Bima inayofuata sheria za kiIslam inayojulikana kama (Takaful) imekua mshindi ktk mkutano wa tatu unaofanyika kila mwaka nchini Kenya na ambao umefanyika kwa mara ya tatu mwaka huu. 
Wakati wanatoa zawadi hiyo waamuzi wa kikao hicho ilibainika kwamba ilikua ni mara ya kwanza ambapo zawadi hiyo imekwenda kwa shirika jipya, shirika ambalo limeanza kazi zake mwezi wa tatu mwaka huu 2012. 
Ni muhimu kukumbushana kwamba  hilo ni shirika la kwanza  ambalo linafanya kazi zake kwa kufuata sheria za kiislam. 
Walisikika wakisema wamiliki wa shirika hilo ‘Tumefurahi na tunahisi faraja kupata zawadi hii. Tukio hili linazungumza kwa sauti ya juu kwamba kazi zetu zimehishimiwa na mashirika mengine ya bima alisema CEO Hassan Bashir’. 
Kupata zawadi kama hii ni ushahidi wa wazi kwamba masharti muhimu kama vile uwazi, heshima, kukubali majukumu ni muhimu ktk biashara ya bima. Mkutano huo wa mwaka unaandaliwa na business intelligence na publishing house Think Business Limited.
Fikra ya bima inayofuata sheria za kiIslam ni kushirikiana na kusaidiana na kudhaminiana. Pamoja na mambo mengine bima ya kiIslam inakataza aina zote za mambo ambayo yatakua na uhusiano na riba, kamari na hadaa.

Kwa maelezo zaidi ni tofauti gani zilizopo kati ya bima inayofuata 
sheria za kiIslam na ile isiyofuata sheria za kiIslam wasiliana na 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Ni habari njema, ninavyofahamu kama sikosei hadi leo hatuna bima inayofuata sheria za kiislam nchini Tanzania, kwanini matajiri wasomi, wasifikirie kuleta huduma hii nchini wakishirikiana na wataalam wa uchumi wa kislam? Hususan ukizingatia kwamba huduma hiyo anaweza kuitumia yoyote hata asiyekua muislam.

    ReplyDelete
  2. wadau watuletee hivyo vitu jamani.
    congrats kenyans mko mbali

    ReplyDelete
  3. Ndugu zangu wa tz, tupo ktk mchakato wa kuanzisha takaful tz tumefanikiwa bank sasa tunaenda takaful lkn tuliambiwa tusubiri nic wamalize research watu waende kusoma km kawaida nchi yetu watu watengeneze safari nje walipane mapesa. Maana wakati tunataka kuanzisha islamic bank bot waakwakapeleka watu nje kusoma ghasia kibao lkn dondoo zinasemekana wapo sawa nic tusubiri inshallah

    ReplyDelete
  4. Naam Mdau wa Sun Sep 02, 05:10:00 PM 2012

    Tanzania mtihani mkubwa tilio nao ni vitu vya kufikia malengo kwa njia za mkato.

    Kama tunavyoona uanzishaji wa Benki za Kiislamu watu wanapata njia ya kubuni safari za nje ili kupata mafao.

    Angalieni, 'inflation changes' yaani mabadiliko ya mfumuko wa bei ktk nchi 3 za Afrika ya Mashariki:

    KENYA:
    Jan-2102 ilikuwa 18.1%
    August-2012 ikawa 6.09%

    UGANDA:
    Jan-2012 ilikuwa 23.5%
    August-2012 imekuwa 11.17%

    TANZANIA:
    Jan-2012 ilikuwa 19%
    August-2012 imekuwa 15.1%

    SASA KAMA KENYA NA UGANDA ZINA NJAA YA CHAKULA NA UPUNGUFU WA CHAKULA KULIKO TANZANIA, KWA NINI MFUMUKO WA BEI UWEPO TANZANIA HUKU NCHI HIZO ZENYE NAFASI NGUMU KUPUNGUZA MFUMUKO?

    JIBU NI KUWA

    1.MFUMUKO WA BEI UNACHOCHOWE ZAIDI TANZANIA NA KUTUMIA ZAIDI UCHUMI WA KODI YA MAFUTA (MAPATO KUPITIA KODI YA MAFUTA) MABAYO INACHOCHEA MFUMUKO WA BEI NA KUPANDA KWA GHARAMA ZA MAISHA.

    2.DHAMANA ZA MADENI YA SERIKALI YAANI (T-BILLS NA T-BONDS)INATAKIWA ZINADIWE NA KUTOLEWA FURSA HADI WATU BINAFSI MCHINI KUFANYA UWEKEZAJI NA KUONGEZA MZUNGUKO WAKE NA KUSHUSHA MFUMUKO WA BEI BADALA YA KAUCHIA TAASISI ZA KIFEDHA PEKEE KUWEKEZA.

    KENYA NA UGANDA WAMEZA WANA NINI , IWE SISI TUSHINDWE TUNA NINI JAMANI WEE?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...