Si ingine bali ni Ngoma Africa band aka FFU,bendi ya muziki wa dansi
yenye makao yake kule Ujerumani.
Katika maonyesho ya kibiashara ya Afrika-Messe Trade fair kule mjini
Bremen,Ujerumani,bendi hiyo maarufu kwa kupelekana puta na washabiki
wake ilikutana na washabiki au wapenzi wa muziki walio gado katika
kuyarudi mangoma siku ya jumamosi 15.9.2012 mjini Bremen.
Ambako maonyesho hayo aliudhuriwa na maelfu ya watu,Ngoma Africa band
ndio walikuwa wakisubiriwa kwa hamu,walipanda jukwaani saa 11 alasiri
na kuanza kupeleka mashambulizi ya muziki kwa washabiki ambao waliupokea
mdundo kwa kila hali.
Wasikilize FFU katika kambi yao at www.ngoma-africa.com
wasiliana nao at contact@ngoma-africa.com
Kamanda wa FFU Ras Makunja akiongoza mashambulizi ya FFU
Ligwaride likiendelea Bremen
Gwaride jukwaani na dogo janja
Kikosi kizima cha FFU ughaibuni
wajamaa wanatisha,yaani wanatumia kila nafasi kuwakamua kisawa sawa ughabuni,kazeni buti ffu,mnakubalika
ReplyDeleteKimataifa
kazi ipo,naona ffu mmepania kushambulia kila kona
ReplyDeletekamanda ? ndio kusema umehamua kukinusha kila kona
ReplyDeletekamanda mkuu wa ffu,naona siku hizi umetulia sana,sikusikii vijembe vyako?
ReplyDeleteau unaowarushia vijembe wamekuziba mdomo kwa vijisenti?