Mkuu wa wilaya ya Hai ,Mh.Norvatus Makunga akipokea mwenge wa uhuru kutoka   katika halimashauri ya wialya ya moshi mjini.Picha na woinde shizza,Hai
==============  =============  ========
 Na Woinde Shizza,
Kilimanjaro
Zaidi ya miradi 51 ya maendeleo ya wananchi itazinduliwa na kuwekwa mawe  ya msingi na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa mwaka huu, kepteni Ernest Mwanosa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 4  mkoani Kilimanjaro.

Akikabidhiwa mwenge wa uhuru  ukitokea mkoa wa Manyara mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama, alisema kuwa mwenge  huo utazindua miradi yote iliyopo  kwenye halimashauri  saba za mkoa.

Gama alieleza kuwa miradi hiyo imegusa sekta zote muhimu ambazo ni miradi ya Afya, maji, kilimo  mifugo na ushirika, miundombinu hifadhi ya mazingira, biashara na ujasiria mali.

Alisema alisema miradi mingine ni Elimu na utawala na miradi mingineyo, na kueleza kuwa mbio za mwenge zitaimarisha  na kuibua upya ari ya kupambana na madawa ya kulevya, rushwa naelimu juu ya umuhimu wa sensa ya watu na makazi.

Gama alisema kuwa mkoa wa Klimanjaro unakabiliwa na changamoto kubwa ya usambazaji na matumizi makubwa ya madawa ya kulevya kutokana na mkoa kupakana na  nchi jirani ya Kenya pamoja na kuwepo kwa uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Kia.

Alisema kutokana na kuwapo kwa changamoto hiyo, serikali kupitia jeshi la polisi limekuwa mstari wa mbele katika mambano dhidi ya matumizi ya madawa ya kulevya, ambapo jumla ya watu 1,243 wamekamatwa kuhusika na matumizi na usambazaji wa dawa hizo.

Kwa upande wake kiongozi wa mwenge kitaifa, Ernest Mwanosa, aliwataka wananchi kutoa ushirikiano katika kushiriki kwenye zoezi la sensa ya watu na makazi litakaloanza Agost 26 mwaka huu, kwa lengo la kuipa serikali uraisi wa kuleta maendeleo wa urahisi.

Mwanosa aliwataka wananchi kutambua kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi ni muhimu kwa kila mtanzania, kwa serikali kupata takwimu za watu itarahisisha zaidi kubainika kwa mahitaji ya maendeleo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...