Dkt.  Mwele Malecela (pichani) ametunukiwa tuzo ya NTD Champion Award huko Washington Marekani kwa kazi yake  ya mapambano dhidi ya magonjwa yasiopewa kipaumbele. Dr Malecela alipewa tuzo hiyo katika hafla maalum iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo Maseneta na wawakilishi wa Congress. Sherehe hiyo maalum ilihudhuriwa pia  na mkuu wa USAID Dr Raj Shah. 
Akimtunkia tuzo hiyo Naibu Mkuu wa USAID anaeshughulikia Afya Dr Areil Pabloz-Mendez alisifia mchango mkubwa wa Dr Malecela kitaifa na kimataifa katika kupambana na magonjwa hayo. Wengine waliopewa tuzo ni Prof Ade Lucas wa Nigeria, Dr Amazigo wa Nigeria an Dr Birtwum wa Ghana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...