Mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa viti Maalum Mkoa wa Tanga Amina Mwidau (CUF), akikabidhi zawadi ya kikombe cha ushindi kwa Nahodha wa timu ya Chuda FC Ibrahimu Bodwe, baada ya timu yake kuibuka kidedea katika michuano ya Haniu Cup, katikati ni Mratibu wa Mashindano hayo Mohammed Haniu.
Mgeni rasmi katika mashindano ya kuwania kombe Haniu Cup, ambaye pia ni Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), akifuatilia fainali hizo, kushoto kwake ni Diwani wa Kata ya Tongoni Mohammed Mwinyihaji (CUF).
Mashabiki wa timu ya Chuda FC yakishangilia kwa ushindi walioupata dhidi ya timu ya Jiwe FC baada ya kumalizika kwa fainali ya michunoa ya Haniu Cup Jijini Tanga.
Na Mwandishi wetu, Tanga
HATIMAYE timu ya Chuda FC ya Chumbageni Jijini Tanga, imetwaa ubingwa wa mashindano ya Haniu Cup, kwa kuichapa kwa mikwaju ya penati timu ya Jiwe FC yenye maskani yake Tanga Sisi.
Fainali hizo ambazo zilihudhuriwa na mamia ya wakazi wa Jiji la Tanga, zilikuwa za aina yake ambapo hadi kipyenga cha mwisho kinapulizwa timu hizo ziliweza kutoka sare ya bao 1-1.
Chuda, ilifanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati 4 kwa 1 hali iliyowafanya mashabiki wa timu hiyo kutoka na shangwe uwanjani.
Akizungumza katika mashindano hayo kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Tanga, Amina Mwidau (CUF), alisema ni muhimu kwa mkoa huo kuwa na kiwanja mbacho kitakuwa ni mahususi kwa ajili ya kuibua vipaji wa soka mkoani humo.
“Mimi kama Mbunge wetu wa Viti maalum na diwani wenu nina wajibu wa kusimamia kwa karibu shughuliza maendeleo ikiwemo kunua soka katika mkoa wetu huu wa Tanga. Mkoa huu ni chimbuko la michezo nchini na katika hili nitahakikisha ninawasilisha hoja katika kikao cha Jiji ili kuweza kijengwe kiwanja maalum ambacho.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Jamai hizi nyuzi za Timu za Soka ya Ulaya zitatugawa!

    Kwani hamuoni ni issue sana mfano mtu ni Liverpool halafu unaona uzi wa Arsenali?

    ReplyDelete
  2. CUF:

    Maendeleo Tanga yajali vipaumbele Afya kwanza halafu ndio Michezo,

    Watu wanajifungulia chini ya simenti ktk Zahanati kwa mirundikano Wodini, taa hakuna Wakunga wanatumia mwanga wa Nokia ya tochi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...