ya Katumba, Mishamo na Ulyankulu. Je waweza kufikiri hiyo ni namba ndogo sana ama unataka nchi yetu iwe ya wahamiaji tu. Hapana hawa wa Mtabila warudi nyumbani. Niwajuavyo hawa wa Mtabira hawafai kabisa nawaomba mfatilie tabia zao.

    ReplyDelete
  6. Nyie mmewavya ukimbinzi na nyie mtavuliwa ubinadamu.Kumbukeni kilichotokea Burundi na sisi kinaweza kututokea.Muwaoneeni huruma wajameni hao ni Binadamu Kama sisi.Kwanza kabisa namraumu alie anzisha mipaka mara hapa TZ mara hapa USA.kwani siku ya hukumu sote tutakua pamoja tukisubili hukumu kutoka kwa Mungu.Rais wetu JK tujua wewe upo karibu na watu saidia hao watu wanao teseka.

    ReplyDelete
  7. Mwakei tunarudigi ku fasi ya Bujumbura!

    Rakini makubwa yamemukuta ALEXIS SINDUHIJE sijui tutapokerewaje na Nkurunzinza?

    ReplyDelete
  8. Si jukumu la nchi kuwapa uraia bali wao kwanza ndio wanatakiwa kuonyesha nia ya kutaka uraia

    ReplyDelete
  9. Mdau unayetaka wapewe uraia waambie kuwa taratibu za kuomba uraia zipo wazifuate siyo tu eti kwa sababu walikimbia vita ndiyo wapewe uraia.Na wewe unayesema mwezi wa Ramadhan waachwe mbona hujasema wafungwa waliopo magerezani waachiwe? Kila nchi ina taratibu zake na pengine hujui uharibifu wa mazingira walioufanya katika mikoa waliyohifadhiwa. Kuzaliwa Tanzania isiwe sababu kwani wazazi wao wanajua vijiji/miji waliyotoka wakati wa vita. Huko ndiyo kwao wasing'ang'anie nchi za wenzao warudi kwao. Hifadhi wamepewa ya kutosha na serikali pamoja na watanzania wanastahili pongezi.

    ReplyDelete
  10. Warejee kwao hali imetulia na huduma zimerejea kuwa za kawaida juzi hapa tumeona wakati wa kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Burundi hali ni nzuri, au nyinyi ndiyo wapinzani mliyo uhamishoni? ikifika usiku mnasumbua, mchana mnakuwa wakimbizi wema hali ya ukimbizi ni mbaya siyo ya kufurahiya sana, kupewa migao kila kukicha na masimango mengi kutoka kwa watumishi wa mashirika, rudini nyumbani mkalijenge taifa lenu hakuna ugonvi usiyokwisha malizenu tofauti zenu kwenye meza na si bunduki; bunduki siyo suluhu ya yote sanasana inaongeza chuki. Wakimbizi wengi huwa ndumila kuwili wengine wanaenda Burundi wakirudi wanatoa habari za uzushi, wanawajengea khofu wale waliyozaliwa makambini na wakinamama. Hali inabadilika kila siku, unapanga hivi kesho yake unakuta mabadiliko hujui wanavyowasiliana kumbe wako kwenye biashara kimaslahi.ECHCER kama waitavyo wenyewe wanayo maslahi binafsi pia kwa kuwepo wakimbizi nchini,mfano mishahara minono, marupurupu manono, manunuzi ya medical items na nonmedics items ya mabilion ya shilingi, ambayo gharama ya vyote huwa ni kupata mafungu ya fedha kwa wafanyakazi kupata mapesa yasiyo na kikomo. Serikali imefanya vyema kufunga camps hizi.

    ReplyDelete
  11. msio ijua kigoma nyamazeni na myaanche hayo hivyo hivyo, hata mkielezwa hamtaelewa, tuichiewe kigoma yetu

    ReplyDelete
  12. Mwandishi unasema uongo mwaka 1961 ilikuwa hakuna Tanzania. Tupe habari zilizoenda shule tafadhali.

    ReplyDelete
  13. KAMBONA ALIKAA UINGEREZA MPAKA AKAFA NA WALA HAJAWAHI KUFUKUZWA AU KUVULIWA HADHI YAKE YA UKIMBIZI.
    TATZO SIYO HALI SALAMA HUKO KWA, JE WAPO VIZURI KISAIKOLOJIA KWA YOTE YALIYOWAKUMBA TANGU MIAKA YA 90?
    KUNA WATU WAMEUWANA KATI MJOMBA NA MKWE HUKO KWA SABABU YA UTUTSI NA UHUTU. HUKO MPAKANI MWA CONGO DR NA RWANDA HALI SI SHWARI LEO MNAWARUDISHA HUKO BURUNDI, MNATEGEMEA HALI ITARUDI KUWA NA AMANI.
    ELIMU NI UPEO MKUBWA WA MAISHA. TEMBEENI MSOME SIO KUKAA DARASANI TUU BASI MNAONA MPO JUU KWA KILA KITU.

    ReplyDelete
  14. Mi naunga mkono swala zima la wakimbizi kurejea makwao. Burundi iko shwari na muda wa kurudi umewadia. Kama hamtajenga nchi yenu, hakuna atakae wajengea. Ni jambo la kusikitisha sana kuona warundi wamezagaa kila kona ya dunia kwa sababu za kikimbizi. Dunia inaelewa kwamba hali sasa ni shwari na hakuna haja ya kupatiwa hadhi za kikimbizi. Bado hamjachelewa. Rudini kwenu mkakae mezani ili kutatua tofauti zenu. Tanzania ina majukumu mengi na si busara kuendelea kuishi makambini wakati kwenu hakuna tatizo kubwa kama mnavyodai.

    ReplyDelete
  15. Zina ra kusema. Kweri watu hamuerewi! Chacha ata wakiludi!.....aaa! bathi! Kitwahili thanifu thina tena! Kwa helini. Bwana Mathubu bost na hii!

    ReplyDelete
  16. me nataka mmoja wa kike ili nimuoe apate uraia kirahisi nipo hapa..loptz@yahoo.co.uk, awe mrembo na mrefu kuanzia sentimita 150, rangi yoyote ile, dini ni vizuri zaid akiwa mwislam, elimu angalau form four...lakn hata kama hajasoma sio mbaya kama vigezo vingine anavyo..uaminifu ndio silaha kuu.asiwe amewahi kuolwa na kwa maana hio asiwe na mtoto...changamkieni dili hili.mwisho kutuma maombi ni mwezi wa 10 mwaka huu

    ReplyDelete
  17. Ninyi wadau mnaosema Warundi ni wabaya kwa hiyo wasipewe uraia hamjatenda haki. Mbona hamuwasemi hao Wasomali 400,000 waliopewa uraia huko Tanga miaka ya hivi karibuni? Kuna watu wabaya kama wasomali? Kama mmewapa wasomali uraia, basi hata warundi wapewe uraia kama wanataka. kwishnei!!!

    ReplyDelete
  18. Wajameni wengine mue na upeo wa kutafakali na kutofautisha kati ya Jua na Mwezi.Nataka nikuelimishe hasa wewe mdau unae linganisha wakimbizi na wafungwa alafu wewe unaleta zako gozigozi.wenzao hao wameikimbia Nchi yao zaidi ya miaka(35)

    ReplyDelete
  19. Kwani bongo sasa imekuwa dili? maweeeeeeeee bongo njaaa tu.umeme wa mgao.maji ujichimbie kisima.ukimwi ndio usiseme.raisi ana ndege yake.madawati shule hamna. viongozi shopping ulaya watoto wao kusoma ulaya. sirudi labdA NYERERE AFUFUKE

    ReplyDelete
  20. Nashauri serikali isichelewe kuwaondoa hapa nchini na itangaze taratibu na ni lini wataondoka.

    ReplyDelete
  21. Nashukuru kwa njinsi watu wanavyo changia. Ila nimegunduwa wengi wamechoshwa nawakimbizi. Natamani ningeona kila mmoja anatarajia kupata nini wakimbizi wakifukuzwa. Wachangiaji wengi wanaonyesha hisia zao bila kutoa hoja ya msingi. Angalau wachache wameweza kujenga na kuonyesha nini kifanyike. Wengi, hatujionyeshe, na kwasababu hii tunatoa taarifa bila kufikiria na kukuta tunavunja heshima yetu na nchi. Nimejaribu kupitia POSTS zote zawachanjiaji, na yafuatayo yamejitokeza:
    1) Kuna mchangiaji ameandika kuwa “ …hawafai kabisa nawaomba mfatilie tabia zao….”: Kwangu binafsi, ningemuomba atoe tabia anazoona wanafanya tofauti na wa Tanzania, ili angalau tumuelewe kidogo. Sibishi kuwa hawana hizo tabia, ila Kuna wenye tabia nzuri.
    2) Mwingine, amegusia Rais kwa kusema hivi “….Rais wetu J.K. ….wewe upo karibu na watu ….saidia hao watu wanaoteseka”: Mchangiaji amegusa sehemu ya juu sana, Rais anatakiwa kama ngazi za chini zimeshindwa kuingiria kati. Mi ningeomba tupate taarifa zawachangiaji wa bunge ili tujue wanasemaje, na hatimaye tumuombe Rais aweze kutoa msimamo wake.
    3) Nanuku mchangiaji mwingine, ambaye amesema hivi”……..pengine hujui uharibifu wa mazingira walioufanya katika mikoa waliyo hifadhiwa…..”. kwa machache nikwamba watu wakiwa pamoja wakiwa wengi , mazingira anaharibika lakini hii haiweze kuwa sababu yakuwafutia ukimbizi. Mimi naona ya kuwa hisia za kupenda mazingira zimedizi za kupenda “binadamu”. Mchanjiaji atafakari hoja yake, na aone itakuwaje yeye akikutwa ameharibu mazingira arafu hati yake yakumiliki Ardhi ikafutwa.
    4) Mwingine amesema kuwa “ …..wasinga’ng’anie nchi za wenzao warudi kwao….”. Naerewa kuwa hawatakiwi kunga’ng’ania Tanzania ila hakuna aliye penda azaliwe sehemu hii au nyingine. Nafikiria kwa hili tumuache Mungu yeye muumba tusije tukaingilie majukumu yake ya uumbaji.
    5) Kuna mchangiaji amejaribu kutoa hoja zake namwisho akasema “…..ikifika usiku mnasumbua, mchana mnakuwa wa kimbizi wema….”. Nimependa hili wazo lake kwani inawezekana na uwamuzi wa kuwarudisha nikwasababu serikali ya Burundi na Tanzania wamefikiria kuwa mwisho wataunda kundi la uasi. Lakini kwa upande wangu, najua kuwa usiku na mchana wanakuwa wakimbizi. Kama usiku wanasumbua, sasa wanajeshi wanao linda kambi watakuwa wanakazi gani, kulala tuu au?
    6) Mchangiaji wa mwisho amesema hivi “……na shauri serikali isichelewe kuwaondoa hapa nchini……”. Nimejaribu kumuelewa ila nimeshindwa. Mchangiaji anafikiri kuwa wamechelewa au? Mi nadhani, haraka haina Baraka. Ukiona serikali imeamua kuendesha hilo shuguri lakuwarejesha nikwasababu inajua lolote linaweza kutokea.

    Hapo juu nimejaribu kuonyesha mawazo yawachangiaji, ila na mimi naomba nichanjie kama ifuatavyo.
    Kwa kupitia barua ya taarifa kwa vyombo vya habari, sijaona sehemu ya msimamo wa Bunge la nchi. Kama kuna nakala yoyote ya Bunge juu ya ufutaji wa ukimbizi wa warudi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...