Umati wa watu wakiwa wanaandamana kuvunja uzio na kuweka soko mikononi mwao

Hapa Wakati wanachoma Mbao pamoja na Mataili wananchi wengine wanabomoa bomoa uzio

Na Woinde Shizza,
Wafanyabiashara ndogo ndogo maarufu kama wamachinga jijini
Arusha leo wamezua tafrani kubwa baada ya kuvamia eneo
la kiwanja cha Ermoil lililopo mkabala na soko la Kilombero na kuanza kugawana maeneo ya kufanyia biashara
kwa kujipimia.
Katika vurugu hizo mfuasi mmoja wa chama cha Wananchi CUF, Athuman
Abrahaman, alishambuliwa kwa mawe na kisha kujeruhiwa eneo la usoni na watu
wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa Chadema huku gari la matangazo la Cuf nalo likijikuta likipopolewa kwa
mawe na spika zake
kuharibika vibaya.
Askari wa jiji la Arusha
walionekana majira ya saa 3;30 asubuhi akipita na gari lao katika maeneo
mbalimbali ya jiji hapa huku wakiwatangazia wamachinga wote kuondoka katika
maeneo ambayo hayajatengwa kufanyia biashara zao.
Askari hao walikuwa
wakiwatangazia wamachinga hao kuondoka katika maeneo ambayo hayajatengwa
kufanyia biashara huku wakitamka ya kwamba endapo wakikahidi watachukua bidhaa
zao kwa nguvu na kuwachukulia hatua za kisheria.
Baadaye askari hao walianza kutekeleza majukumu yao ya
kusomba bidhaa hizo na kisha kuzipakia ndani ya gari lao wakivipeleka katika
ofisi za manispaa ya Arusha. Hatua hiyo iliwapelekea wamachinga hao kujikusanya
kwa pamoja na kisha kuvamia ghafla eneo la wazi wa Ermoil kwa kuvunja uzio wa
mabati uliokuwepo na kisha kuanza kujigawiana maeneo kwa kuyapima kwa kamba.
Wamachinga hao zaidi ya 200
walivamia huku wengine wakitumia nafasi hiyo kupora mali mbalimbali zilizopo
ndani ya eneo hilo kama mabati,nondo na saruji zilizokuwa ni mali za mtu anayedaiwa
kumiliki eneo hilo.
Katika heka heka za kugawana
viwanja ndani ya eneo hilo wamchinga hao walikata miti iliyokuwemo ndani na
kisha kuanza kuichoma kwa moto hali ambayo ilisababisha wingu zito la moshi
kutanda hewani.
Wakati tafrani hiyo ikiendelea polisi waliokuwa
wamesheheni kwenye magari yao walikuwa wakipita mara kwa mara kuzunguka eneo
hilo lakini hawakuonekana wakifanya udhibiti wowote zaidi ya kuwaangalia
wamachinga hao.
Mkuu wa wilaya ya Arusha,John
Mongella alilaani tukio hilo na kusema kwamba wamachinga hao wamevamia eneo
hilo kimakosa kwa kuwa si la kwao huku akikitupia lawama chama kimoja cha siasa
hapa nchini kwamba kimehusika katika kuhamasisha vurugu hizo.
Alisema kwamba kwa sasa
watakutana kujadili tukio hilo kwa undani kwa kuwa wana ugeni mkubwa lakini
alisema kwamba kitendo cha wafuasi wa Chadema kupiga mawe gari la Cuf na mfuasi
wake si cha kiungwana.
Kaimu mkurugenzi wa halmashauri
ya manispaa ya jiji la Arusha,Omary Mkombole alisema kwamba kitendo cha
wamachinga hao kuvamia eneo hilo ni kuvunja sheria na wataondolewa hapo hivi
karibuni.
Mkombole,mbali na kulaani tukio
hilo alisema kwamba uongozi wa jiji umepanga maeneo mbalimbali ya kufanyia
biashara na eneo hilo ni mali ya mtu binafsi ambapo alikuwa ameanza jitihada za
kuliendelez
CHADEMA acheni uhuni,kupiga wafuasi wa cuf na kuiba mali za watu ni uhuni usiovumilika.jamani hiki chama kinaipeleka tanzania kubaya,hawajui kitu zaidi ya maandamano fujo na kuiba.
ReplyDeleteNdio mkome kuwatimua machinga na kupora biashara zao badala ya kuwapitia maeneo ya kufanyia kazi zao., wananchi wamechoshwa na manyanyaso ya polisi na mgambo wa jiji
ReplyDeletearusha hali ni mbaya tangia aikamate lema watu hawataki kutii sheria
ReplyDeletejamaniii sio kila kifanyikachoo ni chadema tu kwa hiyo wamachinga wote 200 ni chadema sijui kwa nn chadema inasingiziwa kila kituuu sidhani kama ni wao
ReplyDeletePeople's POWER! Mnafurahiaaa............
ReplyDelete