Flaviana Matata ang’ara Wiki ya mitindo ya London
Imani Makongoro
MWANAMITINDO maarufu nchini, Flaviana Matata ameendelea kung’ara katika fani hiyo baada ya kung’ara katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya London, London Fashion Week.
Flaviana ambaye kwa sasa anaishi nchini Marekani kwa shughuli hizo za maonyesho mavazi, aliwavutia sana wadau wa maonyesho hayo na kumfanya mwanamuziki nyota wa kike duniani, Stefani Joanne Angelina Germanotta maarufu kwa jina la Lady Gaga.
Mwanamitindo huyo aliwasisimua wadau wengi wa mitindo wakiwemo watu maarufu duniniani na kuendelea kujizolea sifa na kutangaza jina lake na nchi yake pia.
Flaviana amekuwa akishiriki katika maonyesho hayo tangu mwaka 2010, hata hivyo mwaka huu ameonyesha kukomaa zaidi na kuweza kutawala jukwaa hilo.
Maonyesho ya mavazi ya mwaka huu yaliwahusisha wabunifu wengi maarufu wa mitindo ambapo mmoja wapo ni Vivenne Westwood Red Label ambaye anatamba duniani.
Pamoja na kuwepo kwa mbunifu huyo, mbunifu Philip Treacy naye alifanya mambo makubwa katika maonyesho hayo yaliyozinduliwa na Lady Gaga.
Flaviana alipewa heshima kubwa ya kuvaa jaketi la mwanamuziki aliyekuwa mfalme wa muziki wa aina ya Pop, marehemu Michael Jackson. Pia alivaa mavaz ya wabunifu maarufu kama Mike Fast na Christopher Raeburn.
Kutokana na jinsi alivyoweza kutamba katika maonyesho hayo, Flaviana alifanyiwa mahojiano na gazeti maarufu duniani la Marekani, Wall Street Journal.
Flaviana ambaye ni Miss Universe Tanzania wa mwaka 2007, aliweza kuipromoti nchi yake katika maonyesho hayo kama alivyofanya katika mashindano ya Miss Universe ya mwaka 2007 kwa kushika nafasi ya sita kati ya warembo 10 walioingia fainali. Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications, Maria Sarungi Tsehai alisema kuwa anajisikia faraja kubwa kuona Flaviana anaendelea kufanya vyema katika fani hiyo.
Hongera sana Flavy.
ReplyDeletesafi
ReplyDeleteBig Up, endelea na kazi hiyo, na Mungu akutie Nguvu.
ReplyDeleteBINTI HUYU NI MREMBO. HAITAJI WIGI WALA MKOROGO. GOD BLESS YOU FLAVIANA
ReplyDeleteHuyu ndio STAR wa ukweli sio hao waonyesha makalio wakina WEMA na MWENZIE AUNT EZEKIEL, Hao wanaojiita MASTAA bongo mie kwa mtazamo wangu tuwaite WATU MAHARUFU maana hata kibaka au kahaba anaweza kuwa MAHARUFU. Naikumbukwe kuna vitu vitatu 1.STAR2.MASHUHURI 3.MAHARUFU sasa kina WEMA nawenzie wote wa bongo movie ni maharufu tu!Watu mashuuri ni wazee wetu walioiongoza Nchi kwa uadilifu na MASTAA ndo hao kina flaviana, Michael jackson, Naomi Cambell nafikiri nimesomeka.Kina Wema ni maarufu tu maana hata Nguchiro anaweza kuwa maarufu kukamata kuku!
ReplyDeleteFainali wakifikia kama Bi Kidude
ReplyDeleteMtoto Flaviana ni mtamu kwa vile hana misala na maskendo ya ajabu ajabu,
ReplyDeleteNi mfano bora wa kuigwa na wasichana!!!
Kwa nini ktk Kambi za Warembo wanaojiandaa kwa mashindano Kamati ya REDDS MISS TANZANIA isiwe inaalika kutoa mwongozo kwa washindani ,kuwalika wasichana waliopita wenye mafanikio na mwenendo mwema kama huyu ?