Mahmoud Ahmad Arusha
CHAMA Cha Watu wananchi CUF kimetoa tamko kali kwa kuwatuhumu wafuasi sita wa Chadema jijini Arusha kwamba walihusika na vurugu za kulishambulia gari la matangazo na kisha kumpiga mawe mfuasi wao huku wakilitaka jeshi la polisi kuchukua hatua kali za kisheria.
Taswira ya mambo yalivyokuwa wakati wamachinga wa jijini Arusha walivyopora kiwanja na kuanza kujipimia ili kufanyia biashara kabla ya polisi kuinguilia kati
Akitoa tamko hilo leo katika ofisi za chama hicho zilizopo kata ya Kaloleni jijini Arusha,mjumbe wa baraza kuu la uongozi taifa wa CUF, Mbarala Maharagande, alisema kwamba chama chao kina ushahidi wa kutosha kwamba mfuasi wao, Athuman Abdulraham, alipigwa mawe na wafuasi wa Chadema wakati akiwa katika gari la matangazo.
Maharagande,alisema kwamba mfuasi wao alikuwa katika eneo la Levolosi karibu na eneo lililovamiwa na wamachinga na wakati akiwa ndani ya gari hilo wafuasi wa Chadema walianza kumyooshea alama ya vidole viwili kabla ya kuanza kumpopoa kwa mawe.
Hatahivyo,alisisitiza kwamba tayari mfuasi huyo ameshatoa tarifa kwa jeshi la spolisi mkoani hapa na kufungua faili nambari AR/RB/12419/012 na kulitaka jeshi hilo kuwakamata wafuasi hao wa Chadema hadi kufikia septamba 30 mwaka huu na wakishindwa wao watachukua hatua za kisheria wanazozijua.
“Kijana amepigwa na wafuasi wa Chadema na tayari tunawajua wako sita tumeshatoa tarifa polisi wawachukulie hatua na kama wakishindwa basi sisi tutachukua hatua za kisheria tunazozijua”alisema Maharagande
Alisema kwamba wana tarifa za kutosha kwamba Chadema wamefanya vurugu za kutaka kuharibu mkutano wa hadhara wa chama chao unaotaraji kuhudhuriwa na mwenyekiti wake,Prof Ibrahim Lipumba sanjari na makamu mwa kwanza wa Rais Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad .
Alisema kwamba wao wamekuja Arusha kufanya kazi za siasa zikiwa ni pamoja na kujiandaa na uchaguzi wa madiwani,ubunge pamoja na kueneza será ya V4C iliyoasisiwa hivi karibuni.
Hatahivyo,alisisitiza kwamba wao hawapendi kupambana na Chadema kwa kuwa hawana serikali huku akisisitiza kuwa kama ni fujo wanazijua lakini kwa sasa wanaeneza será na kama Chadema wakitaka kupambana nao wakashindane kwa hoja majukwaani.
mbona habari haziendani na picha?
ReplyDeleteHii ni dili ya KUWACHONGANISHA jamaa wa CUF NA CHADEMA..
ReplyDeleteSiasa za Maji Taka!!
chadema wamekwisha iharibu arusha....
ReplyDeletekwa hiyo mtu akinyanyua vidole viwili juu ni CHADEMA? ujinga hauna umri!!
ReplyDeleteCHADEMA-Arusha,
ReplyDeleteAcheni ujinga wenu fanyeni Siasa zenye tija na ustaarabu!
Mtakamatwa mtafungwa na kukaa Gerezani hadi 2015 kabla ya Uchaguzi ujao ndio mtoke kupiga Kura.
Ohooo, mkileta mchezo mtamezwa na MAMBA!
Tusije kulaumiana bureee?
ReplyDeleteMwanawane CHADEMA huko Arusha inafahamika hadi nje ya nchi ni ukanda wa Utalii, isipokuwa msifikiri ndio mpo MSITUNI kabisa kabisa, mkumbuke ya kuwa fanyeni ujinga wenu lakini zipo kazini Idara za Usalama na POLISI !!!
VURUGU ZA CHADEMA ZA MARA KWA MARA:
ReplyDeleteNashauri Msajili wa Vyama vya Siasa nchini asiwe anatoa Usajili wa vyama pekee bali pia atoe sheria ya kila Chama cha Siasa kiwe,
1.Kinaendesha Kozi za Makada wa Chama.
2.Kinaendesha Kozi za muamko wa Kisiasa kwa Wanachama wake,
3.Kinatoa Mafunzo ya jinsi ya kuendesha harakati za Ki-Siasa kwa njia za kistaarabu na kisasa.
4.Kinatoa mafunzo ya kuwajenga Wanachama wake ya kuwa Upinzani wa Kisiasa na uvunjaji wa Sheria ni vitu viwili tofauti.
5.Chama kiwaelimishe wanachama wake kuwa ikitokea mtu akafanya harakati za Kisiasa hadi akavunja sheria ajitambue kuwa ameingia katika hatia na atachukuliwa hatua za Kisheria kwa Makosa ya Jinai.
BILA YA HAYO MATANO KWELI MAISHA YATAWEZEKANA?
NADHANI TUTAKUWA KAMA TUPO SOMALIA!
Chadema-Arusha,
ReplyDeleteAcheni kutuaibisha kwa ndugu zetu majirani ktk Afrika ya Mashariki, kutokana na fujo zenu za uendeshaji wa Harakati za Siasa kishamba ndani ya Jiji hilo.
Ni heshima kubwa sana tumepewa Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kuwa hapo Jijini Arusha!
Chadema muache kuihujumu Arusha kiuchumi kutokana na fujo zenu za kipumbavu kabisa!
ReplyDelete