Hapa iliku bado restaurant inatengenezwa
Mpangilio wa sauce na salad na nyama za tayari kwa kuchoma
Tunachoma samaki maarufu sana aina ya changu mwekundu na mweupe huwezi amini dakika saba tu chakula kipo mezani na ameivaa swaaaaaafi
Huu ni muonekano wakati wa usiku
VIDEO HII NIMETUMIWA NA JAMAA MMOJA ALIETEMBELEA RESTAURANT NA KUFURAHIA SANA BBQ
JE WADAU MNADHANI RESTAURANT HII IPO MJI NA MAENEO GANI? MSHINDI WA KWANZA BBQ BUREEEEE!!!!
WASALAAM CHEF ISSA


Hakuna changu mwekundu. Kuna changu ana changudoa!!
ReplyDeleteWewe njoo Dar watu tupate msosi achana na mambo ya kutuchemsha bongo wakati mate yashajaa mdomoni.
ReplyDelete
ReplyDeleteSio kichangachui hapo?
Hiyo Restaurent iko, Dar maaneo ya Tegeta Masaiti, iko kama 500m kutoka Bahari Zoo au kama unapita njia ya kwenda Ununio kuna kijiji flani kushoto unaingia then unapita makaburi ya Kunduchi na 500m mbele utaikuta mkono wa kulia.
ReplyDeleteBy Chimbyo!
We tuambie tu iko wapi tukuletee biashara wacha kutukoroga na maswali biashara haitangazwi hivyo
ReplyDelete
ReplyDeleteAsante chimbyo.
Changu mwekundu ni Red snapper au fatundu
KUNA RESTAURANT NYINGI TU NZURI NA SAFI DAR. HAYO MA SAUCE SALADS UNAPATA POPOTE TU KUBWA NI JE ZIPO SALAMA?SIJAONA WALA KUSKIA JIPYA KWEMYE HILI TANGAZO. TABASCO ZIMEJAA MADUKANI, HAKUNA JIPYA. THE BEST CHEF IS ONE'S MOTHER.
ReplyDeleteMdau wa Fri Sep 28, 10:11:00 PM 2012
ReplyDeleteKila fani ina mwenyewe utake usitake!
Hapa Chef. Issa anazingatia zaidi Professionally.
WINGI NA UTITIRI WA RESTAURANTS NYINGI ZA JIJINI DAR HAUZINGATII VIWANGO VYA CHAKULA NA KANUNI!
UPUNGUFU:
1-LICHA YA KUWA NA VYANZO VYA VYAKULA HALISI KUTOKA MASHAMBANI, RESTAURANTS NYINGI ZA DAR HAZIANDAI CHAKULA KWA VIWANGO VYA KIMATAIFA KAMA ANAVYOFANYA KAZI ZAKE MTAALAMU CHEF ISSA.
2-UZURI WA MUONEKANO WA CHAKULA KWA RANGI YA BINZARI NA ROJO ROJO SIO KIGEZO CHA UBORA WA CHAKULA...KAA WANAVYOFANYA WAADNAAJI WENGI WA MADISHI DAR.
3-VYAKULA VINGI HAVIANDALIWI KWA KANUNI ZINAZOKUBALIKA (IN HYGIENIC ORDER), UNAKUTA CHAKULA KINAPIKWA ASUBUHI HUKO MBAGALA RANGI 3 AU GONGO LA MBOTO KINASAFIRISHWA KATIKA NDOO ZA PLASTIKI NA KULIWA KATI KATI YA JIJI LA DAR.
4-NI VIGUMU KUMKUTA MZUNGU MTALII LABDA AWE ANAJIAMINI SANA AKALA KATIKA RESTAURANT ZA KAWAIDA ZA JIJINI DAR, UNAWEZA MUONA MZUNGU ANAKUWA TAYARI AINGIE GHARAMA ZA JUU KWA KULA HYATT REGENCY KILIMANJARO HOTEL KWENYE VIWANGO NA KANUNI HATA KAMA ATAKUWA AMEFIKIA NA ANALALA ECONO LODGE (Hoteli ya malazi ya bei za chini)YA UHINDINI KISUTU DAR.
5-NI MUHIMU TUZINGATIE VIWANGO ,KANUNI NA TARATIBU ZA KUANDAA VYAKULA KIMATAIFA ILI KUTOA NAFASI YA KUWEZA KUKUBALIKA NA WALAJI WA KIMATAIFA...MFANO KISIWANI HUKO MAURITIUS INAZINGATIA VIWANGO WAMEFANIKIWA SANA (WAMETUMIA MIPANGO YA WORLD BANK NA UNITED NATIONS KUFIKIA LENGO) KULE WANAKULA HADI MAGENGENI AMBAKO WANAKUTA VYAKULA VINAANDALIWA KWA MASHARITI YANAYOTIMIZA VIWANGO VYA KIMATAIFA...HIKI NDIO KITU ANACHOTOA PROFESSIONAL CHEF. ISSA HAPA ZAIDI YA UTAMU WA CHAKULA KINACHOANDALIWA.
Wewe Mdau wa 7 hapo juu,
ReplyDeleteKwa kuzingatia viwango vya madishi na kanuni za Kimataifa kama anavyotushushia Professionali Chef. issa Restaurant nyingi Bongo Darisalama zinatulisha 'michanyato' na siyo Madishi kamili!
Nyingi zinapika nje na chini ya viwango!,,,sio rahisi ukamkuta mgeni Mtalii anakula Gengeni Bongo labda awe anajiamini sana ama yupo katika Utafiti (Research)!!!!!
Wabongo wana roho mbaya! Kama huyo anon wa 7, 11:00, kama mkaanga sumu vile! Loh!
ReplyDeleteHiyo sehemu kwa muonekano wa usiku na taa zake?, pamenoga sana panafaa kukaa Fungate na mwenza baada ya Ndoa!
ReplyDeleteMdau wa 7 hapo juu,
ReplyDeleteWewe huna ujuzi katika sanaa ya Mapishi na pia bado unao umande miguuni kuhusiana na ulaji wa vyakula Kimataifa.
Huyo Jamaa Chef. Issa ni mtu wa Taaluma ya lishe yaani PROFESSIONAL CULINARY ARTSIST tena kwa kusomea huko Canada!
Hebu angalia mpangilio wa vitu hapo na aina za vitu vilivyo andaliwa kwa kutengenezea chakula, unaweza kuukuta kwa mama ntilie tena yule anaeandaa chakula unachokula wewe Mchana ukiwa Kariakoo Sokoni kwenye kibarua chako wakati Mama ntilie anakaa Mbagala Rangi 3 anakoandalia DISHI HILO BOVU ASUBIHI ANAJAZA KTK NDOO ZA PLASTIKI ANAPANDA DALADALA ANALETA KARIAKOO MCHANA, DISHI UNALOKULA WEWE MCHANA UKIWA KARIAKOO wakati wewe unakaa Mburahati na kibarua chako unafanyia Kariakoo Sokoni ?
NI JANGA LA KITAIFA NA BALAA KUBWA KWA VILE WABONGO WENGI KAMA WEWE HAWAJUI KUTHAMINISHA UBORA WA VITU, HASA KIGTU KAMA CHAKULA!
MTU ANAFIKIRI UBORA WA CHAKULA NI KUWA NA ROJOROJO NA MAFUTA KIBAOOO!
NAWASHUKURU SANA WACHANGIAJI WOTE YOTE NI YA MSINGI NA NI CHANGAMOTO KWA WALAJI KUTAMBUA NINI CHAKULA BORA NA SALAMA. NITAJITAIDI SANA KUENDELEA KUTOA ELIMU KWA MASWALA YA CHAKULA
ReplyDeleteCHEF ISSA
Maisha club Mtwara
ReplyDelete