Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa CPA Africa akitambulisha ujumbe wa Tanzania (hawapo pichani) na baadhi ya Maafisa waliohuduria mkutano huo mjini Colombo Sri Lanka. Ujumbe wa Tanzania unaongozwa na Mhe. Anne Makinda, Spika wa Bunge, Mhe. Zitto Kabwe, Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mhe. Hamad Rashid Mohamed, na Mhe. Muhonga said Ruhwanya. Waliosima wa Kwanza kulia ni Ndg. Said Yakubu, Afisa Dawati wa CPA Tawi la Tanzania na Kaimu Katibu wa CPA kanda ya Afrika Ndg. Demitrius Mgalami.

Chama cha Mabunge wanachama wa Jumuiya ya Madola kanda ya Afrika, (CPA Africa Region) wamekutana kujadili mipango mbalimbali ya umoja wao katika Mkutano wa 58 wa CPA Dunia unaoendelea Mjini Colombo Sri Lanka. Pamoja na Mambo mengine, Kanda hiyo ya Afrika imejadili namna ya kuimarisha chama hicho, pamoja na maswala mbalimbali ya kiutendaji ndani ya Chama hicho ikiwa ni pamoja na msimamo wa Afrika katika maswala kadhaa ndani ya chama hicho duniani.
Wajumbe wa CPA kanda ya Afrika wakiwa katika kikao hicho Mjini Colombo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...