Mwalimu wa darasa la MEMKWA katika shule ya Msingi Mlangali mjini Iringa Angelina Msolla akikagua madaftari ya wanafunzi asubuhi hii baada ya walimu 16 kati ya 21 katika shule hiyo kurejea kazini leo
Mmoja kati ya walimu wa shule ya Msingi Mlangali Iringa mjini akielekea darasani kufundisha
Mkuu wa shule ya msingi Mlangali mjini Iringa Idd Hamis Khanju akionyesha daftari la mahudhurio ambalo walimu 16 kati ya 21 wamerejea kazini leo katika shule hiyo.

Hali ya mgomo wa walimu wa walimu katika mkoa wa Iringa imeendelea kupoteza mwelekeo baada ya idadi kubwa ya walimu kuanza kurejea kazini kuanzia leo .

Uchunguzi wa mtandao  wa www.francisgodwin.blogspot.com ambao umefanya katika shule mbali mbali mjini Iringa na nje ya Manispaa ya Iringa umeshuhudia walimu hao wakiendelea na kazi kama kawaida huku wachache ndio ambao wameendelea na msimamo wao wa mgomo.

Hata hivyo idadi kubwa ya walimu wanadai wanasubiri maamuzi ya mahakama hapo kesho ndipo wataweza kutoa msimamo wao dhidi ya mgomo huo ila kwa leo wameona ni vema kuendelea na kazi kama kawaida.

Mfano katika shule ya Msingi Mlangali mjini Iringa walimu 16 kati ya 21 ndio ambao wamefika katika shule hiyo wakati shule ya Msingi Maendeleo walimu wamefika ila hawajaingia madarasani . 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Mwalimu ,mbona wanafunzi wako bado wana mabegi yao mgongoni wakati tayari wameketi darasani ?? au unataka tuzomewe ??? Zebedayo msema kweli.

    ReplyDelete
  2. Wanafunzi nao wamegoma? Idadi yao ndogo na sehemu kubwa ya darasa ipo tupu ndio kusema Iringa wamejitosheleza katika kuwa na shule nyingi kupelekea darasa moja kuwa na wanafunzi 13 tu? au mpiga picha kachukua sehemu tu?

    ReplyDelete
  3. Nyele, muache kuangusha wenzenu. Iringa walimu ndio mpo hoi. Afadhali hata hawa wa dar--lakini mnajitia kimbelele. Wenzenu wanasema pesa hakuna wakati safari za ulaya kila siku, wanafanya kazi kwenye viyoyozi---magari yakifahali---na nyinyi mnakubali. Daini chenu bila fujo.

    ReplyDelete
  4. Zebedayo uliza yenye msingi.

    ReplyDelete
  5. Unkala tunafahamu upo upande wa watawala lakini chonde chonde usichakachue madai wa walalahoi (walimu).Hali ya mgomo nyanda za juu kusini (iringa, mbeya na songea) NI MBAYA SANA. Kwa kuposti hii kitu unaonyesha uwajali watoto wa wanzania walio wengi wanasoma shule hizo. ukichukulia watoto wako wanasoma shule bora kabisa zinaanzia na neno" international na saint".

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...