Ankal za miaka!
Hongera kwa kazi nzuri.
 Nina Kero moja kubwa sana naomba uniwekee kwenye Blog Yako.
Barabara ya Old Moshi Road ( Kuanzia Mushono kuelekea Mandela Institute of Technology) ina hali mbaya sana kutokana na magari makubwa( kwa siku yanapita zaidi ya trip mia moja ) yabebayo kifusi kwa ajili ya utengenezaji wa barabara za Arusha Mjini zimeiharibu sana sana. Ni miezi mingi sana sasa imepita tangu tuambiwe wanaweka LAMI …..tukahamisha mipaka waliokumbwa na bomoa bomoa ikawapitia lakini hakuna kinachoendelea. Kama miezi 9 sasa imepita wameshaifanyia grading mara tatu lakini sasa hivi hali mbaya, Kuna hilo eneo la Jeshini hali mbaya sana na ajali si rahisi kuzuilika.
Tumetangaziwa el nino sasa sijui itakuwaje.

TAFADHALI WAHUSIKA SERIKALINI NA TANROADS tafuteni suluhu ya hili, kwani hii ni barabara muhimu sana...na mashamba mengi ya maua na mboga mboga, chuo cha Nelson Mandela N.K, ni fupi kwa wale wanaoitumia kwenda USARIVER wakitokea Arusha Mjini.

Samahani hizo picha si nzuri sana kwani imebidi nizipigie ndani ya gari kwani hilo vumbi sijui jinsi ya kulieleze. Kwa kweli watembea kwa miguu na wenye nyumba pembeni ya barabara wanataabika sana.

Mtumiaji wa kila siku wa Barabara hiyo.

Barbara

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mshukuru Mungu angalau ninyi mna barabara...huko kwetu hakufikiki...!!

    ReplyDelete
  2. Yeuuuuuii! Wa-old moshi si tuchange tutengeneza bara bara kuliko kusubiri kila kitu tufanyiwe na serikali??? Hii ni hatari

    ReplyDelete
  3. mdau hii ni barabara ya kutoka Kijenge arusha kupitia Chuo kikuu cha Nelson Mandela hadi Usa river inaitwa old moshi road au barabara ya zamani ya arusha-moshi na wala si ya kwenda oldmoshi mwanangu!Mbaya kuchangamkia deal usilolifahamu

    ReplyDelete
  4. Hii barabara si ndiyo ipo kwenye mradi wa East Africa wa kutengeneza super high way ya kwenda Arusha au?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...