Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Akofu Dk Alex Malasusa ameongoza maelfu ya waumini wa kanisa hilo katika ibada ya kilele cha maadhimisho ya miaka 125 tangu kuingia kwa injili katika dayosisi ya Mashariki na Pwani.
Maadhimnisho hayo yameambata na uzinduzi wa mnara wa kumbukumbu ya jubilei, uzinduzi wa ujenzi wa uzio wa seminari ya Kisarawe pamoja na kuwekwa wakfu na ubarikio wa watheolojia kumi na wanne kuwa wachungaji, ambao wamekiri na kuweka nadhiri zao mbele ya mUngu kufanya kazi yao kwa uaminifu na uadilifu mkubwa.
Ibada hiyo iliyofanyika katika seminary ya Kisarawe mkoani Pwani na kuhudhuriwa na maaskofu kutoka Sweden, Ujerumani, Marekani, viongozi wa serikali na wageni mbalimbali ilitanguliwa na maandamano kutoka kanisa la usharika wa Sanze hadi kenye eneo la seminari.
 Askofu Mstaafu wa kwanza wa KKKT-Dayosisi ya Mashariki na Pwani ambaye pia ndiye alikuwa Mkuu wa kwanza Mwafrika wa Sinodi ya Uzaramo na Uluguru akikata utepe kama ishara ya kuzinduliwa rasmi ujenzi wa ukata/ Uzio wa shule ya Seseminari ya Kisarawe mkoani Pwani leo.

  Wachungani wapya kabla ya kubarikiwa wakiwa katika maandamano wa kati wa ibada ya kilele cha maadhimisho ya jubilee ya mika 125 ya injiili DMP
 Baadhi ya wachungaji wakiwa kwenye maandamano ya ibada ya mika 125 tangu kuja kwa injili Pwani ya Mashariki.
 Mke wa Mkuu wa KKKT-DM Askofu Dk. Alex Malasusa, Mama Rebeka Malasusa (kulia) akiimba wakati wa ibada ya kilele cha Jubilee ya miaka 125 ya injili kushoto ni Mke wa Askofu mstaafu wa DMP Dk. Mama Elinaza Sendoro 

Wachungaji wapya (waliovalia majoho meupe) kabla ya kubarikiwa  wakiwa kwenye ibada ya kilele cha miaka 125 tangu kuingia kwa injili Pwani. 

 Kwaya ya Kinamama wa wa DMp wakiimba kwa umoja wao wakati wa ibada ya kilele cha Jubilee ya miaka 125 ya injili DMP
Askofu Mstaafu wa DMP ambye pia alikuwa mkuu wa Sinodi ya Uzaramo na Uluguru Elinaza Sendoro akitoa salamu zake za Jubilee ya 125 tangu kuingia kwa injili DMP

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...