MIAMBA ya masumbwi nchini, bingwa wa Mabara Francis Cheka [SMG] na aliyekuwa bingwa wa Dunia Karama Nyilawila [Kapten] wanatarajia kupanda ulingoni kesho Jumamosi kuoneshana umwamba. Promota wa pambano hilo Oswald Mlay alisema pambano hilo litapigwa katika uwanja wa PTA Sabasaba Barabara ya Kilwa road jijini Dar es salaam.
Cheka na Nyilawila walitwangana mbambanmo wao uliofanyika Morogoro ata hivyo ulizua utata baada ya mpambano wao kugubikwa na alama za mshangao ambalo cheka aliibuka na ushindi wa point mashabiki kuhisika wa mabondia hao wanaogopana na kutafutana kwa mda mrefu watapoza kiu yao kwa mpambano huo jumamosi ya kesho.
Alisema pambano hilo litakuwa la raundi 12 uzito wa kg 72 ambapo leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano uho utakaoamua nani zaidi
Katika Mchezo huo kutakua na uuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Karama Nyilawila akipima uzito leo jijini Dar es salaam
Bingwa wa Mabara Francis Cheka akipima uzito leo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...