Zaidi ya tani tatu na nusu ya madawa ya kulevya aina ya bangi yameteketezwa na jeshi la polisi mkoani Arusha katika kukamilisha operesheni ya kupambana na uhalifu na madawa ya kulevya inayoendelea mkoani hapa kwa mujibu wa mrakibu wa polisi na kaimu kamanda wa jeshi hilo mkoani hapa Zuberi Mombeji alisema kuwa zoezi hilo ni endelevu na kuwataka wananchi mkoani hapa kutoa ushirikiano katika kutokomeza vitendo vya kihalifu.
Baadhi ya maofisa wa polisi akiwemo msemaji wa jeshi hilo mkoani hapa Rashid Nchimbi wakiangalia zoezi hilo likiendelea kwenye sehemu wanaochomea madawa hayo eneo la FFU nje kidogo ya jiji la Arusha.Picha na Mahmoud Ahmad,Arusha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Unajua kama wateketeza bangi high class kwa moto, all you have to do is park yourself down wind and you will get high.

    ReplyDelete
  2. Balaa nyingi nyingine zinaleta maafa makubwa kwa afya ya binAdam kuliko hiyo bangi.Kwa mfano beer,pia unajuwa kuwa sigara around the world kill more people than hizo bangi, lakini serikali hazithubutu to ban cigarettes because of its being a major source of revenue.

    ReplyDelete
  3. Sasa mmezuia wavuta bangi kufaidi bangi zao mmeamua kuvutisha bangi mji mzima wa Arusha...wapi na wapi? Mdau, CA-USA

    ReplyDelete
  4. Yaani Arifu wanachomaje asee hawa jamaa niaje niaje ati?

    ReplyDelete
  5. Huu ni ulimbukeni ukichanganya na umbulura bangi imetoa watu wengi ukiangalia kina obama, lil wayne, 50 centand manya more mbona hata jamaica wameruhusu na pia bangi inaleta appetite ya kula na mtu unakua na afya njema na akili sawia arrrifu...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...