Mashabiki wa soka wakifuatilia mtanange wa fainali ya Mashindano ya Ujirani mwema Cup yaliyodhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF) katika uwanja wa Ilulu katika manispaa ya  Lindi leo
 Hatari golini wakati wa mchezo huo
 Mgeni rasmi Bi Fatuma Mikidadi,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi akiwa meza kuu na kombe. Chini akikabidhi kombe hilo kwa washindi Afrika Gereji

Picha na habari na Abdulaziz Video, Lindi
Mashindano ya Ujirani mwema Cup yaliyodhamini wa Mfuko wa Hifadhi wa Mashirika ya Umma (PPF) yamemalizika katika Manispaa ya Lindi huku Timu ya Afrika Garaje ikiibuka kidedea baada ya kuifunga Timu ya Kusini Soccer Academy kwa Jumla ya Mabao 2 KWA 1 na kufanikiwa kutwaa kikombe pamoja na Seti ya Jezi.

 Mashindano hayo yaliyoshirikisha jumla ya Timu 8 za Manispaa ya Lindi na kuhudhuriwa na wadau wengi wa michezo na walioshuhudia Timu ya Afrika Gereji ikiliandama lango la Wapinzani wake karibu dakika zote za
mchezo huo.


Alikuwa ni Salum Abilahi wa Afrika Gereji alieamsha ari ya ushindi huo baada ya kuunganisha krosi safi iliyopigwa na Anafi Jamvi na kuunganishwa vizuri na mfungaji huyo katika dakika ya 38 ya kipindi cha kwanza. Hadi Mapumziko Bao ni 1 kwa Bila….Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo  timu ya Kusini soccer ilisawazisha bao hilo katika dakika 8 kwa njia ya Penalti baada ya Mshambuliaji wa Timu hiyo kuchezewa vibaya alipowatoka walinzi wa Afrika Gereji. Goli  ambalo halikudumu baada ya Anafi Selemani Jamvi kuipatia timu yake bao la ushindi alilofunga kwa shuti kali lililoenda nyavuni moja kwa moja.
Akiongea na Globu ya Jamii  kuhusiana na Mashindano hayo Meneja wa PPF kanda ya kusini-Mtwara na Lindi, Bw. Anthony Ndadavala  Alieleza dhumuni la shirika lake kudhamini Michezo ni pamoja na kujulisha jamii kuhusiana na mfuko huo ikiwemo kufunguliwa rasmi kwa ofisi ya Kanda hiyo mkoani Mtwara.  
Naye  Mgeni rasmi Bi Fatuma Mikidadi,Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Lindi akiongea kabla ya kufunga mashindano hayo na  Kukabidhi zawadi kwa washindi alitoa wito kwa Wanasiasa pamoja na wanajamii kujitoa kusaidia Michezo katika Mkoa wa Lindi Mkoa ambao kwenye miaka ya Nyuma ulikuwa inatoa sana kila aina ya  wanamichezo bora hapa nchini, tofauti na ilivyo leo.
Licha ya Timu hiyo ya Afrika Gereji  kutwaa kikombe pia ilipata zawadi nyingine ya seti ya  jezi  huku washindi wa pili,tatu na Nne kila moja ikijipatia seti Moja ya JEZI Huku waamuzi nao wakiambulia Tshirt na Fedha Taslimu zilizotolewa na Mfuko huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. BWAWA VIPI TUMESHINDWA KUTIZAMA MECHI KWA JIRANI HAJAWASHA TV WANAUGOMVI NA MKEWE TUPE MATOKEO MITHUPU!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...